Tuesday, July 16, 2019

KILWA WATENGA MILIONI 16 KUINUA UBORA WA ELIMU.

Mwalimu Mshamu Ndandavale Ofisa Elimu vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kilwa akizungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG, ofisini kwake.

Mwalimu Ayub Mwakatika, Mratibu Elimu Kata ya Tingi Halmashauri ya Wilaya ya kilwa Mkoani Lindi Miongoni mwa waratibu Elimu waliopatiwa Pikipiki na Mradi wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP T)

............................................

 Na Hadija Omary, LINDI.


Serikali Wilayani kilwa Mkoani Lindi imetenga kiasi cha Tsh. Milioni 16 kwa ajili ya kuendeleza shuguli mbali mbali zilizokuwa zikifanywa na Mradi wa kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP T) ambao umekwisha muda wake ili usimamizi huo wa Ubora wa Elimu uweze kuwa Endelevu.


Hayo yameelezwa na Mwalimu Mshamu Ndandavale Ofisa Elimu vifaa na Takwimu wa Wilaya hiyo kwa niaba ya Ofisa Elimu Msingi jana Ofisini kwake alipokuwa akizungumza na Bagamoyo kwanza Blog.


Mradi huo wa kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP T) ulianza mwaka 2015 Ukiwa na malengo ya Kuinua umahiri wa KKK (kusoma kuandika na kuhesabu), kuboresha mbinu za uongozi Halmashauri, maafisa elimu kata na walimu wakuu wa Shule za Msingi pamoja na kuboresha mfumo wa utoaji wa taarifa mbali mbali katika Shule ambao unaisha muda wake July mwaka 2017.


Ndandavale alisema kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana kutoka katika Mradi huo wa kuinua Ubora wa Elimu Tanzania Halmashauri yao imeona ipo haja ya kuendeleza shughuli hizo ili kuongeza ufauru katika shule yao.


Aliongeza kuwa fedha hizo zitatoka katika vyanzo vyao vya Ndani vya mapato katika Bajeti ya 2018/2019 ambapo zitatumika kwa ajili ya kuwezesha waratibu Elimu kata mafuta na matengenezo ya Pikipiki hizo pamoja na Semina za Walimu wa Darasa la kwanza na la pili.


Aidha, Ndandavale aliongeza kuwa tokea Mradi huo umeanzishwa mwaka 2015 umekuwa na chachu kubwa katika mabadiliko ya uongozi, ushiriki wa wazazi kufuatilia taarifa za watoto wao, kupunguza utoro kwa wanafunzi, walimu kupata mbinu mbali mbali za kufundishia hali ambayo imeongeza ufaulu kwa wanafunzi kutoka asilimia 34 mwaka 2015 hadi kufikia 64% mwaka 2018.


Kwa upande wake Mwalimu Kuluthumu Mwaibasa Mratibu Elimu kata ,Kata ya Somanga alisema kuwa Mradi huo wa EQUIP T umewasaidia Waratibu Elimu Kata kufanya ufuatiliaji na ukusanyaji wa mara kwa mara wa taarifa mbali mbali jambo ambalo huwafanya kuwa na taarifa sahihi zinazohusu Shule zao katika kata husika.


Nae Mwalimu Ayubu Mwakatika Ofisa Elimu kata, Kata ya Tingi alisema kuwa hapo awali Kabla ya kupatiwa piki piki hizo walikuwa wanalazimika kutumia baiskeli ili kufanya ufuatiliaji wa taarifa mbali mbali katika shule jambo ambalo wakati mwingine wanashindwa kuzifikia Shule zingine kutokana na umbali wa Maeneo yalipo.


Alisema mara nyingine hulazimika kutumia gharama zao binafusi ili kutembelea Shule hizo hali ambayo ilikuwa inawafanya kushindwa kuzifikia mara kwa mara shule zilizopo pembezoni kutokana na kutokuwa na fedha za kutosho

Sunday, July 14, 2019

MAHDI WA PARADISE BAGAMOYO AUWAWA NCHINI SOMALIA.

Mfanyabiashara Mahad Nur Gurguurte,wakati wa uhai wake.
 
Mfanyabiashara Mahad Nur Gurguurte,wakati wa uhai wake.
.....................................

Mfanyabiashara Mahad Nur Gurguurte, wa Tanzania ambae alikuwa mmiliki wa hoteli ya Paradise Bagamoyo ameuawa katika shambulio la kigaidi nchini Somalia.


