Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya
Bagamoyo Aboubakary Mlawa kushoto akimkabidhi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno, fedha taslimu pamoja vifaa vya ujenzi kwajili ya shule ya msingi Voda iliyopo kata ya Mbwewe Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo.
..............................
Jumuiya
ya wazazi wa CCM wilaya ya Bagamoyo imeadhimisha sherehe za wazazi kwa
kujitolea Damu katika kituo cha Afya Lugoba Halmashauri ya Chalinze pamoja na
kutoa msaada wa vifaa vya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Voda
iliyopo kata ya Mbwewe.
Akizungumza
katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Bagamoyo
Aboubakary Mlawa amesema wameamua kuadhimisha sherehe hizo katika kufanya
shughuli zenye kuleta tija kwa jamii ikiwa ni pamoja kutoa damu ili kuunga
mkono juhudi za kuchaangia damu salama ambazo zitawasaidia wananchi wenye
uhitaji.
Aidha,
Mlawa alisema pamoja na hilo
maadhimisha hayo yanakwenda sambamba na wiki ya upandaji miti kitaifa ambapo
jumuiya hiyo imeweza kupanda miti kadhaa katika kituo cha Afya Lugoba.
Wakati
huohuo Jumuiya wazazi wa CCM wilaya ya Bagamoyo wameweza kutoa msaada wa vifaa
vya ujenzi katika shule ya msingi Voda iliyopo kata ya Mbwewe Halmashauri ya
Chalinze.
Alisema
miongoni mwa vifaa hivyo vya ujenzi walivyovitoa na kumkabidhi Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Pwani Ramadani Maneno ni pamoa na Saruji mifuko 50, Mabati 100, na
Matofali 200.
Alisema
Elimu ni kitu muhimu katika jamii hivyo kila mmoja anapaswa kuchangia katika
elimu ili kuunga mkono juhudi za serikali ya Chama cha Mapinduzi ambayo imekuja
na sera ya elimu bure kwa watu wote.
Alisema,
serikali haiwezi kutekeleza mambo ya maendeleo bila wananchi kutoa ushirikiano
hivyo alimuomba Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani kuwahamasisha wazazi,
wananchama wa CCM na wananchi kwa ujumla kuchangia mambo mbalimbali ya elimu
ili watoto wapate elimu bora
Aliongeza
kwa kusema kuwa Jumuiya ya wazazi ni kioo katika jamii hivyo imeanza kuonyesha
njia na wengine wafuate na hatimae kufikia lengo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa pwani Ramadhani Maneno amemtaka Mtendaji
kata wa Mbwewe kuwa na mahusiano mazuri na wananchi ili ajue ni changamoto gani
zinazowakabili kushindwa kuwapeleka watoto shule ili kuongeza idadi ya
wananfunzi katika shule hiyo.
Alisema
viongozi katika kila ngazi wanapaswa kuwa karibu na wananchi ili kutoa
suhirikiano wa mambo mbalimbali hata yale yanayohusu maendeleo ya kijamii.
Mwenyekiti
huyo wa CCM Mkoa wa Pwani alisema viongozi wa CCM kazi yao ni kuhakikisha ilani ya chama hicho
inatekelezwa ipasavyo ili kuondoa kero mbalimbali za wananchi.
Kauli
mbiu ya maadhimisho ya jumuiya ya wazazi ni
WAZAZI
TUKO IMARA KUSIMAMIA MAADILI MEMA YA TAIFA LETU.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno, akizungumza katika shule ya msingi Voda kata ya Mbwewe Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Bagamoyo Aboubakary Mlawa akitoa damu katika kituo cha Afya Lugoba ili kuunga mkono mpango wa taifa wa kuchangia damu salama.
Katibu wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Bagamoyo, Aeshi Rajabu, akitoa damu katika kituo cha Afya Lugoba ili kuunga mkono mpango wa taifa wa kuchangia damu salama.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Saidi Zikatimu, akitoa damu katika kituo cha Afya Lugoba ili kuunga mkono mpango wa taifa wa kuchangia damu salama.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Bagamoyo Aboubakary Mlawa (kushoto) Katibu wa CCM wilaya ya Bagamoyo (katikati) Kombo Kamote, na Kulia ni Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Bagamoyo, John Francis(Bolizozo)
No comments:
Post a Comment