Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Rais wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Jeremy Aguma wa pili kutoka kulia
wakivuta utepe kwenye jiwe la msingi kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma
katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika
kiwango cha lami. Sherehe hizo za ufunguzi zilifanyika katika kijiji cha
Ndolela kilichopo Isimani nje kidogo ya mji wa Iringa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Rais wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Jeremy Aguma, Balozi wa Japan Masaharu
Yoshida wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma katika
sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha
lami. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Waziri wa
Ujenzi Profesa Makame Mbarawa , Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na viongozi
wengine wa Serikali na wageni kutoka nje ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika
sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya
Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara
baada ya kuwasili Isimani Mkoani Iringa.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli
akiwa jukwaa kuu pamoja na Balozi wa Japan Masaharu Yoshida, Waziri wa
Ardhi Wiliam Lukuvi, pamoja na Waziri wa Mambo ya nje Balozi Dkt. Augustine
Mahiga wakifatilia sherehe za ufunguzi wa barabara ya ya Iringa-Dodoma katika
sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha
lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Iringa
mjini waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili akitokea Isimani mkoani Iringa.
PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment