Friday, November 23, 2018

WASHIRIKI WA MASHINDANO YA RIADHA KWA WANAWAKE WAKABIDHIWA VIFAA.

Baadhi ya washiriki wa mashindano ya riadha kwa wanawake yanayoitwa “Ladies First” wakipokea vifaa toka kwa waandaaji kwa ajili ya mashindano hayo yatakayofanyika kesho katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa mashindano ya riadha kwa wanawake yanayoitwa “Ladies First” wakipokea vifaa toka kwa waandaaji kwa ajili ya mashindano hayo yatakayofanyika kesho katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa mashindano ya riadha kwa wanawake yanayoitwa “Ladies First” wakisubiri utaratibu toka kwa waandaaji wa mashindano hayo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Alex Mkenyenge akifafanua jambo kwa washiriki wa mashindano ya riadha kwa wanawake yanayoitwa “Ladies First” wakati wa semina elekezi iliyofanyika mapema hii leo jijini Dar esa Salaam.

Mtaalamu toka Japan, Dk. Okada akitoa mafunzo kwa washiriki wa mashindano ya riadha kwa wanawake yanayoitwa “Ladies First” wakati wa semina elekezi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam
Baadhi ya washiriki wa mashindano ya riadha kwa wanawake yanayoitwa “Ladies First” wakimsikiliza Mtaalamu toka Japan Dk. Okada (hayupo pichani) wakati wa semina elekezi iliyofanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

DKT. NDUGULILE – “SEKTA YA AFYA NCHINI INAKUWA KWA KASI”

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akionyesha mafuta maalum kwa ajili ya kuwakinga wenye ulemavu wa ngozi dhidi ya miale ya jua yanayotengenezwa na  kitengo cha Kilimanjaro Sunscreen Production kilichopo Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akihojiana na Bw. Longini Mtalo, Mteknolojia kutoka kituo cha utengenezaji wa viungo bandia katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC  huku akiwa ameshika sampuli ya kiungo bandia kilichotengenezwa na kituo hicho.
.............................................

Sekta ya afya inakua kwa kasi huku huduma muhimu za afya kwa sasa zikiwa zinapatikana hapa hapa nchini”


Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile alipokua akizungumza na watumishi wa Hospitali ya rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) iliyopo katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro jana Novemba 22, 2018.


Dkt. Ndugulile amesema kuwa Sekta ya Afya imepewa kipaumbele cha hali ya juu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. 


Dkt.John Pombe Magufuli katika kipindi cha miaka mitatu mageuzi makubwa ndani ya sekta ya afya yameanza kuonekana huku huduma za matibabu ya kibingwa yakiwa zikipatikana hapa hapa nchini.


“Tunasimama hapa kifua mbele tukiona mabadiliko katika hali ya upatikanaji wa dawa kuimarika zaidi, bajeti ya dawa imeongezeka toka Shilingi Bilioni 30 mpaka Shilingi Bilioni 270 yaani mara tisa zaidi ndani ya miaka mitatu” alisema Mhe.Naibu Waziri na kuendelea 


“Tumeboresha vituo vya afya takribani 300, huku Mkoa wa Kilimanjaro ukiwa na Vituo 8 vilivyoboreshwa vilivyogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 3.5 na kwa mwaka huu 2018 Serikali imeanza kujenga Hospitali za Wilaya 67 nchini”


Aidha, Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali imetenga Shilingi Bilioni 30 kwa ajili ya Hospitali mpya za Rufaa za Mikoa ili  ziweze kutoa huduma za kibingwa, kupunguza msongamano wa wagonjwa na ucheleweshwaji wa huduma katika Hospitali za rufaa za kanda.


Naibu Waziri huyo Aliendelea kusema  kuwa fedha hizo Shilingi Bilioni 30 zitaelekezwa katika maeneo makuu matano ambayo aliyataja kuwa ni kuhakikisha kila Hospitali ya Mkoa ina Kitengo cha dharura, chumba cha upasuaji, kitengo cha uangalizi wa wagonjwa mahututi pamoja na kitengo cha mama na mtoto.


“Hospitali hii inatakiwa kuhudumia wagonjwa waliopata rufaa toka hospitali za mikoa ya jirani waje huku kupatiwa huduma za matibabu na sio wagonjwa wa malaria na mafua alisema Dkt. Ndugulile.


