Na Albert Kawogo, Mtwara
BANDARI ya Mtwara imeongeza kiasi cha mizigo inayohudumiwa hapo kutoka kiasi cha tani laki nne hadi tani milioni 1.6 katika kipindi cha mwaka 2022/2023.
Chachu ya ongezeko hilo linatokana na hatua kubwa ya kimkakati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA kufanya maboresho yenya thamani ya shilingi bilioni 157.8 kwenye eneo la gati ya bandari hiyo sambamba na ununuzi wa mtambo wa kupakia na kushusha mizigo.
Ferdinand Nyathi meneja wa Bandari ya Mtwara amewaeleza wahariri wa habari kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) waliotembelea bandari hiyo kuwa, jitihada kubwa zinazofanywa na TPA kwenye uwekezaji wa miundombinu ya bandari ndio zinaongeza ufanisi katika utendaji.
"Uwekezaji umeimarishaji mifumo ya bandari na matunda ya kazi hii ni kwamba msimu wa korosho ambao sasa uko mwishoni tumeweza kuhudumia meli kubwa 28" Alisema Nyathi
Nyathi aliendelea kufafanua kuwa Bandari hiyo imekuwa ikisafirisha makaa ya mawe, saruji ya kiwanda Cha Dangote Cement ambapo saruji hiyo husafirishwa kupelekwa Zanzibar na Comoro.
Naye Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Dk George Fasha alisema Bandari ya Mtwara ni Bandari ya kimkakati kwa ushoroba wa kusini.
Dk Fasha alisema mpango wa sasa ni kuanza usafirishaji wa madini ya graphite kutoka Wilaya Ruangwa Lindi,huku akisisitiza kuwa ili kuimarisha ushoroba huo TPA inaendelea kuboresha Bandari za MbambaBay ili iweze kusaidia bandari ya Mtwara kuhudumia mizigo ya Malawi na Msumbiji.
Saturday, February 10, 2024
MIZIGO YAONGEZEKA BANDARI YA MTWARA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment