Sunday, December 9, 2018

WAZIRI MKUU AFURAHISHWA NA UWEKEZAJI WA VIWANDA CHALINZE


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa afurahishwa na uwekezaji wa viwanda katika halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, kwa kutembelea na kukagua viwanda vikubwa viwili katika ziara aliyoifanya Jana katika halmashauri hiyo.

Mheshimiwa Majaliwa ametembelea kiwanda cha kuzalisha vigae cha Twyford kilichoko katika kitongoji cha Pingo katika mamlaka ya mji mdogo wa Chalinze na kujionea shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho,ambacho ni kiwanda kinachozalisha vigae bora katika afrika mashariki na kinauza ndani na nje ya nchi.

Aidha Waziri Mkuu alitembelea pia kiwanda cha kutengeneza bidhaa zinazotokana na matunda cha Sayona Fruits Ltd kilichopo katika kijiji cha Mboga, kiwanda ambacho kinamilikiwa na mwenyekiti wa wamiliki wa viwanda Tanzania Subashi Patel, ni kiwanda kikubwa katika afrika mashariki chenye mitambo ya kisasa na kinachonunua matunda kwa wingi kama malighafi ya kuendesha kiwanda hicho.

Mheshimiwa Majaliwa alikagua na kuona uzalishaji wa vinywaji mbalimbali na kuona jinsi watanzania wanavyonufaika na ajira kiwandani hapo.

Mheshimiwa Majaliwa katika hotuba yake kiwandani hapo alimpongeza mwekezaji wa kiwanda hicho Subashi Pateli kwa uwekezaji wenye tija unaotoa huduma za jamii, kuzalisha ajira kwa watanzania lakini pia kutoa kodi ya serikali kuu na halmashauri ya wilaya kwa maendeleo ya nchi na kuwataka wawekezaji wengine wawekeze kwa tija ili kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Chama cha Mapinduzi kama ilivyonadiwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

" Katika kipengele cha viwanda kama kilivyotajwa kwenye Ilani kazi yetu ni kuweka vema kwani kimetekelezwa na muda wa uchaguzi utakapofika ni kuwauliza watanzania mnataka tufanye kitu gani kingine ." Waziri Mkuu alisema.

Majaliwa aliendelea kutoa wito kwa wanachalinze kulima matunda ambayo soko lake sasa linapatikana hapa kiwandani na kuwahamasisha kuleta matunda hayo kwani soko ni la uhakika na pasipo matunda uzalishaji haupo, akawataka wananchi kwa ujumla kuwalinda wawekezaji kwa udi na uvumba ili waweze kuzalisha kwa tija na kwa amani na utulivu kwani pasipo amani hakuna uzalishaji utakaofanyika hivyo aliwataka wananchi kwa ujumla kuwalinda wawekezaji popote pale nchini Tanzania ili uzalishaji ukafanyike kwa amani na wawekezaji wasikate tamaa kwa kutokuwa na amani katika maeneo waliyowekeza

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Pwani alitoa wito kwa wawekezaji wanaotaka kuja kuwekeza mkoani Pwani wanakaribishwa Pwani ni salama,mazingira ni rafiki kwa uwekezaji na amani ni ya kutosha," Tunayo ardhi ya kutosha kwa uwekezaji wa aina yoyote karibuni Pwani ya Viwanda." Ndikilo alisema.
 

WAZIRI KALEMANI AZITAKA TAASISI ZINAZOJENGA DODOMA KULIPIA UMEME ILI KUHARAKISHA UJENZI.

Taasisi zinazojenga majengo katika mji wa Serikali Dodoma zatakiwa kulipia gharama ya umeme mapema.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ameziagiza Wizara na Taasisi zilizoanza ujenzi na zilizo katika maandalizi ya ujenzi wa majengo katika Mji wa Serikali jijini Dodoma kuhakikisha kuwa, wanalipia gharama ya kupeleka umeme katika maeneo yao ili kuharakisha shughuli za ujenzi.

