Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza wakati alipofungua Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA) kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma Machi 31, 2018
..........................................
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini popote walipo wahakikishe
wanaipigania na kuilinda amani kwa kila hali ikiwa ni pamoja na kupambana na
viashiria vya uvunjifu wa amani.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Machi 31, 2018) kwenye Mkutano Mkuu wa
BAKWATA uliofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma,
ambapo amesisitiza kuwa ni muhimu wasaidizi wa Mufti wakasimamia suala hilo.
“Dini
ni taasisi muhimu sana
kwa maisha yetu ya kila siku ndio maana Serikali inaheshimu na kuzitambua dini
zote kutokana na mchango wake mkubwa katika amani ya nchi yetu. Niwaombe
viongozi wangu popote mlipo muilinde amani yetu”
Waziri
Mkuu amesema amani ni miongoni mwa neema kubwa sana kwa binadamu na ndio maana wote
wanamtambua Mwenyezi Mungu, hivyo wasiruhusu mtu au kikundi chochote kujaribu
kuchafua na kuharibu amani iliyopo nchini.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amewasisitiza viongozi Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA) wahakikishe kuwa chombo hicho kinaendelea kuwaunganisha
waislamu bila ya kujali makabila yao, rangi zao
au madhehebu yao.
Waziri
Mkuu amesema Mufti wa Tanzania
Sheikh Aboubakar bin Zubeiry ambaye ndiye kiongozi wa Waislamu nchini mara zote
amekuwa akisisitiza jambo hilo
na kuwataka waislamu popote walipo watambue kuwa hicho ni chombo chao.
“Ni
muhimu sana kwa
ninyi wasaidizi wa Mufti mlio kusanyika hapa muhakikishe mnalisimamia hili
katika maeneo yenu. Katika hili napenda kuwahakikishia kuwa Serikali yenu iko
pamoja Mheshimiwa Mufti kutekeleza nia hiyo njema.”
Amesema
ahadi ya Rais Dkt. Magufuli ni kuwa Serikali anayoiongoza ipo tayari kusikiliza
maoni, ushauri na mapendekezo yeyote kutoka kwa viongozi wa dini .
‘Milango iko wazi saa zote ‘
Ameongeza
kuwa yeye si mtaalamu sana kama
walivyo Masheikh hao lakini anakumbuka maneno ya Mwenyezi Mungu ndani ya
Qur’ani sura Al Imran aya ya 103 yanayosema “ Shikamaneni na kamba ya Mwenyezi
Mungu nyote na wala msifarakane”
Mkutano
huo umehudhuriwa na Sheikh Mkuu wa Mufti wa Tanzania Sheikh Zubeir,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, wajumbe wa Baraza la Ulamaa, Masheikh na
viongozi wa BAKWATA wa mikoa na wilaya zote Tanzania.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania,
Abubakary Zubeiry wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma kufungua mkutano
wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Machi 31, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA) baada ya kufungua mkutano wao kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma, Machi 31, 2018.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
No comments:
Post a Comment