Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo Mkoa wa Pwani ndg David Mramba amesema hawako tayari kuwafumbia macho wanaojiita boko haramu kwani kujiita hivyo ni kuhatarisha maisha ya Watanzania.
Mramba ameyasema hayo leo tarehe 06/02/2024 katika Ofisi za CCM Mkoa wa Pwani kuwa CCM ina macho mengi hata mtu akiwa kwenye shimo ataonekana na akibainika hataachwa salama kimaadili.
Amesema wako watu wanataka kuwatishia Wanaccm kwa kujiita wao ni boko haramu jambo ambalo si jema ndani ya CCM.
" Unapojiita boko haramu tafsiri yake wewe ni mtekaji na mbakaji hivyo lazima tuwashughulikie watu wa aina hiyo amesema Mramba
Ameendelea kusema kuwa hakuna kikundi ndani ya CCM kitakachokuwa na uwezo wa kubadili mawazo ya Wanaccm kwa kuwatishia.
Amesema wako wanaowatishia Viongozi walioko madarakani wakidai kuanza kutengeneza safu zao huku wakijipachika majina ya aina hiyo.
Hatutawavumilia wanaokiuka taratibu za Chama na tuko tayari kuwaadhibu ili Chama na wanachama wabaki salama amesema Mramba
Acheni vihelehele vya kuwasumbua Viongozi walioko madaraka waacheni watekeleze Ilani ya CCM kwa mioyo safi* - asema Mramba
Mramba amezungumzia usemi usemao kuwa acha haki iamue haki usitafute haki pasipo haki akimaanisha unaweza ukawa na haki ya kugombea nafasi yoyote lakini ukaipoteza haki hiyo kwa sababu ya rafu za mapema.
Amehitimisha kwa kuwataka Wanaccm kulinda heshima ya Chama na kujilinda wao ili wakati wa uchaguzi wasiwe kikwazo kwenye vikao vya mchujo.
Taarifa hii imeandaliwa na
No comments:
Post a Comment