Dkt Kalemani ameyasema hayo wakati alipokuwa akikagua maandalizi ya ujenzi wa Jengo la Wizara ya Nishati katika Mji wa Serikali, Ihumwa jijini Dodoma ambapo aliambatana na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Raphael Nombo na Kamati ya Wizara inayosimamia ujenzi huo.

Dkt Kalemani amesema kuwa tayari miundombinu ya umeme imeshafika katika eneo hilo kwani Tanesco wameshafunga transfoma inayosambaza umeme katika eneo husika.

Ameeleza kuwa endapo Taasisi hizo zitalipia gharama hizo mapema zitaweza kufanya shughuli za ujenzi, usiku na mchana na hivyo kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa.

Aidha ametoa agizo kwa Meneja wa TANESCO mkoa wa Dodoma kuhakikisha kuwa, anafahamu mahitaji ya umeme ya eneo hilo la Serikali ili nishati ya umeme isiwe kikwazo cha utekelezaji wa kazi za ujenzi katika eneo hilo.

Kuhusu maandalizi ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati, ameridhishwa na hatua ya maandalizi na kumuelekeza mkandarasi ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
kuwa, kazi hiyo inakamilika kabla ya mwezi Januari, mwakani.

Aidha amemuagiza kuwa azingatie ubora na kuhakikisha kuwa anakuwa na vibarua wa kutosha kukamilisha hiyo ndani ya wakati.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uendelezaji Milki kutoka NHC, Haikamen Mlekio amesema kuwa watatekeleza maagizo ya Waziri kwa kumaliza ujenzi wa jengo hilo ndani ya wakati kwa kuwa wanauzoefu katika kazi hiyo.

Ameeleza kuwa tayari wana vibarua wa kutosha wa kuwawezesha kufanya kazi kwa haraka na ubora unaotakiwa.

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAIBUKA NA TUZO MBILI ZA TAARIFA BORA YA HESABU KWA MWAKA 2017

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akielezea kuhusu taaluma ya  Uhasibu kuwa nia  muhimu katika maendeleo ya Viwanda  na kutimiza ndoto ya Serikali ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 wakati wa kuhitimisha mkutano wa mwaka wa Wahasibu na kugawa tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa washindi wa mwaka 2017, katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi  eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
..........................................

Na, Peter Haule. WFM, Dar es Salaam

Wizara ya Fedha na Mipango Fungu Hamsini (Vote 50) linalohusika na masuala ya utawala, na Fungu ishirini na tatu (Vote 23) la Mhasibu Mkuu wa Serikali yamepata tuzo ya mshindi kwa nafasi ya pili na tatu katika utoaji wa Taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2017 katika kundi la Wizara na Idara za Serikali inayoandaliwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).

Tuzo hizo zimetolewa kwa washindi na Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa Mkutano wa mwaka wa Wahasibu nchini uliofanyika katika eneo hilo.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, taaluma ya Uhasibu inamchango mkubwa katika kukuza uchumi wa viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 kwa kuwa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu wanahusika moja kwa moja katika suala la utawala na uongozi kupitia mipango, kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali na pia kuweka mazingira bora ya uwekezaji  kuelekea katika maendeleo ya uchumi wa viwanda hivyo kuwa na tija katika agenda hiyo ya Taifa.

“Ni wazi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, inafanya kazi kwa bidii kuhakikisha Tanzania inakua na uchumi wa kati ifikapo 2025, jambo hili haliwezi kufikiwa na Serikali pekee bali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ambao wanaweza kutumia taaluma yao na kuishauri Serikali kwa njia mbalimbali, ikiwemo mijadala inayotokana na mikutano ya mwaka ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu”, alieleza Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa, ni vema Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu kuhakikisha wanaandaa taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu maendeleo ya viwanda ili wawekezaji wasipotoshwe kuhusu uhalisia wa maendeleo ya Sekta hiyo, kwa kuwa taarifa za fedha huwasaidia walipa kodi, wawekezaji na wadau wengine kufanya maamuzi.

