Wanafunzi
kidato cha sita 2018 Sekondari ya Bagamoyo wakiingia Ukumbini kwa mtindo huu
siku ya Mahafali ya 16.
Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo Alhaj, Majid Mwanga akizungumza wakati wa mahafali ya 16
ya kidato cha sita 2018.
..........................
Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga amesema serikali inafanya juhudi ya
kuinua kiwango cha ufaulu shuleni hivyo
walimu, wanafunzi na wazazi wanapaswa kuunga mkono juhudi za serikali
ili kufanikisha malengo hayo.
Hayo
aliyasema alipokuwa akizungumza katika mahafali ya 16 ya kidato cha sita shule
ya sekondari Bagamoyo
Alisema
kila mmoja anatakiwa kutambua maukumu yake katika kufanikisha malengo ambapo
serikali tayari inatekeleza majukumu yake ya kuingiza fedha za elimu bure
shuleni pamoja na kuajiri walimu wa kutosha wa masomo mbalimbali.
Aliongeza
kwa kusema kuwa kufuatia sera ya elimu bure shule ya sekondari Bagamoyo
imepokea zaidi ya milioni mia mbili katika kipindi cha miezi sita ambapo ndani
yake zipo fedha za ukarabati ili kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi.
Mkuu
wa shule hiyo Khalfani Milongo alisema shule hiyo imejipanga katika kuwajengea
uwezo wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuwapa mitihani ya majaribio ya mara kwa
mara .
Aidha
alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mmomomonyoko wa
maadili unaosababishwa na utandawazi.
Alisema
wanafunzi wamekuwa wakiiga tabia ambazo hazina maadili kutokana na kumiliki
simu ambapo wanaweza kuona vitu mbalimbali kwenye mitandao vinavyowashawishi
mambo yasiyofaa.
Jumla
ya wanafunzi 328 wametunukiwa vyeti vya kuhitimu kidato cha sita 2018 ambapo
wote ni wavulana.
Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo, Alha, Majid Mwanga na Mwenyekiti wa Bodi ya shule
sekondari ya Bagamoyo, wakiangalia jarida ambalo limeanzishwa kwa ubunifu wa
wanafunzi wa sekondari ya Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment