Posts

MEYA MANISPAA YA KIBAHA AWATAKA WAZAZI KUIMARISHA NA KUBORESHA ELIMU KWA KUSHIRIKIANA NA WALIMU

Image
  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dr Nicas Mawazo amewataka wazazi wa Shule zilizopo Manispaa ya Kibaha kuiga  jitihada zinazofanywa na Shule zingine katika kuimarisha na kuboresha elimu kwenye Shule zao kwa kushirikiana na walimu. Hayo ameyasema wakati wa kikao na Kamati ya Shule ya Sekondari ya Mwambisi, iliyofika katika Ofisi ya Mstahiki Meya kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali. Akizungumza baada ya Kamati hiyo kuwasilisha mapendekezo yao, Mstahiki Meya Dr Nicas ameipongeza Kamati hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha wanafunzi wa Shule yaSekondari Mwambisi wanaendelea kufanya vizuri kwenye mitihani yao. "Nawapongeza sana Kamati ya Shule kwa jitihada kubwa mnazofanya , Shule zingine wangekuwa wanafuata utaratibu huu ina maana tungekuwa tunafanya vizuri zaidi  na zipo baadhi ya Shule zinafanya hivyo na matokeo yao yanakuwa ni mazuri," amesema Dr Nicas. Ameongeza kuwa,, Ofisi ya Mstahiki Meya itaongezea hela ya ununuzi wa mashine ya P...

MAONESHO YA MADINI YAIPAISHA LINDI KIMAPATO - MAKUSANYO YAFIKIA BILIONI 10.5

Image
  MAONESHO YA MADINI YAIPAISHA LINDI KIMAPATO - MAKUSANYO YAFIKIA BILIONI 10.5 Na Hadija omary  LINDI. Mkoa wa Lindi umeandikisha mafanikio makubwa katika Sekta ya Madini baada ya makusanyo ya maduhuli ya Serikali kuongezeka kwa zaidi ya mara nne ndani ya kipindi cha miaka sita. Hayo yamebainishwa na Afisa Madini Mkoa wa Lindi, Mhandisi Emmanuel Shija, alipozungumza kuhusu mwenendo wa sekta hiyo na maandalizi ya Maonesho Makubwa ya Kimataifa ya Madini yanayotarajiwa kufanyika Wilayani Ruangwa. Mhandisi Shija amesema kuwa kwa miaka sita iliyopita, Mkoa wa Lindi ulikuwa unakusanya maduhuli ya wastani wa Shilingi Bilioni 2.5 pekee, lakini katika mwaka wa fedha wa 2025/2026, makusanyo hayo yamepanda hadi kufikia takribani Bilioni 10.5. "Mkoa wetu wa Lindi ulikuwa unakusanya maduhuli ya Serikali Bilioni 2.5 lakini mpaka kufika mwaka uliopita wa fedha Mkoa wetu wa Lindi umeweza kukusanya Bilioni takribani 10.5," amesema Mhandisi Shija. Ameeleza kuwa ongezeko hilo linatokana na ukua...

MAGAZETI YA TANZANIA LEO TAREHE 04 SEPTEMBA 2026

Image
 

MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA.

Image
  MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya utoaji wa tuzo za 19 za Rais za Wazalishaji Bora Viwandani, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam.   Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu wa Rais ametoa wito kwa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na wazalishaji wa saruji nchini, kuhakikisha wanatafuta suluhu ya haraka ili kurejesha bei ya kawaida ya saruji kwa wananchi. Amesema maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona wananchi wanaweza kununua mfuko wa saruji kwa gharama nafuu hivyo ni lazima kuoanisha uzalishaji wa malighafi zote zinazochangia katika uzalishaji wa saruji ili bidhaa hiyo ipatikane kwa urahisi.   Halikadhalika, Makamu wa Rais amesema ni muhimu kufanya tathimini ya ukuaji wa viwanda hapa ...