TANROADS YATANGA BARABARA SITA ZA PPP KUUNGANISHA MIKOA YA DAR, PWANI, DODOMA, SINGIDA NA TANGA KM 969
Katika hatua nyingine kubwa ya kuharakisha maendeleo ya miundombinu na kuimarisha ukuaji wa uchumi wa Taifa, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) umetangaza fursa za uwekezaji katika miradi sita mikubwa ya barabara yenye urefu wa kilomita 969 kupitia mfumo wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP). Tangazo hilo la kimataifa la kutafuta wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kubuni, kujenga, kugharamia, kuendesha, kutunza na hatimaye kukabidhi miradi hiyo kwa Serikali kupitia mfumo wa Design, Build, Finance, Operate, Maintain and Transfer (DBFOMT), linaendelea kudhihirisha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutumia nguvu ya sekta binafsi kuharakisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo. Hatua hiyo pia inaakisi mafanikio ya mageuzi makubwa yanayosimamiwa na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) chini ya Mkurugenzi Mtendaji David Kafulila, ambaye amekuwa mstari wa mbe...