Aidha alisema kuw,a Serikali inaendelea kupambana na wararushwa na watumiaji wabaya wa fedha za umma, kwa kuwa bado wapo Wahasibu ambao sio waaminifu ambao wanacheza na hesabu kupitia taaluma hiyo kupotosha ukweli, alisema kipindi cha kufanya mambo hayo kimepita na yeyote anayeendelea na tabia hiyo awe na uhakika hatabaki salama kama hata badilika.

Alibainisha kuwa suala la maadili ni muhimu sana kwa wahasibu kwa kuwa wao wanaweza kufanya Serikali ikapata mapato au kupoteza na kufanya ndoto za kuwa na uchumi wa viwanda kufikiwa au la

Hata hivyo kufikiwa kwa uchumi wa Viwanda kunategemea uimara wa Sekta ya Umma na Binafsi kwa kuwa wote wanajukumu la msingi la kufikia maendeleo hayo kwa kuwa na taarifa za soko, taarifa za kihasibu na kutafuta suluhisho kwa masoko ya fedha.

Naibu Waziri huyo amefurahishwa na kuongezeka kila mwaka kwa idadi ya washiriki katika ushindani wa taarifa bora ya fedha kutoka Sekta binafsi na umma, hasa Mamlaka ya Serikali za Mitaa na Taasisi za Serikali, kwa kuwa ni hatua kubwa kuelekea katika uwajibikaji na uwazi katika Sekta ya umma na kuongeza imani ya wananchi katika utendaji wa sekta hiyo.

 Naibu Waziri Kijaji, amewapongeza washindi wote kwa juhudi walizozifanya na kuwataka waendelee kufanya hivyo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla. Aidha amewapongeza wahasibu kwa kuamua kukaa pamoja na kujadili taaluma ya uhasibu katika maendeleo ya Sekta mbalimbali ikiwemo ya  viwanda ambayo ni ajenda ya kipaumbele kwa Serikali ya awamu ya tano.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA. Pius Maneno, alisema kuwa tuzo zinazotolewa na NBAA zinalengo la kuhamasisha uwajibikaji na kuandaa taarifa ya fedha zilizo na viwango vya kitaifa na kimataifa.

Alisema kuwa washindi wa tuzo hizo wanapatikana kupitia mchakato uliosheheni weledi wa hali ya juu kutoka kwa wabobezi wa taaluma ya uhasibu nchini ambao wanaangalia vigezo kadhaa vikiwemo taasisi kusajiliwa nchini, kuwasilisha hesabu kwa wakati na pia kufikisha kiwango cha ubora wa taarifa kuanzia asilimia 75.

Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50, Bw. Christopher Nkupama na Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi Fungu 23,  Bw. Aziz Kifile, walisema kuwa tuzo hizo walizopata zinawapa morali ya kufanyakazi kwa umahili zaidi na kuwapongeza watumishi walioko katika idara hizo  kwa kufanyakazi kubwa na bila kuchoka kuhakikisha kuwa wanazingatia kanuni na taratibu za uhasibu wanapotekeleza majukumu yao.

Mshindi wa Jumla katika tuzo hizo kwa taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2017 ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Tanga Cement  Plc na kwa upande wa Wizara na Idara za Serikali ni Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya  

Washiriki wa Tuzo hizo ni pamoja na Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Wakala wa Serikali, Wizara na Idara za Serikali na Sekta Binafsi. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akimkabidhi tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2017 Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi Fungu 23,  Bw. Aziz Kifile, katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi  eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis Mwakapalila (katikati), Mhasibu Mkuu wa Fungu  50 Bw. Christopher Nkupama (wa pili kushoto), Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi Fungu 23,  Bw. Aziz Kifile, na maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa na furaha baada ya kupokea tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2017 iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) eneo la Bunju, Nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
 
Washindi wa wa makundi mbalimbali ya  Tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2017 zinazotolewa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA)  wakiwa katika picha ya pamoja na Meza kuu baada ya kukabidhiwa tuzo hizo eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

 (Picha na Peter Haule- Wizara ya Fedha na Mipango)

JESHI LA WANANCHI JWTZ LATANGAZA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini Madaktari wa Binadamu na fani nyingine za Tiba.

      Nafasi hizo zinatolewa ili kuongeza idadi ya wataalamu wa tiba watakaotoa huduma za afya katika Hospitali zetu, vituo vya afya na Zahanati kulingana na mahitaji  ya sasa na siku zijazo.

      Watakao andikishwa Jeshini ni wale wenye taaluma zifatazo:-

a.           Daktari Bingwa wa Meno    –  Dental Surgeon

b.          Daktari Bingwa     –       Specialist Neurasurgeon

c.           Mkemia   (Chemisist)

d.          Mteknolojia Msaidizi (Maabara) – Assistant Laboratory Technician.

e.           Tabibu msaidizi     –  Assistant Clinical officer.

f.            Katibu wa Hospitali  –  

g.          Msaidizi wa kumbukumbu.  – Medical Records (Certificate)

h.          Daktari           – Medical Doctors. 

j.      Afisa Muuguzi  –  Registered Nursing Officer. 

k.     Fundi sanifu vifaa tiba  –  Bio Medical Engineer.

l.      Tabibu   – Clinical Assistant  (Certificate).

m.    Mteknolojia msaidizi –  Laboratory Assistant (Certificate)

n.     Mfamasia –  Pharmacist  (Degree) 

o.     Mtoa tiba kwa vitendo  – Physiotherapist  (Diploma)

p.     Afisa Muuguzi msaidizi  – Assistant Nursing officer

Sifa za kuandikishwa Jeshini ni zifuatazo:-

a.    Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.

b.    Awe na umri kati ya miaka 18 hadi 28 isipokuwa specialist

c.     Awe na afya njema ya mwili na akili timamu.

d.    Awe mwenye tabia njema na nidhamu nzuri

e.    Awe hajawahi kupatikana na hatia ya makosa ya jinai Mahakamani na kufungwa jela.

f.     Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate), vyeti vya shule (Academic & School Leaving Certificates) na vyeti vya Chuo (Transcript & Academic Certificates).

g.    Kama ni Daktari awe amemaliza mafunzo kwa vitendo (Internship) na kutunukiwa vyeti pamoja na kusajiliwa na Bodi.

h.    Awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo.

       Wenye sifa tajwa na kuhitaji kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania waripoti katika Kambi ya Jenerali Abdallah Twalipo, Mgulani    Dar es Salaam tarehe 17, Desemba, 2018 kuanzia saa 1.00 Asubuhi kwa usaili.

Waombaji wafike na vyeti halisi (Original Certificates) vya kuzaliwa na masomo pia wajitegemee kwa usafiri, chakula na malazi.

Aidha, watakaochaguliwa na kuandikishwa Jeshini watapatiwa mafunzo mbalimbali ya Jeshi na yatakayo waendeleza katika taaluma zao.

 Wakiwa Jeshini majukumu watakayopatiwa ni yale yatakayowapa changamoto na fursa nzuri za kutumia taaluma zao.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini Madaktari wa Binadamu na fani nyingine za Tiba.

      Nafasi hizo zinatolewa ili kuongeza idadi ya wataalamu wa tiba watakaotoa huduma za afya katika Hospitali zetu, vituo vya afya na Zahanati kulingana na mahitaji  ya sasa na siku zijazo.

