Mganga mkuu wa Mkoa wa Pwani
,Yudas Ndungile akitoa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa mmoja
wa wanafunzi, wakati wa uzinduzi wa zoezi ya chanjo hiyo kwa watoto wenye umri
wa miaka 14 ,kimkoa yaliyofanyika kituo cha afya mkoani,Kibaha.
..........................
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
JUMLA ya akinamama 20,815 waliofanyiwa uchunguzi wa
saratani ya mlango wa shingo ya kizazi mkoani Pwani katika kipindi cha miaka
mitatu kati yao
530 walikutwa na dalili za awali za saratani hiyo,ambapo watatu walifariki.
Aidha kati ya akinamama hao waliofanyiwa uchunguzi
akinamama 412 walitibiwa matibabu na 115 walipata rufaa ya kwenda
Oceanroad na hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Akitoa takwimu hizo ,wakati wa uzinduzi wa zoezi la
chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa shingo ya kizazi kwa watoto wenye umri
wa miaka 14 ,kimkoa yaliyofanyika kituo cha afya mkoani,Kibaha,mganga mkuu wa
Mkoa wa Pwani ,Yudas Ndungile alisema , ipo changamoto ya kutojua idadi ya vifo
kamili kwa kuwa wengi hupata rufaa.
Pamoja na hayo ,alisema ipo haja ya kuona ukubwa wa
tatizo hilo kwa
kuangalia afya mapema na watoto wa mashuleni kupata chanjo.
Ndungile alisema jumla ya watoto wa kike 18,823
waliopo shule na nje ya shule mkoani hapo watapatiwa chanjo ya kukinga saratani
ya mlango wa kizazi mwaka huu.
Alielezea, tayari wameshapokea chanjo na wataanza
kuzitoa katika vituo mbalimbali vya huduma.
Ndungile aliitoa shaka jamii kuwa chanjo ya kukinga
saratani ya mlango wa kizazi ni salama ,haina madhara na haiathiri uwezo wa
binti kupata watoto hapo baadae
” Serikali imethibitisha usalama wa umadhubuti wa
chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi ndiyo maana imeiongeza kwenye
mpango wa Taifa wa chanjo ili iweze kusaidia kudhibiti tatizo hilo kwa akinamama”:!
Ndungile alieleza mwaka 2018 chanjo itatolewa kwa
wasichana waliofikisha umri wa miaka 14 na ili kupata kinga kamili walengwa
watahitaji kupatiwa dozi mbili.
Alisisitiza chanjo hiyo huwakinga wasichana wasipate
saratani ya mlango wa kizazi pindi wawapo watu wazima wakiwa na familia zao.
“Nchini Tanzania saratani ya mlango wa
kizazi ni ya kwanza kwa vifo ikifuatiwa na saratani ya matiti ” Saratani hizi
mbili kwa pamoja husababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya wakinamama
vitokanavyo na saratani”alibainisha Ndungile.
Kwa upande wake ,Mganga mkuu wa halmashauri ya Mji
wa Kibaha ,Dkt.Tulitweni Mwinuka alisema ,wamezindua chanjo hiyo kwa wasichana
wenye umri wa miaka 14.
Alielezea ,kiwilaya wamezindua chanjo hiyo kwa
wasichana 100 kituoni hapo na wanatarajia kufanikisha na kuleta matokeo
kutokana na chanjo hiyo .
Akizindua zoezi hilo ,kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa
Pwani,mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama aliwataka wanafunzi wa kike
kuacha kujiiingiza kwenye vitendo vya ngono mapema ili kujiepusha kuingia
kwenye hatari ya kupata magonjwa ya zinaa,ukimwi na hata saratani ya mlango wa
kizazi.
Alisema moja ya sababu zinazosababisha saratani hiyo
ni kuwa na wanaume wengi ,kuvuta sigara ,wenye mitala, na kuanza mapema kufanya
ngono.
“Acheni kujiingiza kwenye mapenzi mapema ni hatari
katika maisha yenu, ukivua sketi ,na mwanaume akavua suruali jua kuna hatari ya
kuhatarisha maisha yako kwa magonjwa yanayosababishwa kutokana na ngono”
“Jizuieni hadi hapo mtakapoolewa ,msikimbilie ngono
za haraka,mtapata saratani”: alisisitiza Mshama.
Mshama aliwahimiza wazazi na walezi kuwapeleka
watoto wao wa kike wenye umri wa miaka 14 kupata chanjo hiyo kwani haina
madhara.
No comments:
Post a Comment