Katika kuhakikisha huduma bora za afya zinatolewa kwenye hospitali za rufaa za mikoa, Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeweka maeneo muhimu katika mafunzo kwa watumishi wa kada ya afya huku akitaja watumishi wenye kuhitajika zaidi kwa sasa kuwa ni madaktari wa magonjwa ya ndani, watoto, wakina mama, upasuaji, mifupa pamoja na madaktari wa usingizi.


Kuhusu upatikanaji wa huduma za kibingwa, Dkt.Ndugulile alisema  mafanikio  kuona huduma hizo zikiwa zinapatikana hapa nchini tofauti na zamani  “Tunafanya upandikizaji wa figo pamoja na upandikizaji wa vifaa vya usikivu kwa wa watoto huduma ambazo zilikuwa ni za kufikirika ndani ya miaka mitatu sasa zinapatikana hapa nchini” alisema Dkt. Ndugulile.


Awali akitoa taarifa yake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC Dkt. Gileard Masenga aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Hospitali hiyo “Licha ya kumilikiwa na Taasisi ya kidini lakini Serikali imeendelea kutupatia wataalam, 
misamaha ya kodi za malighali zinazoingizwa nchini ambazo hutumika kutengeneza mafuta ya kuwakinga wenye ulemavu wa ngozi dhidi ya jua.


Aidha, Dkt.Masenga alisema hospitali yake imetengewa  Shilingi Bilioni 1 kwa ajili ya dawa za Saratani huku fedha kiasi cha Shilingi Milioni 250 tayari  zimeshapelekwa Bohari ya dawa kwa ajili ya ununuzi wa dawa hizo.


 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto yupo Mkoani hapa kwa ziara  ya kikazi  inayolenga kukagua shughuli za huduma ya Afya,Maendeleo ya Jamii pamoja na kuongea na watumishi wa sekta  hizo.

MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 23, 2018.

Thursday, November 22, 2018

ELIMU YA MAENDELEO ITOLEWE- KIWANUKA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Amina Kiwanuka,(kushoto)  akizungumza jambo na Diwani wa Kata ya Talawanda ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu (kulia) anaesikiliza (katikati) ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa katika moja ya vikao vilivyowahi kufanyika Halmashauri ya Chalinze.
..................................................... 

Na Omary Mngindo, Lugoba- Chalinze.

VIONGOZI katika Vijiji na Kata zinazounda Halmashauri ya Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wameshauliwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujiletea maendeleo, ili waondokane na dhana kuwa watakapoanza mradi, Serikali itaongezea nguvu.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Amina Kiwanuka, alipozungumza na Madiwani, kwenye Baraza la kupokea taarifa za Kata, ambapo alisema suala la maendeleo ni la wananchi wenyewe, na si kuitegemea Serikali.

Aidha Kiwanuka alisema kuwa, inapobidi wananchi na Wadau wa maendeleo kwenye maeneo yao, washirikiane kuendeleza miradi, kwani fedha zinapopatikana kuna mambo mengi yanayotakiwa kufanyika katika nyanja mbalimbali.

"Nikuombe Mwenyekiti kwa kushirikiana na viongozi wenzetu tushirikiane katika kuwapatia elimu wananchi wetu, tutambue kwamba kazi ya kujiletea maendeleo ni yetu wenyewe, kwakuwa tupo changamoto lazima zitukabili," alisema Kiwanuka.

Diwani wa Kata ya Miono Juma Mpwimbwi aligusia changamoto za wingi wa wanafunzi katika shule zake, maji, barabara ya kutoka njiapanda ya Mandera, Miono, Mkange mpaka Saadani ambayo kipindi cha mvua hazipitiki.

"Sanjali na changamoto hizo, pia kuna uhaba wa nyumba za walimu katika shule ya sekondari ya Kikaro, iliyoanzishwa miaka ya 58, mpaka sasa ina nyumba tano tu za walimu naliomba Baraza liiangalie shule ile," alisema Mpwimbwi.

Mhandisi Juma Mgweno diwani wa Kata ya Mkange aliliambia Baraza hilo kwamba kwenye eneo lake shughuli za kimaendeleo zinafanyika, huku akisema pamoja naa shughuli za maendeleo, uhamasishaji wa upimaji afya unafanyika kwa wananchi wake.