      Watakao andikishwa Jeshini ni wale wenye taaluma zifatazo:-

a.           Daktari Bingwa wa Meno    –  Dental Surgeon

b.          Daktari Bingwa     –       Specialist Neurasurgeon

c.           Mkemia   (Chemisist)

d.          Mteknolojia Msaidizi (Maabara) – Assistant Laboratory Technician.

e.           Tabibu msaidizi     –  Assistant Clinical officer.

f.            Katibu wa Hospitali  –  

g.          Msaidizi wa kumbukumbu.  – Medical Records (Certificate)

h.          Daktari           – Medical Doctors. 

j.      Afisa Muuguzi  –  Registered Nursing Officer.  

k.     Fundi sanifu vifaa tiba  –  Bio Medical Engineer.

l.      Tabibu   – Clinical Assistant  (Certificate).

m.    Mteknolojia msaidizi –  Laboratory Assistant (Certificate)
n.     Mfamasia –  Pharmacist  (Degree) 

o.     Mtoa tiba kwa vitendo  – Physiotherapist  (Diploma)

p.     Afisa Muuguzi msaidizi  – Assistant Nursing officer

Sifa za kuandikishwa Jeshini ni zifuatazo:-

a.    Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.

b.    Awe na umri kati ya miaka 18 hadi 28 isipokuwa specialist

c.     Awe na afya njema ya mwili na akili timamu.

d.    Awe mwenye tabia njema na nidhamu nzuri

e.    Awe hajawahi kupatikana na hatia ya makosa ya jinai Mahakamani na kufungwa jela.

f.     Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate), vyeti vya shule (Academic & School Leaving Certificates) na vyeti vya Chuo (Transcript & Academic Certificates).

g.    Kama ni Daktari awe amemaliza mafunzo kwa vitendo (Internship) 
na kutunukiwa vyeti pamoja na kusajiliwa na Bodi

h.    Awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo.

       Wenye sifa tajwa na kuhitaji kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania waripoti katika Kambi ya Jenerali Abdallah Twalipo, Mgulani    Dar es Salaam tarehe 17, Desemba, 2018 kuanzia saa 1.00 Asubuhi kwa usaili.

Waombaji wafike na vyeti halisi (Original Certificates) vya kuzaliwa na masomo pia wajitegemee kwa usafiri, chakula na malazi.

Aidha, watakaochaguliwa na kuandikishwa Jeshini watapatiwa mafunzo mbalimbali ya Jeshi na yatakayo waendeleza katika taaluma zao. 

Wakiwa Jeshini majukumu watakayopatiwa ni yale yatakayowapa changamoto na fursa nzuri za kutumia taaluma zao.

TASWA YAKAMILISHA RASIMU YA KWANZA YA KATIBA YA CHAMA HICHO

KAMATI ya Marekebisho ya Katiba ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), imekamilisha Rasimu ya Kwanza ya Mapendekezo ya Katiba ya chama hicho na itaanza kutolewa kwa wadau mbalimbali leo Jumapili Desemba 9, 2018 kwa ajili ya kujadiliwa.

Hatua ya kuandaa rasimu hiyo ya kwanza imefanywa na Kamati ya Marekebisho ya Katiba ya TASWA kwa kuangalia Katiba za vyama mbalimbali duniani vinavyohusiana na waandishi wa habari za michezo na pia kupitia muongozo kutoka Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS), ambacho TASWA ni mwanachama.

Pia Kamati imechambua Katiba ya sasa ya TASWA na kupokea maoni kutoka kwa waandishi wa habari za michezo kuhusu maeneo yenye upungufu kwa nia ya kuiboresha.

Maeneo mbalimbali yamefanyiwa kazi  katika rasimu hiyo baadhi yakiwa ni sifa za mwanachama, wajibu wa mwanachama, muundo wa uongozi, sifa za viongozi na pia ukomo wa uongozi.

Pia kuna mapendekezo katika rasimu hiyo ya kuanzishwa kamati mbalimbali kwa nia ya kuisaidia Kamati ya Utendaji.

Kutokana na hali hiyo, Kamati imepanga hatua ya kwanza baada ya kuitoa rasimu hiyo leo, itapokea maoni binafsi ya wadau kwa njia ya email (katibataswatz@yahoo.com), kisha itakutana na wahariri wa habari za michezo, waandishi waandamizi na waandishi chipukizi kwa kadri mtakavyotaarifiwa.

Baada ya kupokea maoni kutoka makundi hayo, Kamati itafanya mikutano miwili, ambapo wa kwanza utakuwa wa wadau wote kuijadili kwa pamoja na kisha kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji ya TASWA utafanyika Mkutano Mkuu wa kuipitisha na kuiwasilisha kwa Msajili tayari kwa Uchaguzi Mkuu haraka iwezekanavyo.

Ni matumaini ya Kamati ya Katiba kila mdau ataisoma vyema rasimu hiyo na kutoa mchango wake na mwisho wa kufanya hivyo ni Desemba 12 mwaka huu. Mapendekezo ya Rasimu hiyo nimeambatanisha katika email zenu.

Kamati ya Katiba ya TASWA imeundwa kutokana na agizo la Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe aliyeitaka BMT isitishe uchaguzi wa TASWA uliokuwa umepangwa kufanyika Novemba 25 mwaka huu na badala yake BMT ikutane na viongozi wa TASWA pamoja na baadhi ya wanahabari wa michezo kuona namna ya kuifanyia marekebisho Katiba ya TASWA iendane na wakati. 

Kamati ya Katiba inayoongozwa na Mwenyeketi wa zamani wa TASWA, Boniface Wambura ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), viongozi wengine ni Katibu wa Kamati Amir Mhando ambaye pia ni Katibu Mkuu wa TASWA na mwanahabari, Gift Macha ambaye ni Katibu Msaidizi wa Kamati. 

Wajumbe ni Katibu Mkuu wa zamani wa TASWA, Abdul Mohammed, Mhazini wa zamani wa TASWA, Nasongelya Kilyinga na wanahabari Thabit Zacharia na Devotha Kihwelu.

UJENZI WA GATI NYAMISATI WAANZA, SHEHENA YA VIFAA YAANZA KUWASILI -KUANDIKWA

NA MWAMVUA MWINYI, KIBITI

NAIBU waziri wa Ujenzi, Elias Kuandikwa amesema ujenzi wa gati, uliokuwa ukisubiriwa kwa kipindi kirefu na wakazi wa Nyamisati wilayani Kibiti mkoani Pwani umeanza ambapo shehena ya vifaa  vya ujenzi vimeanza kuwasili tayari kwa ajili ya kazi. 

Aidha amewatoa wasiwasi wakazi wa Mafia kuhusu gati la Kilindoni ,kwamba linatarajiwa kuboreshwa kwa kuondoa dosari ndogondogo zilizopo ili liwe la kisasa. 

Akizungumza na wananchi wakati alipotembelea eneo litakapojengwa gati hilo, katika muendelezo wa ziara yake mkoani hapo, Kuandikwa alisema ujenzi utakuwa wa miaka miwili kwa gharama ya sh. bilioni 14 .

Alimtaka , mkandarasi wa gati hilo kufanya kazi inayotakiwa kwa kuhakikisha, ujenzi unakamilika kwa wakati ikiwezekana kuukamilisha kabla ya miezi 24.

Kuandikwa alisema, ujenzi umeshaanza na mkataba ulisainiwa tarehe 24,octoba mwaka huu, ombi lake ni kuona mkandarasi anamaliza kazi haraka. 

“Fedha zipo hatutaki kuona mkandarasi anasuasua, gati litasaidia kurahisisha usafiri kwani ndio kiu ya wakazi wa Nyamisati na Mafia”
“Itakuwa gati la kisasa na sasa tunakwenda kufanya maboresho katika gati la Kilindoni wilayani Mafia ili kuwa na gati la uhakika ,kwa kuwa itazingatia ubora, teknolojia mpya kwa lengo la magati haya yaweze kudumu kwa miaka mingi “alisisitiza Kuandikwa. 

Pamoja na hayo, alielezea ujenzi huo utakwenda pamoja na maboresho ya barabara ya Bungu -Nyamisati itakayosaidia kurahisisha usafiri . 

Akiwa barabara ya barabara ya Mkuranga -Kisiju kiwango cha lami,  yenye urefu wa 1.8km alimpongeza meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoani Pwani, Yudas Msangi kwa kubana matumizi kwenye miradi na kuweza kutumia katika miradi mingine. 

Msangi alisema kwasasa wanaendelea na kazi za kufungua na kuboresha baadhi ya barabara muhimu kuelekea katika miradi mikubwa mbalimbali.
 

MAGAZETI YA LEO DESEMBA 9, 2018.

Saturday, December 8, 2018

TAKUKURU LINDI YAWAONYA WANAOKWEPA USHAHIDI.

Na hadija Hassan Lindi.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Lindi, imetoa onyo kwa wananchi,na watumishi wa mkoa huo walio na tabia ya kupeleka Malalamiko Ofisini kwao kisha kukataa kutoa ushahidi wa kumtetea Mhalifu.

Onyo hilo limetolewa na kamanda wa Takukuru mkoani hapa Steveni Chami Jana alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari  Ofisini kwake.

Chami ametoa onyo hilo ,kufuatia watumishi watatu wa Idara ya Afya Katika kituo cha Afya cha Manispaa ya Lindi ,kufika Ofisi ya Taasisi hiyo kulalamikia aliyewahi kuwa Kaimu Mganga Mkuu  wa Manispaa hiyo,Abirahi Rashid Mbingu,kudaiwa kudhurumu fedha za malipo kwa Manesi waliokuwa wamefanya kazi ya ziada.

Alisema kufuatia taarifa hiyo,waliifanyia kazi ikiwemo kukusanya nyaraka zilizotumika kufanyia malipo,kuwaita wale watumishi waliodaiwa kulipwa fedha hizo,ili kutambua iwapo sahihi zilizokuwa zimeonekana ni za kwao na kuzikataa kwamba sio zao na hawajawahi kulipwa.

Chami alisema baada ya taratibu zote za ki-Ofisi kukamilika,mtuhumiwa Mbingu Juni 15/2017,alifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Lindi kwa kesi Namba 57/2017,kujibu Shitaka linalomkabiri, lakini ilipofika zamu ya watumishi hao kutoa ushahidi wao,waligeuka na kumtetea mshitakiwa.

“Hawa watumishi ambao hapo awali waliiambia Takukuru hawakuwa wamelipwa fedha za On-Call allowance zilizoonyesha katika orodha ya walipwaji sio zao,lakini walipofika Mahakamani waligeuka na kudai sahihi sio zao fedha wamepata”Alisema Chami.

Aidha kamanda  chami amewataja watumishi  hao ambao wote amedai ni manesi wa Kituo cha Afya cha Manispaa hiyo kuwa ni,Stephen Haji,Mwanahawa Swalehe na Mayila Chikamtenda.

“Ugeugeu uliofanywa na watumishi hawa,kwa makusudi wameamua kumsaidia mtuhumiwa kwa kusema uongo Mahakamani,kitendo ambacho ni kosa la jinai na kinyume na Kifungu cha 102 cha Sheria ya kanuni ya adhabu,Sura ya 16/2002”Alisema Chami.

Alisema kutokana na ugeugeu ulionyeshwa na watumishi hao,Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Lindi,Liliani Lugalabamo alilazimika kumuachia huru mshitakiwa Abirahi Rashidi Mbingu,baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kumtia hatiani.

Hata hivyo,Chami alisema kutokana na kitendo hicho Ofisi ya Takukuru Mkoani Lindi,imewafungulia kesi ya jinai namba 122/2018,watumishi hao watatu kwa kosa la kusema uongo na kukataa kueleza ukweli Mahakamani.