MEYA MANISPAA YA KIBAHA AWATAKA WAZAZI KUIMARISHA NA KUBORESHA ELIMU KWA KUSHIRIKIANA NA WALIMU
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dr Nicas Mawazo amewataka wazazi wa Shule zilizopo Manispaa ya Kibaha kuiga jitihada zinazofanywa na Shule zingine katika kuimarisha na kuboresha elimu kwenye Shule zao kwa kushirikiana na walimu. Hayo ameyasema wakati wa kikao na Kamati ya Shule ya Sekondari ya Mwambisi, iliyofika katika Ofisi ya Mstahiki Meya kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali. Akizungumza baada ya Kamati hiyo kuwasilisha mapendekezo yao, Mstahiki Meya Dr Nicas ameipongeza Kamati hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha wanafunzi wa Shule yaSekondari Mwambisi wanaendelea kufanya vizuri kwenye mitihani yao. "Nawapongeza sana Kamati ya Shule kwa jitihada kubwa mnazofanya , Shule zingine wangekuwa wanafuata utaratibu huu ina maana tungekuwa tunafanya vizuri zaidi na zipo baadhi ya Shule zinafanya hivyo na matokeo yao yanakuwa ni mazuri," amesema Dr Nicas. Ameongeza kuwa,, Ofisi ya Mstahiki Meya itaongezea hela ya ununuzi wa mashine ya P...