Zikatimu alisema kuwa kwenye Baraza hilo zimejitokeza changamoto saba, zilizogawanyika katika sekta za watumishi, na kwamba wamewasilisha kwa viongozi husika, maji huku akisema kuhusu barabara watawasiliana na Wakala was Ujenzi wa Barbara Mijini na Vijijini TARURA.

Dignity Kwanza YAWAPA SEMINA WAHARIRI KUHUSU WAKIMBIZI.

 Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika semina ya siku moja iliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu maswala ya wakimbizi.

Semina hiyo ambayo imeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Dignity Kwanza imefanyika leo Novemba 22, 2018 katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa semina hiyo ambao ni wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mada zilizowasilishwa na wawezeshaji kutoka Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR pamoja na waandaaji Dignity Kwanza.
Mkurugenzi wa BAGAMOYO KWANZA BLOG, Athumani Shomari Mkwama (katikati) ambae pia ni Mhariri Mkuu wa BAGAMOYO KWANZA BLOG akiuliza swali kwenye semina hiyo iliyolenga kuwajengea uwezo wahariri kuhusu maswala ya wakimbizi ambayo imefanyika katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam, leo Novemba 22, 2018. kushoto ni mhariri wa gazeti la Tanzania Daima na kushoto ni Mhariri msaidizi wa Gazeti imaan.
 Mhariri wa Gazeti la Serikali Habari lelo, Beda Msimbe akifuatilia kwa makini semina hiyo iliyohusu kujenga uelewa kuhusu maswala ya wakimbizi iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Dignity Kwanza
ambayo imefanyika katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam, leo Novemba 22, 2018.

Washiriki wa semina hiyo ambao ni wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mada zilizowasilishwa na wawezeshaji kutoka Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) pamoja na waandaaji Dignity Kwanza semina iliyofanyika katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam, leo Novemba 22, 2018.
 Meneja wa maswala ya kisheria na utetezi kutoka Dignity Kwanza, Mwajabu Khalid akiwasilisha mada inayohusu kiwango cha ulinzi kichaohitajika kwa wakimbizi katika nchi na kimataifa kwa ujumla.
 
Meneja wa maswala ya kisheria na utetezi kutoka Dignity Kwanza, Mwajabu Khalid, akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza semina hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam, leo Novemba 22, 2018.
 
 Meneja wa Uhamasishaji wa Rasilimali na uhusiano wa nje, kutoka Dignity Kwanza, Nobel Nondo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo iliyofanyika Hoteli ya New Africa jijini Dare es Salaam leo Novemba 22, 2018.

 Picha ya pamoja wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, waandaaji wa semina hiyo Dignity Kwanza na wawakilishi kutoka Shirika la Kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR)

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ)

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama mnavyofahamu linashiriki Ulinzi wa Amani ndani na nje ya Bara la Afrika.

JWTZ linasikitika kuwataarifu kwamba limewapoteza wapiganaji wake watatu (3) waliofariki kwa tarehe tofauti nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Afrika ya Kati (CAR) wakiwa kwenye jukumu la Ulinzi wa Amani baada ya kushambuliwa na vikundi vinavyosadikiwa kuwa ni vya waasi.  
         
Mashujaa wetu waliouwawa ni Koplo Mohamed Mussa, Koplo Erick Masauri John na Praiveti Musa Shija Machibya.  Miili ya marehemu hao tayari imepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kuhifadhiwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo.

Heshima za mwisho kwa mashujaa wetu hao zitatolewa katika sehemu ya kuagia Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo kesho tarehe 23 Novemba 2018 kuanzia saa 2.30 asubuhi.  Vyombo vya Habari na Wananchi wanakaribishwa tuungane katika kuaga mashujaa wetu.

Mungu azilaze Roho za Mashujaa wetu mahali pema Peponi, Amina.

REA AWAMU YA III MZUNGUKO WA PILI KUNUFAISHA VIJIJI VILIVYOSALIA KUANZIA JUNE 2019

Naibu waziri wa nishati ,Subira Mgalu, ambae ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Pwani akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Chalinze.
..........................................................
 
NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE.

MWELEKEO wa mradi wa wakala wa umeme vijiji (REA III )mzunguko wa pili unatarajia kuanza June 2019 ,ili kuvifikia vijiji ambavyo vimesalia katika utekelezaji wa mradi huo awamu ya kwanza.

