Posts

TANROADS YATANGA BARABARA SITA ZA PPP KUUNGANISHA MIKOA YA DAR, PWANI, DODOMA, SINGIDA NA TANGA KM 969

Image
  Katika hatua nyingine kubwa ya kuharakisha maendeleo ya miundombinu na kuimarisha ukuaji wa uchumi wa Taifa, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) umetangaza fursa za uwekezaji katika miradi sita mikubwa ya barabara yenye urefu wa kilomita 969 kupitia mfumo wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).   Tangazo hilo la kimataifa la kutafuta wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kubuni, kujenga, kugharamia, kuendesha, kutunza na hatimaye kukabidhi miradi hiyo kwa Serikali kupitia mfumo wa Design, Build, Finance, Operate, Maintain and Transfer (DBFOMT), linaendelea kudhihirisha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutumia nguvu ya sekta binafsi kuharakisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.   Hatua hiyo pia inaakisi mafanikio ya mageuzi makubwa yanayosimamiwa na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) chini ya Mkurugenzi Mtendaji David Kafulila, ambaye amekuwa mstari wa mbe...

TWPF YAKAGUA ENEO LAKE LA KIMKAKATI DODOMA

Image
    Na Oscar Mbuza, MNRT   BODI ya Mfuko wa Kuhifadhi Wanyawapori (TWPF) imetembelea kiwanja kinachomilikiwa na Mfuko huo   eneo la Njedengwa katika Manispaa ya Dodoma ambacho kitapangiwa matumizi yake hivi karibuni.   Msafara wa Bodi hiyo umeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TWPF Profesa Jafari Kideghesho akiambatana na   Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Alexander Lobora na baadhi ya wajumbe wa Bodi.   Wajumbe wengine ambao wameshiriki   ziara hiyo ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Dkt. Eblate Mjingo na   Kamishna wa Uhifadhi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mlage Kabange.   Aidha ujumbe huo pia ulimjumuisha   Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCCA), Victoria Shayo aliyemwakilisha Kamisha wa Uhifadhi wa NCCA.   Akizungumza baada ya kukagua eneo hilo lil...

KATAMBI AWAONYA WAHALIFU NA MAANDAMANO HARAMU YA TAREHE 07

Image
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amewaasa watu wanaotoa kauli za kichochezi katika mitandao ya kijamii, majukwaa ya kisiasa na maeneo mbalimbali ambapo kauli hizo za kibaguzi na kichochezi zinahusu Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Viongozi mbalimbali wa serikali au wa dini.   Waziri Katambi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waumini wa Msikiti wa Mukadam uliopo Kata ya Chang’ombe iliyopo wilaya ya Dodoma Mjini ambapo kumefanyika Mashindano ya Quran na Harambee ya Ujenzi wa Msikiti huo.   “Taifa hili limejengwa kwa maumivu makubwa ya waasisi, limejengwa kwa jasho na hata damu ilipobidi ili Taifa Tanzania liwepo, nitumie fursa hii kuwaomba sana na kuwaasa wale wote ambao wanatumia majukwaa ya kisiasa kuchonganisha wananchi, kuwajaza chuki, kuchochea lakini pia kuhamasisha kufanya uhalifu na wanaounda magenge ya uhalifu yanayolenga kuharibu taifa letu, niwasihi na kuwaomba waache mara moja kwasababu kufanya hivyo hakuna ambae at...

VIONGOZI WA REA ZAMBIA, WAWASILI TANZANIA KWA ZIARA YA KIKAZI

Image
  Viongozi wa Mamlaka ya Nishati Vijijini (REA) kutoka nchini Zambia wamewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kujifunza na kubadilishana ujuzi na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).   REA Zambia ambao wameongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Zambia anayeshughulikia Umeme, Mhandisi Arnold Simwaba wamewasili Tanzania Juni 21, 2026 katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Tanzania, Wilson Nyamanga pamoja na Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kutoka REA Tanzania, Mhandisi Jones Olotu, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa REA Tanzania, Renatus Msangira.   Uongozi wa REA Zambia utakuwa nchini kwa ziara ya kikazi ya Siku 7 ambapo pamoja na vikao vya kubadilishana ujuzi, wajumbe hao wanatarajiwa kutembelea miradi mbalimbali ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini.

SERIKALI YAAHIDI KUSIMAMIA HAKI ZA WAKIMBIZI

Image
    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM   Serikali ya Tanzania imeahidi kuendelea kulinda, kusimamia na kutekeleza haki za binadamu ikiwemo haki za raia wa Tanzania na Wakimbizi kutoka nchi mbalimbali wanaohifadhiwa hapa nchini ambapo pia imesema itaendelea kusimamia Amani na Usalama ili madhila yanayotokea katika nchi nyingine yasitokee hapa nchini.   Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Patrobas Katambi (MB) wakati akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Tarehe 20 ya mwezi Juni, kila mwaka, huku kauli mbiu ya mwaka huu ikisema “Hadi Kila Mtu awe Salama”   Waziri Katambi akizungumza mbele ya Wakimbizi wanaoishi jijini Dar es Salaam ambao waliwawakilisha wakimbizi wanaoishi katika maeneo mbalimbali nchini amesema nchi ya Tanzania inajifunza kwa yaliyotokea nchi jirani huku akitoa ahadi ya serikali ya kuwahudumia Wakimbizi.   “Ni agizo ...

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 24 MACHI 2026

Image
 

SERIKALI YAHIMIZA MELI YA NEW MV MWANZA KUKUZA UCHUMI, UTALII KANDA YA ZIWA.

Image
  Serikali imetoa wito kwa wafanyabiashara, wasafirishaji na wawekezaji mbalimbali kutumia fursa ya meli mpya ya MV New Mwanza kibiashara na kiutalii ili kukuza uchumi wa Kanda ya Ziwa. ‎ Itakumbukwa meli hiyo imejengwa kwa zaidi ya Tsh. Bilioni 120, ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200, tani 400 za mizigo, magari makubwa matatu na madogo, ambapo itafanya safari zake katika bandari zote zinazozunguka Ziwa Victoria ikiwemo Kisumu (Kenya), Port Bay (Uganda) na Kemondo (Bukoba). ‎ ‎Akizungumza Jumapili Machi 22, 2026 na waandishi wa habari katika bandari ya Mwanza Kusini jijini Mwanza ilipoegeshwa meli hiyo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kutokana na uwekezaji huo wakazi wa Kanda ya Ziwa, wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa na wadogo wanapaswa kuitumia kwenye shughuli zao na kuleta tija ya uwekezaji huo mkubwa. ‎ ‎Amesema Serikali imetimiza jukumu lake la kutekeleza wajibu wa kujenga mazingira mazuri ya biashara, uwekezaji na ustawi wa jamii, hivyo mpira sasa unaha...