JKCI YAENDELEA KUWA LULU UTALII TIBA AFRIKA
Madaktari wake waitwa Zambia kufanya upasuaji wa moyo Na Mwandishi Wetu Uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya afya umeendelea kuipaisha Tanzania ambapo sasa madakati bingwa wanne wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI wako nchini Zambia wakiendelea kufanya upasuaji wa moyo. Timu hiyo ya madakari hao itashirikiana na wenzao wa Hospitali ya Taifa ya Moyo ya Zambia na watafanyakazi upasuaji wa moyo kwa muda wa wiki moja . Mkuu wa ujumbe huo, Dk Viviane Mlawi wa (JKCI), ambaye ni daktari bingwa wa moyo kwa watoto, alisema ujumbe huo pia umeambatana na mtaalam mbobezi wa chumba cha upasuaji na mtaalamu wa usingizi katika upasuaji Moyo. Alisema wameambatana pia na mbobezi katika kuhudumia wagonjwa wa nje wanaokuja kupata matibabu Tanzania, Dk. Maiyer Msengi na wauguzi wawili ambao ni wabobezi wa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Dk Mlawi alisema malengo makubwa ya safari hiyo ni matano ambayo ni kufanya u...