Aidha mradi wa ujazilizi unatarajiwa kuanza mwezi machi mwakani huku mradi wa peri -urban utakaohusisha mkoa wa Pwani na Dar es salaam unategemewa kupata mkandarasi Januari mwaka huo na umeshatengewa sh.bilioni 83.

Naibu waziri wa nishati ,Subira Mgalu alieleza hayo katika kikao cha madiwani cha kata kwa kata kilichofanyika Lugoba Chalinze, mkoani Pwani ,wakati akitolea ufafanuzi utekelezaji unavyoendelea wa miradi ya umeme vijijini na mipango ya miradi hiyo ya kimkakati .

Alisema,kwa jitihada zote hizo za serikali kutekeleza miradi ya vijijini tayari vijiji 4,702 vimeshafikiwa hadi sasa .

Subira alisema maeneo yote iliyolengwa wakandarasi wanaendelea na kazi .

Kwa mujibu wake ,mkoa wa Pwani katika REA awamu ya III vipo vijiji 150 ,ambapo baadhi ya vijiji vimeshawekwa miundombinu na vingine mita .

Alilielekeza shirika la umeme (TANESCO) kuendelea kusambaza umeme kwenye maeneo ya wananchi pasipo kusubiri utekelezaji wa mradi wa REA.

“Serikali inafanya kazi ,nia yetu ni ushindi na sio ushindi tuu katika chaguzi zinazokuja bali tuwe na majibu ya namna tunavyotekeleza ilani vijijini na vitongojini” alisisitiza Subira.

Nae mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze ,Saidi Zikatimu aliiomba serikali kuwa, vijiji vinavyopitiwa na umeme vifikie vitongoji vyake na kufikia vijiji ambavyo tangu dunia iumbwe havina umeme.

Diwani wa kata ya Miono ,Juma Mpwimbwi alieleza bado kuna tatizo la ukosefu wa umeme kijiji cha Mkwajuni na Makaomakuu ambapo tangu wapimiwe nguzo hawajapelekewa vifaa wala kuandaa miundombinu .

ELIMU BURE HAIMUONDOLEI MZAZI WAJIBU WA KUTUNZA WATOTO.

Mbunge wa viti maalu kupitia CCM kutokea mkoa wa Pwani Zaynabu Vulu akizungumza na wazazi wa mkoa huo.


Na Shushu Joel,Mlandizi.
MBUNGE wa viti maalumu mkoa wa Pwani kupitia chama cha mapinduzi CCM Zaynabu Vulu amewataka wazazi na walezi  wote mkoani humo kutambua kuwa uamuzi wa serikali katika kutoa elimu bure haitomuomdolea mzazi au mlezi wajibu wake wa kumtuza mtoto kwa ajili ya mahitaji yake pindi anapokuwa shuleni ambayo ni nguo,madaftari na mchango wa chakula ili kuimalisha afya ya mwanafunzi katika uelewa wake masomoni.

Elimu ni nguzo kubwa kwa mahitaji ya wataalamu katika nchi yeyote ile kwa lengo la kuendesha shughuli za serikali hivyo wazazi na walezi kwa pamoja wanamajukumu ya kuwajali kwa kuwatimizia mahitaji yao ya kila siku watoto wao.

Kauli hiyo aliitoa jana alipokuwa katika mkutano na mwenyekiti wa UWT uliokuwa ukiwahamasisha wazazi kutambua wajibu wao kwa watoto wao na si kila jambo la shule waliachie serikali.

Aliongeza kuwa madhumuni ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ni kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne kwa lengo la kuwapunguzia wazazi mzigo mzito na pia ilikuwa ni moja ya sera ya CCM katika kujinadi walipokuwa wakiomba ridhaa kwa wananchi pindi walipokuwa wakiomba nafasi ya kuwatumikia.

“Serikali ya awamu ya ano imeamua kuwekeza katika elimu kwa ajili ya maendeleo ya taifa,na kwamba kwa kutoa fursa hiyo kumetengeneza idadi kubwa ya watoto walioandikishwa kuanza darsa la kwanza mwaka huu na wale wanaoingia kidato cha kwanza nchini kote”Alisema Vulu.

