Monday, August 7, 2023

MAKAMU WA RAIS AWATAKA VIJANA KUWA NA MAADIKI MEMA ILI KUJENGA UAMINIFU.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia viongozi, watoa mada pamoja na vijana mbalimbali wakati akifungua Kongamano la Vijana linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Tarehe 07 Agosti 2023.

....................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa vijana hapa nchini kujiepusha na matendo yote yasioendana na maadili ya taifa ili waweze kuaminika katika taasisi za kifedha, katika uongozi pamoja na kuwa raia wema.

 

Makamu wa Rais ametoa wito huo leo Agosti 07 2023 wakati akifungua Kongamano la Vijana la Mkoa wa Dodoma linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Amesema maadili miongoni mwa vijana wengi yameporomoka ikiwemo kukosa uadilifu na hivyo kujiingiza katika vitendo visivyofaa kama vile matumizi ya madawa ya kulevya, unyang’anyi, mapenzi ya jinsia moja, rushwa na utapeli.

 

Amesisitiza vijana wanapaswa kutambua uadilifu ni mtaji wa kuaminiwa na kufanikiwa hivyo ametoa rai kwa kongamano hilo kujadili kwa kina nafasi na wajibu wa wazazi, walezi, viongozi wa dini, kimila, vyombo vya ulinzi na usalama, vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na vijana wenyewe katika kujenga na kutunza maadili ya vijana wa Kitanzania.

 

Halikadhalika Makamu wa Rais ametoa maagizo mbalimbali kwa Halmashauri hapa nchini ili kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi ikiwemo kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya uzalishaji mali kwa vijana ikiwemo kuanzisha kongani zinazoendana na fursa zilizopo kwenye maeneo, kuwaunganisha vijana na fursa za mitaji, kuhamasisha na kusimamia urasimishaji wa vikundi vya vijana ili viweze kutambulika. 


Maagizo mengine ni pamoja na kutengeneza kanzidata ya vijana na ujuzi au taaluma zao ili kuweza kuwaunganisha na fursa mbalimbali zinazojitokeza, kuhamasisha na kuwezesha vijana kuunda klabu za mazingira na kuunganisha vijana katika uzalishaji ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kitaasisi zitakazosaidia kutoa ufumbuzi wa changamoto zao.

 

Makamu wa Rais amesema serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ina dhamira njema ya kuona vijana wa Tanzania wanaendelezwa na wanawezeshwa kushiriki katika ujenzi wa Taifa. Amesema Kutokana na dhamira hiyo serikali imeendelea kuwawezesha vijana ili kujiari, kushiriki kwenye shughuli za maendeleo na kuchangia katika pato la Taifa. 


Ameongeza kwamba katika mwaka 2022/2023, Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ulitoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.88 kwa ajili ya kuwezesha miradi 85 ya vijana katika sekta za kilimo, viwanda na biashara katika halmashauri 28. 


Aidha amesema Serikali ilitoa mafunzo ya ujasiriamali, usimamizi, kurasimisha na kuendeleza biashara kwa vijana 2,497 pamoja na kukamilisha kazi ya kuboresha Mwongozo wa Utoaji mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambapo kwa sasa unatoa mikopo kwa vijana walio katika vikundi, mtu mmoja mmoja na Kampuni.

 

Makamu wa Rais ametoa rai kwa vijana kujitokeza na kushiriki katika juhudi za kukabiliana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi kwa ajili ya maendeleo endelevu. Pia amewataka kutumia fursa zitokanazo na uhifadhi wa mazingira kama vile kuanzisha na kuendesha kampuni za ukusanyaji na uzoaji taka, uzalishaji wa funza kutokana na taka kwa ajili ya chakula cha kuku na samaki, biashara ya kaboni, uanzishaji wa vitalu na kufanya biashara ya miche ya miti na ufugaji wa nyuki.

 

Makamu wa Rais amesema Kongamano hilo linapaswa kufanyika katika Mikoa yote nchini ili kuwawezesha vijana kutambua fursa na kutafuta namna ya kutatua changamoto zinazowakabili.

 

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Deogratius Ndejembi amesema mara baada ya kupitia upya utaratibu wa utoaji wa mikopo ya asilimia kumi kutoka katika Halmashauri nchini, serikali inatarajia kuanzisha mfumo wa kielekroniki wa uombaji wa mikopo hiyo ambapo itatoa nafasi pia kwa mtu mmoja mmoja mwenye wazo zuri na lenye tija kuweza kupata mkopo pasipo kuwa na kikundi.

 

Awali akitoa taarifa kuhusu Kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema uwepo wa idadi kubwa ya vijana katika mkoa huo umepelekea kufanyika kwa kongamano hilo ili kuwakutanisha vijana hao na kuwaeleza mipango ya serikali na fursa zilizopo kwaajili ya kupata ajira na kujiajiri. 


Pia amesema kusanyiko hilo limelenga kutambua changamoto zinazowakabili vijana na kupata suluhu ya pamoja.

