RATIBA YA LIGI KUU BARA.
Wakati wadau na mashabiki wa soka nchini wakisubiri kuanza kwa Ligi Kuu msimu wa 2023/24 bodi ya ligi hiyo nchini (TPLB) imesema ratiba ya mashindano hayo wataiachia siku mbili zijazo. Ligi Kuu inatarajia kuanza Agosti 15, huku ikishuhudiwa baadhi ya timu zilizokuwapo msimu uliopita zikikosekana, huku zikitokea mpya tatu kwa michuano hiyo. Timu za Mbeya City, Ruvu Shooting na Polisi Tanzania zilizokuwapo msimu huo, hazitakuwapo baada ya kushuka daraja, huku Tabora United, Mashujaa na JKT Tanzania zikichomoza msimu ujao. Hadi sasa timu, mashabiki na wadau wa soka nchini wanasubiria kujua rariba inatoka lini ili kujua nani anaanza na nani na wapi ili kuanza mipango na mikakati rasmi. Ofisa Habari wa bodi ya Ligi Kuu chini (TPLB), Karim Boimanda amesema hadi sasa ratiba imeshakamilika na muda wowote kuanzia kesho Jumapili au Jumatatu wataiachia rasmi. Amesema wamechelewa kuitoa kutokana na shirikisho la soka Afrika (CAF) kuchelewesha kalenda yao huku akibainisha wameboresha na huenda chan...