Monday, April 16, 2018

FEDHA ZA ELIMU BURE WANANCHI WAZIJUE.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhaj, Majid Mwanga amewaagiza maafisa Elimu kata wilayani Bagamoyo kutoa taarifa za fedha za Elimu bure wanazopokea kila kata.

Mwanga aliyasema hayo kwa nyakati tofauti katika ziara yake ya kuweka mawe ya msingi miradi ya maendeleo Halmashauri ya Chalinze na Bagamoyo.

Alisema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imetangaza elimu bure ambapo kila shule inapewa fedha za kuwezesha mpango huo wa elimu bure.

Aliongeza kwa kusema kuwa wananchi hawaui kama serikali inagharamia elimu hivyo ni vyema fedha hizo zikawa wazi kwa kila mwananchi na matumizi yake yabanishwe kwenye vikao vya Halamashauri za vijiji.

Aliwataka Maafisa Elimu kata kutoa tarifa kwenye vikao vya kata ili kujua kila kata imepokea kiasi gani huku fedha zilizotengwa kwaajili ya ukarabati zikztumika kama ilivykusudiwa na wananchi wapewe taarifa juu ya fedha hizo.

Alisema serikli inatumia fedha nyingi katika kuwezesha elimu bure ambapo alitolea mfano wa kata ya Lugoba iliyopokea milioni 200 katika kipindi cha Oktoba 2017 hadi Machi 2018 na kwamba kila kata imepewa fedha hizo kulingna na mahitaji yake.

Aidha, aliwaonya wakuu wa shule wanaoendelea kuchangisha fedha katika shule zao kwamba wakibainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwa kukiuka agizo la Rais la kufuta michango ya aina zote.

Alisema wananchi wanayo nafasi ya kuchangia katika elimu lakini michango hiyo ni lazima ipate kibali cha Mkuu wa Mkoa na kwamba Mwalimu hatakiwi kujisisha na aina yoyote ya mchango na badala yake Bodi na kamati za shule zihusike kukusanya michango hiyo na kusimamia matumizi yake wao wenyewe bila ya kungiliwa na walimu.

Mkuu huyo wa wilaya alisisitiza fedha za ukarabati zitumike vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa kwa kubadilisha mandhari ya majengo ili wanafanzi wapate ari ya kupenda kusoma.

Katika ziara hiyo aliweza kuweka mawe ya msingi ujenzi wa madara katika shule za Kiwangw, Vigwaza, Msoga, Msata Miono na Ubena ambapo katika kata hizo zipo shule mpya zilizoanzishwa kutokana na hamasa yake na kupelekea shule moja inayojengwa kata ya Ubena kupewa jina la MAJID MWANGA.

 
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhaj, Majid Mwanga(kulia) akikagua ujenzi wa vyumba viwili vya maabara na chumba kimoja cha maktaba katika shule ya Sekondari Mboga iliyopo kata ya Msoga Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo, picha ya juu ni muonekano wa jengo hilo.
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhaj, Majid Mwanga akikagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule mpya inayoanzishwa kijiji cha Diozile kata ya Msoga Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo, Picha ya juu Mkuu wa wilaya akiongea na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho waliofika kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi wa shule hiyo.
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhaj, Majid Mwanga akiweka jiwe la msingi ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule mpya inayoanzishwa kijiji cha Diozile kata ya Msoga Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo, Picha ya juu Mkuu wa wilaya akiongea na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho waliofika kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi wa shule hiyo.
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhaj, Majid Mwanga akiweka jiwe la msingi ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Vigwaza Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo.

 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhaj, Majid Mwanga akizungumza na wananfunzi wa shule ya Msingi Lulenge iliyopo kata ya Ubena Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo.

No comments:

Post a Comment