Malkia wa nguvu 2018 Teddy Davis kutoka Bagamoyo akionyesha tuzo yake ya Malkia wa nguvu katika Ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, TaSUBa.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga akizungumza wakati wa hafla za kumtangaza Malkia wa nguvu 2018 iliyofanyika Ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, TaSUBa.
........................................
Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga amewataka wanawake kushirikiana ili
kujiletea maendeleo kupitia vikundi vya ujasiliamali.
Majid
aliyasema hayo wakati wa sherehe za kumtangaza Malkia wa Nguvu 2018 Teddy Davis
ambae ametoka wilayani Bagamoyo.
Alisema
ushindi wa Teddy kuwa Malkia wa nguvu ni
wazi kuwa wanawake wakifanya juhudi wananweza kufanikiwa hivyo ni vyema wakawa
na ushirikiano ili kuonyeshana njia.
Aliongeza
kwa kusema kuwa, Halmashauri za Bagamoyo na Chalinze zinatenga asilimia tano
kwa wanawake na vijana ili waweze kujikwamua kiuchumi kupitia vikundi vyao.
Aidha,
Mkuu huyo wa wilaya alisema Serikali ya wilaya Bagamoyo itashirikiana na
wanawake wote wilayani humo wenye kuonyesha nia ya kujikwamua kiuchumi kwa
kujishughulisha na mambo mbalimbali ya uzalishai mali kupitia vikundi vyao.
Nae
katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Bagamoyo, John Francis (Bolizozo) alisema
wanawake wanapaswa kuiwekea malengo ya maendeleo kwakuwa wao ndio dira ya
familia.
Alisema
kuna baadhi ya wanawake waba tabia ya kujiuza miili yao hivyo aliwataka kuacha tabia hiyo na
badala yake wafanye shughuli zitakazowaingizia kipato kwa njia ya halali.
Aliongeza
kwa kusema kuwa ili mwanamke awe na thamani katika jamii na kuweza kupata
msaada wa kitaalamu anapaswa kwanza kujiheshimu yeye mwenyewe na kujitambua
thamani yake.
Bolizozo
alikemea tabia ya wanawake wanaovaa mavazi ya kujidhalilisha pamoja vijana
wakiume ambao huiga tamaduni zisizo na maadili.
Alimpongeza
Teddy pamoa na ukwaa zima la uwezeshai wanawake Bagamoyo kwa kuikita katika
shughuli za kujiletea maendeleo na kuongeza kuwa hayo ndio matunda ya CCM.
Kwa
upande wake Mshindi wa Malkia wa Nguvu 2018 Teddy Davis alisema anaishukuru
serikali ya wilaya ya Bagamoyo kwa kumuunga mkono yeye na wanawake wenzie
katika shughuli za uasiliamali.
Teddy
ambae ni Mwenyekiti wa Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi wilayani Bagamoyo
aliwashukuru watu wote waliompigia kura ili kupata nafasi hiyo ambayo
hakuitarajia.
Jukwaa
analoliongoza la uwezeshaji wanawake kiuchumi ni agizo la makamo wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
la kuundwa kwa Majukwaa hayo nchi nzima ili wanawake wapate fursa za kujiajiri
na kujiwezesha kiuchumi.
Teddy
ni mjasiliamali anaejishghulisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zitokanazo
na Lozela huku akiwaonyesha wanawake wenzie fursa za kujikwamua kiuchumi
kupitia bidhaa za kutengeneza kwa mikono na ubunifu wa aina mbalimbali.
Akizungumzia
namna ya mchakato wa kumpata Malkia wa nguvu, Muwakilishi kutoka Clouds Media Group,
Amani Maltin ambao ndio waandaai wa shindano la Malkia wa nguvu alisema kura
zimepigwa kutoka kwa wasikilizaji wa Clouds fm na Clouds tv ambapo majina ya
washiriki yalitoka nchi nzima.
Maltin
Alisema miongoni mwa sifa za kumpata Malkia wa nguvu ni pamoja na
kujishughulisha kwake na mambo ya kimaendeleo yeye wenyewe pamoja na
kushirikiana na wanawake wenzie sehemu anayoishi na ni kwa jinsi gani
anakubalika katika jamii.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga pamoa na kamati ya ulinzi na Usalama wakipiga makofi kumkaribisha Malkia wa nguvu wakati akiingia ukumbini.
Mshindi wa Malkia wa Nguvu 2018 Teddy Davis akiingia Ukumbini.
Mshindi wa Malkia wa Nguvu 2018 Teddy Davis akizungumza katika sherehe hizo.
Diwani
wa Kata ya Dunda, Dckson Makamba akimkaribisha Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ili kuzungumza katika sherehe hiyo.
Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Bagamoyo, John Francis (Bolizozo) akizungumza katika sherehe hiyo.
Mshindi wa Malkia wa Nguvu 2018 Teddy Davis akikata keki katika sherehe hizo.
Mshindi wa Malkia wa Nguvu 2018 Teddy Davis akimlisha keki mama yake mzazi, kulia na kushoto ni watoto wake.
Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Bagamoyo, John Francis (Bolizozo)kimlisha keki Malkia wa nguvu 2018, Teddy Davis.
Malkia wa nguvu 2018, Teddy Davis, akimkabidhi zawadi ya kanzu kofia na tasbih Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga.
Picha
ya pamoja Mgeni rasmi, Malkia wanguvu, Kamati ya ulinzi na usalama na viongozi
wengine waandamizi pamoja na watoto wa Malkia wa nguvu waliochuchumaa chini na
Katibu mwenezi wa CCM wilaya Bolizozo.
No comments:
Post a Comment