Aliongeza kuwa baadhi ya wazazi wanapaswa kubadilika kwani wamekuwa wakibweteka na mpango wa serikali ya awamu ya tano katika utoaji wa elimu bure,wamekuwa hawataki kujishughulisha hata kwa uhitaji wa manunuzi ya mahitaji muhimu ya wanafunzi shuleni.

Katika taarifa yake katibu wa UWT mkoa wa Pwani Mwajuma Nyamka alisema kuwa tangu kutangazwa kwa elimu bure kumekuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wazazi wakidai ni kwanini watoto wasinunuliwe nguo za shule pia ilivyo kwa ada,kitu ambacho amekuwa akikitolea ufafafuzi mkubwa kwa wazazi na walezi walio wengi kutambua umuhimu na nafasi zao katika familia zao.

Alisema kuwa katika suala la serikali serikali kuwasaidia wazazi katika jambo la ada basi wazazi na walezi wengi wamekuwa wakihitaji kila kitu serikali ifanye kupitia wanafunzi wao walioko mashuleni kitu ambacho si sahihi kutokana na kuwa serikali inahitajika kufanikisha maendeleo katika kila nyanja ili wananchi wote waweze kupata huduma za kijamii kwa wakati.

Naye mwenyekiti wa UWT mkoa wa Pwani Farida Mgomi amempongeza mbunge huyo kwa kutoa neno lilikuwa likiwaumiza kichwa wao kama viongozi wa kisiasa kwa wananchi wao,hivyo amewataka viongozi wote wanapokuwa na shughuli za kukutana na wananchi wanapaswa kulisema hilo kwa baadhi ya wananchi wasiotaka kubadilika kwa watoto wao ambao wanakosa hata nafasi ya kupumua kwa hofu ya kulipa ada.

Aidha amewapongeza wazazi wote waliojitokeza  katika mkutano huo na kuwahakikishia shuwa serikali itaendeleo kuwasaidia wananchi wote katika kuhakikisha elimu bure inakwenda mbali zaidi ya hapo ilipo sasa.

Hivyo Mgomi alitumia fursa hiyo kuwataka kinamama wote mkoa wa Pwani kuhakikisha wanachangamkia fursa za mikopozilizoko katika halmashauri za mkoa huo ili kujikwamua katika uchumi wa viwanda ambapo mkoa huo umezidi kujichukulia umaarufu wa kuongoza katika sekta hiyo.
Zaynabu Vulu akimsikiliza moja wa wazazi hayupo pichani juu ya sula la elimu bure .

MKOA WA PWANI UMEKUSANYA KILO MIL. 17.3 SAWA NA TANI 17,313,010 ZA KOROSHO -NDIKILO

mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo
..............................................

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

MKOA wa Pwani umekusanya kilogramu milioni 17.3 sawa na tani 17,313,010 za zao la kibiashara la korosho katika maghala mbalimbali yaliyopo kwenye wilaya za mkoa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha baada ya kutembelea iliyokuwa kiwanda cha kubangulia korosho cha Tanita Kibaha mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alisema korosho hizo zimekusanywa hadi Novemba 21.

Alieleza,korosho hizo zimekusanywa kwenye vyama vya msingi na vikuu vya ushirika (Amcos )kwenye halmashauri za wilaya .

Ndikilo alisema halmashauri ya Mkuranga inaongoza kwa kukusanya kilo milioni 6.2 ikifuatiwa na Halmashauri ya Kibiti milioni 6.6.

Alitaja halmashauri nyingine ni Rufiji milioni 2.9,Kisarawe 390,000,Kibaha Mjini 354,318,Kibaha 316,205,Chalinze 86,719 Bagamoyo 90,724 na Mafia 108,000.

Alielezea,kwa utaratibu wa sasa wa serikali wa kununua korosho zote utawafanya wakulima kupata malipo yao halali na kwa wakati tofauti na ilivyokuwa zamani.

“Faida nyingine tutaweza kujua uzalishaji halisi ndani ya mkoa wetu kwani udhibiti wa usafirishaji korosho kwenda mikoa mingine kwa sasa haupo,” alisema Ndikilo.

Kipindi cha nyuma korosho ilishuka na kuuzwa shilingi 1,800 hadi 1,900 lakini kwa sasa korosho itauzwa kwa shilingi 3,300 kwa kilogramu.

Aliwaasa wakulima kuhakikisha wanakausha korosho zao ili zifikie viwango na ziwe zenye ubora unaotakiwa.