 

Mkuu wa Mkoa ameongeza kwamba baada ya kongamano hilo wanatarajia kupata maazimio ya namna ya kukabiliana na ukosefu wa ajira pamoja na maadili kwa vijana. Amesema kongamano hilo litasaidia katika kukamilisha mpango mkakati wa vijana kwa mkoa Dodoma unaotarajiwa kukamilika mwezi Novemba 2023. 

 

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

07 Agosti 2023

Dodoma. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasikiliza vijana waliojiajiri kupitia tehama wa Dodoma Data Tech walionufaika na mkopo wa asilimia 4 kwa vijana kupitia Halmashauri wakati akitembelea mabanda ya mbalimbali alipowasili kufungua Kongamano la Vijana linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Tarehe 07 Agosti 2023.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana mara baada ya kufungua Kongamano la Vijana linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Wengine katika picha kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Anamringi Macha, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, Naibu Waziri Tamisemi Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi, Mbunge wa Kilosa na mtoa mada wa Kongamano hilo Prof. Palamagamba Kabudi pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ally Gugu.



MAGAZETI YA LEO TAREHE 07 AGOSTI 2023.

 

















Sunday, August 6, 2023

FURSA ZA MIFUGO NA UVUVI ZAZIDI KUPAA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), (wapili kutoka kushoto) akiangalia baadhi ya mifugo iliyopo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya). Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Daniel Mushi. 

Na. Edward Kondela

Serikali imewaasa wadau wa sekta za mifugo na uvuvi kujisajili na kushiriki vyema katika Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika 2023 (AGRF) ili waweze kufungua fursa za kibiashara ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) amebainisha hayo (06.08.2023) katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, ambapo amesema tayari wizara imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuhamasisha wadau wa sekta za mifugo na uvuvi kushiriki katika mkutano huo ambao utafanyika kuanzia tarehe 5 hadi 8 Mwezi Septemba mwaka huu na unatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 3,000 kutoka ndani na nje ya nchi.


Mhe. Ulega amesema mkutano huo wa Afrika utakaofanyika jijini Dar es Salaam unatarajia kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi na kuongeza wigo wa mawasiliano ya kibiashara kwa wadau wa ndani na nje ya nchi.


Kuhusu Programu ya Kielelezo “Jenga Kesho Iliyo Bora” BBT – LIFE kwa ajili ya kuwezesha vijana kupata elimu ya vitendo katika unenepeshaji wa mifugo na viumbe vya kwenye maji, Waziri Ulega amebainisha kuwa programu hiyo inafanyika kutokana na maono na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo hadi sasa takriban vijana 240 wapo kwenye mafunzo hayo.


Ameongeza kuwa vijana wanashirikishwa katika hatua zote ikiwemo ya kujenga mabanda na kwenda minadani na kuchagua ng’ombe wazuri ambao wanaweza kunenepeshwa na namna hatua za unenepeshaji zinavyofuatwa ambapo hadi sasa ng’ombe 500 wameuzwa.


Aidha, amesema programu hiyo ilivyo ni kwamba tangu siku ya kwanza kila kijana anajua idadi ya ng’ombe atakaowasimamia na kila anapowauza ule mzunguko faida inayobaki ndiyo atakayoondoka nayo kuanzisha biashara yake na upande wa uvuvi imetolewa elimu juu ya unenepeshaji wa kaa na jongoo bahari pamoja na ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.


Pia, amesema matumaini ni kwamba Programu ya Kielelezo “Jenga Kesho Iliyo Bora” ni kupanua zaidi program hiyo na kuishusha katika ngazi ya mkoa na wilaya ili ziweze kujiendesha pamoja na kuongeza kundi la vijana kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili wapate pia mafunzo hayo.


Kuelekea Uchumi wa Buluu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), amesema serikali inaenda kuwezesha wavuvi wadogo wadogo kuingia kwenye maji marefu ili waweze kufanya huko shughuli za uvuvi.


Waziri Ulega amebainisha kuwa wavuvi hususan wadogo watawezeshwa boti kupitia mikopo isiyo na riba sambamba na kutumia fursa za uchumi wa buluu kwa kunenepesha jongoo bahari na kilimo cha mwani pamoja na uwepo wa vizimba vya kufugia samaki lengo ni kuongeza uzalishaji kupitia uchumi wa buluu kwa kuwa na ongezeko la samaki katika soko la ndani na nje ya nchi.










 

GARA LA KUBEBA MAFUTA LAPINDUKA NA KUWAKA MOTO KIMARA JIJINI DAR ES SALAAM.


Gari la kubeba mafuta limeripuka na kuwaka moto eneo la Kimara jijini Dar es Salaam barabara ya Morogoro huku moto huo ukionekana kusambaa.


Kufuatia hali hiyo taruki imetanda miongoni mwa wakazi wa eneo hilo lilipotokea ajali hiyo ya moto.


Baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo wameiambia BAGAMOYO KWANZA BLOG kuwa moto huo haukuzimwa kwa haraka hali iliyopelekea kusambaa katika maeneo ya jirani.


Inaelezwa kuwa ndani ya Gari hiyo kukikuwa na dereva  na abiria wawili ambao wakionekana kunusurika japo haikufahamika mara moja walipokimbilia.


Chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika mara moja na pia hasara iliyopatikana kutokana na ajali hiyo haikuweza kufahamika mara moja.


USHIRIKIANO NA WADAU UTACHOCHEA MIUNDOMBINU BORA NA IMARA KWA ELIMU BORA-KIKWETE

USHIRIKIANO NA WADAU UTACHOCHEA MIUNDOMBINU BORA NA IMARA KWA ELIMU BORA-KIKWETE


Kiwanda cha kutengeneza Marumaru cha KEDA kilichopo Chalinze kimetoa Boksi 1750 zenye thamani ya Shilingi Milioni 46 ikiwa ni mchango wao kwa shule za sekondari za Jakaya Mrisho Kikwete na Miono High School zilizopo katika halmashauri ya Chalinze.


Akiwashukuru wahisani hao, Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Ndugu Ridhiwani Kikwete amewahasa Wananchi kutunza Mbinu hiyo ili kudumisha shule hizo.


#KaziInaendelea #Keda #Elimu 










 

BALOZI DKT. DAU ATEULIWA UWENYEKITI BODI YA UTALII.





 

MAGAZETI YA LEO TAREHE 06 AGOSTI 2023

 




















MAPOKEZI YA CDE KAWAIDA OFISI NDOGO ZA MAKAO MAKAO MAKUU YA UVCCM TAIFA

 


UVCCM TAIFA
05 AGOSTI, 2023

📍📍 _Upanga Dar es salaam_

*

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa Ndugu Mohamed Ali kawaida (MCC) amewasili ofisi ndogo za Makao Makuu ya UVCCM Taifa ambapo anaongoza kikao cha Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa tarehe 05 Agosti, 2023.

Makamu Mwenye wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Rehema Sombi Omary (MNEC) Amewaongoza Wajumbe wa kamati ya Utekezaji pamoja na Watumishi wa Jumuiya katika mapokezi ya Ndugu Kawaida.

Imetolewa Na:

Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa

#SautiYaVijana
#MtumishiWenu
#SautiYenu
#KulindaNaKujengaUjamaa
#SisiNaMamaMleziWaWa





RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS MIPANGO NA UWEKEZAJI TANZANIA MHE.PROF. KITILA MKUMBO IKULU


 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Tanzania Mhe.Prof. Kitila Mkumbo, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha akiwa na Ujumbe wake, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Tanzania Mhe.Prof. Kitila Mkumbo (kulia kwa Rais) akiwa na Ujumbe wake walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa TUZO Maalumu ya Kupongeza “ Kwa kuendelea kuleta mageuzi ya kiuchumi kupitia Uchumi wa Buluu”, akikabidhiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Tanzania Mhe.Prof.Kitila Mkumbo,baada ya kumaliza mazungumzo na kujitambulisha alipofika Ikulu Jijini Zanzibar 


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Tanzania Mhe.Prof. Kitila Mkumbo, baada ya kumaliza mazungumzo na kujitambulisha alipofika Ikulu Jijini Zanzibar na Ujumbe wake, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar l






Saturday, August 5, 2023

UKAGUZI WA AFCON UMEENDA VYEMA – YAKUBU


 Na Eleuteri Mangi, WUSM, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw Saidi Yakubu amesema timu ya Wakaguzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) kwa maandalizi ya AFCON 2027 imemaliza ukaguzi wao vyema katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda kupitia kapeni ya EA Pamoja Bid.

Akiongea katika Kipindi cha Jambo kinachorushwa ya Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) Agosti 5, 2023 jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu Bw Yakubu amesema timu hiyo imemaliza kazi yao vizuri hapa ambapo ukaguzi wao ulianzia nchini Kenya, Uganda na Tanzania na kuhitimisha kazi yao kikao cha majumuisho kilichofanyika Zanzibar.


Maeneo mengine waliyokagua ni pamoja na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, HospitaIi ya Taifa Muhimbili, Uwanja wa Amaan Zanzibar, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Hospitali ya Mnazi Moja, Uwanja wa uwanja wa Mao Tse Tung Zanzibar pamoja na hoteli zitakazotumiwa wakati wa mashindano hayo kulingana na viwango vya CAF.


“Baada ya ziara yao hiyo Kenya, Uganda na Tanzania, walifanya mkutano wa majumuisho, Hatupo vibaya, tupo vizuri. Kinachotazamwa na wakaguzi ni pamoja na utayari wa Serikali namna ilivyojipanga katika kuhakikisha tukio hili tumelipokea, ukweli ni kwamba ziara yote hii ilikuwa inaongozwa Katibu Mkuu tayari inaonesha kwamba Serikali ipo tayari” amesema Katibu Mkuu Bw Yakubu.


Vigezo zingine ambavyo wakaguzi hao wa AFCON waliangalia ni mtiririko wa matukio kuelekea AFCON, kwa maana ya miundombinu ni lazima yote ikamilike kabla ya tarehe 31 Desemba 2025, Tanzania inajenga kiwanja kipya cha Arusha ambapo walioneshwa michoro, nyaraka zote muhimu na mapango wa mtiririko wa fedha utakavyokuwa katika kukamilisha ujenzi wa uwanja huo.