Mkurugenzi wa Kampuni ya Highland Estates
Limited akizungumza kwenye mkutno kijiji cha Lulenge na kutoa ahadi ya Vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 10.
.......................................................
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Highland Estates Limited, Naweed Mulla, amechangia vifaa vya
ujenzi vyenye thamanai ya shilingi milioni 10 kwaajili ya ujenzi wa zahanati ya
kijiji cha Lulenge kata ya Lugoba.
Naweed
ametoa ahadi hiyo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga katika
Mkutano wa kijiji cha Lulenge ambapo Mkuu wa wilaya alifika kuweka jiwe la
Msingi ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Lulenge.
Awali
akizungumza katikaa Mkutano huo, Diwani wa kata ya Ubena Nicholaus Mluwa alisema kijiji cha Lulenge
kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa Zahanati hivyo wananchi huttembea
umbali mrefu kufuata huduma ya Afya.
Alisema
makundi yanayopata shida katika kutafuta huduma ya Afya ni kina mama na watoto
ambapo kijiji hicho kingekuwa na zahanati kero ingewaondoka.
Kufuatia
hali hiyo Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo alitoa wazo la uanzishwaji wa ujenzi
kwaajili ya Zahanati na kuwataka wananchi kuchangia ili Serikali kupia
Halmashauri ya Chalinze iweze kuongeza nguvu pale watakapoishia.
Mkuu
wa wilaya alimuagiza Mwenyekiti wa kijiji hicho kuitisha mkutano na wenyeviti
wa vitongoi ili kuangalia uwezekano wa kuanza ujenzi huku wakitakiwa kuchangia
vifaa, nguvukazi na fedha kufanikisha ujenzi huo
Kutokana
na hali hiyo Mkurugenzi wa Highland Estates Limited Naweed Mulla meahidi kutoa
vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 10 ikiwa ni sehemu ya
mchango wake kama muwekezaji katika kata hiyo
ya Ubena.
Diwani
wa kata ya Ubena Nicholaus Mluwa alimshukuru muwekezaji huyo kwa misaada
mbalimbli anayotoa kwenye kata hiyo.
Mluwa
alisema Naweed amekuwa akijitolea mambo mbalimbali ya kimaendeleo ndani ya kata
hiyo ikiwemo kuchonga barabara za vijiji vya kata hiyo na mengineo
Aidha,
Diwani Mluwa aliwataka ananchi wake kumpa ushirikiano muwekezaji huyo na kutoa
wito kwa wawekezaji wa kata hiyo kujitokeza katika kuchangia miradi ya
maendeleo ambayo faida yake inarudi kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mh. Alhaj, Maid Mwanga akizungumza katika kijiji cha Lulenge.
No comments:
Post a Comment