Shambulio hilo la kujitoa muhanaga limetokea ijumaa ya tarehe 12 julai 2019 katika hoteli ya Asasey iliyopo  mji  wa bandari  wa  Kismayo nchini Somalia.


Watu 26 wameripotiwa kufariki dunia katika shambulio hilo wakiwemo watanzania watatu, na wengine 56 kujeruhiwa.


Miongoni mwa watanzania watatu waliofariki ni pamoja na mmiliki wa Hoteli ya Paradise ya Bagamoyo, Mahad Nur Gurguurte na wengine wawili (2).


Aidha mbali ya kupoteza Watanzania watatu, wengine waliopoteza maisha ni raia wa Kenya watatu, Wamarekani watatu, Muingereza mmoja na Mcanada mmoja.


Watu walioshuhudia  wamesema  miongoni  mwa  waliouwawa  ni mwanaharakati  maarufu  katika  mitandao  ya  kijamii  na  mwandishi habari  wa Somalia.


Ndugu wa  mwandishi  habari Mohamed Sahal wamethibitisha  kifo chake  na kusema  kuwa  mwanaharakati  katika  mitandao  ya kijamii  Hodan Naleyeh  na  mume  wake  pia  wamefariki  katika mripuko  huo.


Chama cha  waandishi wa habari nchini  Somalia  SJS kimethibitisha kifo  cha  mwandishi  huyo.


"Ni  siku  ya masikitiko makubwa  kwa  waandishi  habari  wa  Somalia," katibu  mkuu  wa chama  hicho  Ahmed Mumin  alisema  katika  taarifa yake.


Kwa mujibu  wa  vyanzo kadhaa, wengi  wa  wale  wanaoishi katika hoteli  hiyo walikuwa  ni  wanasiasa  na  wafanyabiashara  kabla  ya uchaguzi  ujao  wa  kimkoa.

Jengo la hoteli hiyo kama linavyoonekana mara baada ya kushambuliwa.

MAGAZETI YA LEO JULAI 14, 2019.

Saturday, July 13, 2019

BAGAMOYO: MWENYEKITI WA KITONGOJI (CHADEMA) AJIUZULU, AJIUNGA CCM.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo, Abdul Rashid Zahoro (kulia) akimkabidhi kadi ya CCM mwanachama mpya, Frank Daniel Masiaga ambae alikuwa Mwenyekiti wa Kitongoji  kwa tiketi ya CHADEMA.
.............................

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyakahamba kata ya Kerege wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, kwa tiketi ya CHADEMA, Frank Daniel Masiaga amejiuzulu nafasi yake na kutangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo tarehe 13 julai 2019.


Akitangaza uamuzi huo mbele ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya ofisi ya CCM kata ya Kerege, Masiaga alisema ameamua kurudisha kadi ya CHADEMA na kuchukua kadi ya CCM kutokana na kile alichokiita ni kumuunga mkono Rais John Magufuli katika juhudi zake za kuleta maendeleo.


Alisema katika kipindi chote cha miaka mitano amekuwa Mwenyekiti wa Kitongoji kupitia Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lakini amefanya kazi katika mazingira magumu hivyo ameona ni bora ajiunge na CCM ili aweze kufanya mambo mbalimbali ya maendeleo.


Alisema ili kuweza kuleta maendeleo katika eneo lake ameona ni vyema ajiunge na CCM kwakuwa CHADEMA haiwezi kuleta maendeleo.


Masiaga alisema uamuzi wake wa kujiunga na CCM umepokelewa kwa furaha na wananchi wa kitongoji chake hali iliyopelekea wanachama 300 wa CHADEMA kurudisha kadi za CHADEMA nakujiunga na CCM.


Akizungumza mara baada ya kumpokea, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo, Abdul Rashid Zahoro amesema anampongeza Masiaga kwa kitendo chake cha kurudi nyumbani na kuwataka viongozi wa CCM kata ya Kerege kumpa ushirikiano  ili kuimarisha CCM katika kitongoji cha Nyakahamba.


Alisema CCM ni kuchapa kazi hivyo wanachama wapya hao wanapaswa kuwajibika na kuahidi kuwanunulia kadi zote mia tatu kwa fedha zake ikiwa kama motisha kwa wanachama hao wapya waliotoka CHADEMA.
 
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo, Abdul Rashid Zahoro, akionesha kadi za CHADEMA ambazo wanachama wake wamejiunga na CCM.
   
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo, Abdul Rashid Zahoro,  (kushoto) akimpongeza mwanachama mpya, 
Frank Daniel Masiaga ambae alikuwa Mwenyekiti wa Kitongoji  kwa tiketi ya CHADEMA.