Mkurugenzi mkuu wa makampuni ya IPP, DKT. Reginald Mengi amechangia
upatikanaji wa madawati katika wilaya za Bagamoyo na Handeni, ikiwa ni kumuunga
mkono Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ,DKT. John Magufuli katika
kampeni ya upatikanaji wa madawati kwa nchi nzima ambayo inaishia tarehe 30
mwezi huu.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi mchango huo katika
Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Dkt. Mengi alisema ni wajibu wakila mtanzania kuiunga
mkono serikali katika harakati za kuhakikisha kila shule inapata madawati ya
kutosha ili kuondoa adha ya kukaa chini kwa vijana wanapokuwa madarasni.
Katika mchango huo Mwenyekiti huyo wa makampuni ya IPP
amekabidhi hundi ya shilingi milioni 35 kwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji
Majid Hemed Mwanga, huku mkuu wa wilaya ya Handeni nae alikabidhiwa hundi ya
shilingi milioni 35 ikiwa ni sawa na madawati 500 kila wilaya.
Mengi amesema umoja ni nguvu, hivyo matajiri wote wakiweka
azma ya kuchangia kampeni hiyo ya madawati hakuna motto atakae kaa chini
darasani.
Wakizungumza mara baada ya kupokea msaada huo wakuu wa
wilaya hizo za Bagamoyo na Handeni wamesema wanamshukuru DKT Mengi kwa mchango
wake na kuwataka matajiri na wadau mbalimbali waige mfano huo katika kuunga
mkono juhudi za serikali.
No comments:
Post a Comment