Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Kushoto, Majid Hemedi Mwanga, akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Aliy Aliy katika mkutano uliofanyika kijiji cha Kidomole kata ya Fukayosi wilayani humo. |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo Aliy Aliy amepiga
marufuku utoaji wa hati za ardhi ikiwemo hati za kimila, katika maeneo
yanayopakana na ardhi iliyohifadhiwa kama vile Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo
(RAZABA) inayomilikiwa na wizara kilimo Zanziba, na Ranchi ya ruvu iliyopo
wilayani Bagamoyo ambayo iko chini ya umiliki wa Kampuni ya Ranchi za Taifa
(NARCO).
Mwenyekiti huyo wa Halmashauri ametoa kauli hiyo katika mkuu
maalum wa kijiji cha Kidomole kata ya Fukayosi wilayani hapa na kuongeza kuwa
afisa aridhi atakaebainika kutoa hati katika kipindi hiki ndani ya maeneo hayo
hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kusimamishwa kazi.
Kauli hiyo ya Mwenyekiti huyo imekuja kufuatia taarifa za
kuuzwa kwa baadhi ya maeneo ndani ya Ranchi hizo jambo ambalo ni kinyume na
sheria kwakuwa kampuni zinazomiliki maeneo hayo bado hazijavuliwa umiliki wake.
Aidha, amemuomba mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kuanda mpango wa
uhakiki mipaka katika maeneo hayo ili kuondoa utata uliopo baina ya Ranchi hizo
na wananchi hasa katika vijiji vinavyopakana na Ranchi hizo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majidi Hemedi
Mwanga, amewataka kuacha kuvamia maeneo yalihifadhiwa ili kuepusha usumbufu wa
kuondolewa kwa nguvu na serikali.
Majidi alitolea mfano wa maeneo yalihifadhiwa ikiwa ni
pamoja na Hifadhi za misitu, Ranchi za taifa na maeneo tengefu kwaajili ya
shughuli maalumu kama vile Barabara.
Aidha, alisema serilkali ya wilaya haitavumilia kuona
mwananchi yeyote anavamia maeneo hayo ili kujenga nidhamu ya utawala bora, haki
na utii wa sheria bila ya shuruti.
Akitoa kauli hiyo katika mikutano ya kutatua migogoro ya
aridhi wilayani hapa, mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi wenye mahitaji ya
ardhi katika vijiji kushirikiana na viongozi wa vjiji kuainisha mahitaji yao
ya aridhi ili kuona kama kuna haja ya kuomba kuongezewa ardhi kwaajili ya
matumizi ya makazi na kilimo.
Hata hivyo aliwataka viongozi wa vijiji kuelezea aridhi waliyonayo
katika vijiji vyao na wanaitumia kwa kazi ipi huku akiwataka kutoa ufafanuzi
kuhusu watu waliopewa aridhi na vijiji ili kuona kama sheria zinamefuatwa.
Alisema si vyema kuona wananchi wanatafuta aridhi na kuvamia
maeneo yaliyohifadhiwa wakati serikali ya kijiji inatoa aridhi kwa wawekezaji
bila ya kufuata taratibu za ugawaji wa ardhi.
Imeandikwa na Athumani Shomari.
No comments:
Post a Comment