Tuesday, November 13, 2018

WAFUGAJI KUFANYA UCHAGUZI NOVEMBA 30

Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi ya Chama Cha Wafugaji Tanzania, Veronica Ndetieai (kushoto) akinukuu maombo muhimu katika kikao na waandishi wa Habari kuzungumzia uchaguzi wa Chama hicho unaotarajiwa kufanyika Novemba 30, 2018.
......................................................

Na Omary Mngindo, Dakawa

CHAMA Cha Wafugaji Tanzania (CCWT), kinataraji kufanya uchaguzi wa viongozi wake wa Kitaifa, unaotarajiwa kufanyika  mwishoni mwa mwezi huu, mkoani Dodoma.

Hayo yamebainishwa mwishoni mwa wiki na Veronica Ndetiai Mwenyekiti wa Tume wa chama hicho, alipozungumza na waandishi wa habari katika Mnara wa kumbukumbu ya Edward Sokoine, Kijiji cha Sokoine, Kata ya Dakawa wilaya ya Mvomelo mkoani Morogoro.

Ndetiai alisema kuwa fomu za kuwania nafasi mbalimbali zimeanza kutolewa Ijumaa ya Nov 9, huku akiwahimiza wanachama kuchangamkia uchukuaji wa fomu hizo, ili zoezi la uchaguzi liweze kufanyika kama ilivyopangwa.

"Nafasi zitazowaniwa kwenye uchaguzi huo unaoyaraji kufanyika mkoani Dodoma ni Mwenyekiti, Makamu, Katibu Mkuu ma Msaisizi wake, Mhasibu na Wajumbe wa Kamati Tendaji," ilieleza taarifa hiyo.

Aidha tarifa ya Ndetiai imetaja sifa za wanachama ikiwa ni pamoja na kuwa mwanachama hai Kikatiba, ajeu kusoma na kuandika, mwenendo mzuri kitabia na anayekubalika, awe tayari kujitolea.

"Awe mvumilivu, msikivu na mwenye uwezo wa kutetea na kulinda maslahi ya Chama kwa uadilifu mkubwa, Katibu awe na uwezo wa kuongoza wengine," ilieleza sehemu ya taatifa hiyo.

Taarifa hiyo ikizungunzia nafasi ya Mtunza fedha, imeelezea kwa awe na uwezo wa kutunza kumbukumbu na vitabu vya fedha, mwajibikaji, mwaminifu
na ikibidi awe na taaluma ya fedha.

Ndetiai imeongeza kuwa alisema kuwa chama hicho kilichoanzishwa rasmi mwaka 2013, na kupatiwa usajili namba S.A 19186 kikiwa na malengo ya kuunganisha Wafugaji wote wa Tanzania Bara na Visiwani.

UVCCM LINDI WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI.

 Hadija Omary, Lindi.

Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa  Lindi wampongeza Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wa kununua korosho kwa bei inayomletea tija mkulima.

Akizungumza na waandishi Wa habari ofisini kwake leo Novemba 13, 2018 Wilayani Nachingwea, Mwenyekiti wa uvccm mkoa wa Lindi, Majid Lupanda, amesema hatua iliyochukuliwa na Mh. Rais, ni hatua ya kishujaa, na imeonesha wazi kuwa, ni moja ya mfulululizo wa matendo ya kishujaa yanayofanywa  na Mh. Rais, kwa maslahi mapana ya Taifa, na sio kwa maslahi binafsi.

 " Mh. Mh.Rais ameonesha ushujaa mkubwa katika hili, tunampongeza sana kwa hatua mzuri aliyoichuku ya kununua korosho kwa bei yenye tija kwa mkulima,  na tunamuoba Mungu azidi kumpa nguvu ya kuendelea kuitumikia Tanzania kwa maslahi mapana ya Taifa " alisema Luponda.

 Aidha Lupanda pia alimpongeza  Mh. Rais kwa hatua ya kufufua kiwanda cha kubangua  korosho ikiwa ni mwelekeo wa serikali katika Tanzania ya viwanda pia ni moja ya njia ya kuongeza pato kwa Taifa na chanzo cha ajira kwa vijana wa kitanzania.

Hata hivyo katika mazungumzo yake na waandishi wa habari, Mwenyekiti huyo wa uvccm mkoa, alilaani vikali wanasiasa wanajaribu kurudisha nyuma jitihada za Mh. Rais, katika kuipambania Tazanzania.

" Tunajua kuwa Mh. Rais wetu anafanya kazi mzuri sana inayompendeza Mungu, na pia kuna watu wachache wanaotumika vibaya na wasioitakia mema nchi yetu katika kuharibu ama kurudisha nyuma jitihada za Mh. Rais katika mapambano ya kuipeleka mbele nchi yetu kimaendeleo, sisi kama umoja wa vijana mkoa wa Lindi tunasema shida yetu watanzania ni maendeleo na sio makelele, "aliongeza Luponda 

Pamoja na mambo Mengine Luponda pia  aliendelea kumdhihirishia Mh. Rais kuwa umoja wa vijana mkoa wa Lindi wapo pamoja nae na  wapo tayari  kuungana na timu nzima itakayoshughulikia mchakato mzima wa ununuzi wa korosho  ikiwa kutakua na nafasi ya  vijana hao kushiriki katika zoezi hilo katika jitihada za kurahisisha zoezi hilo na kuleta ufanisi.

TIMU YA WIZARA YA KILIMO YATUA LINDI NA MTWARA KUANZA NA KOROSHO.

Waziri wa kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Evod Mmanda leo Novemba 13, 2018 mara baada ya kuwasili Mkoani humo kwa ziara ya kikazi kwa ajili ya kuhakiki Korosho zilizopo katika maghala makuu kabla ya kuanza ununuzi. (Picha Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo).
.................................

Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo, Mtwara
…………………………………………………………………………………………………
Ikiwa ni siku moja tu mara baada ya kuapishwa kuongoza wizara ya kilimo katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam Jana Jumatatu Novemba 12, 2018, Waziri wa kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) Leo Tarehe 13 Novemba 2018 ameongoza viongozi wakuu wa Wizara yake kutembelea katika Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kwa ajili ya kuhakiki Korosho zilizopo katika maghala makuu.

Katika msafara huo Waziri Hasunga atatembelea Mkoani Mtwara ambapo ameambatana na Naibu Waziri wa kilimo Mhe Innocent Lugha Bashungwa na Katibu Mkuu Mhandisi Mathew Mtigumwe watakaotembelea Mkoa wa Lindi, na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Prof Siza Tumbo atakayetembelea Mkoa wa Ruvuma.

Katika ziara hiyo viongozi hao wakuu watahakiki usimamizi wa maghala ambao kwa sasa unasimamiwa naBodi ya usimamizi wa stakabadhi ya ghala na Usimamizi wa ziada wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko.

Vilevile watahakiki taarifa za Ubora wa maghala kama zilivyopitishwa na Bodi ya usimamizi wa Stakabadhi ya ghala (Warehouse Receipt Regulatory Board-WRRB) pamoja na Ubora wa ghala.

Watahakiki uwezo wa maghala na kiasi kilichopo ghalani, na kuhakikisha taarifa ya umiliki wa Korosho zilizopo kwenye ghala.

Aidha, viongozi hao watahakiki kiasi cha Korosho kwenye ghala kwa kupitia nyaraka za mapokezi ya Korosho kwenye ghala ambazo zinawasilishwa na Vyama vya msingi (AMCOS) na kuoanisha taarifa hizo na taarifa zilizomo kwenye taarifa za stakabadhi ya ghala (Warehouse Report).

Katika ziara hiyo timu ya viongozi wakuu kutoka wizara ya kilimo wataambatana pia na Ofisini za Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Bodi ya Mazao Mchanganyiko, Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI)-Naliendele, na Bodi ya usimamizi wa Stakabadhi ya ghala (WRRB).
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) akijadili jambo na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Byakanwa leo Novemba 13, 2018, mara baada ya kuwasili Mkoani humo kwa ziara ya kikazi kwa ajili ya kuhakiki Korosho zilizopo katika maghala makuu kabla ya kuanza ununuzi.

Naibu waziri wa kilimo Mhe Innocent Lugha Bashungwa (Mb) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi kwa ajili ya kuhakikisha Korosho zilizopo katika maghala makuu kabla ya kuanza ununuzi. Mwingine pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Evod Mmanda, leo Novemba 13, 2018.

Kulia ni katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu wizara ya kilimo Prof Siza Tumbo walipowasili Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi kwa ajili ya kuhakikisha Korosho zilizopo katika maghala makuu kabla ya kuanza ununuzi leo Novemba 13, 2018.

AMANA BANK, PIL WAZINDUA MIKOPO YA VIWANJA KWA WATEJA WAO.

 Mkuu wa Kitengo cha Biashara Amana Bank, Munir Rajabu akimkabidhi zawadi Mteja wao Aisha Sfana ambae amekamilisha mkopo wake wa kiwanja katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Amana Bank jijini Dar es Salaam, anaeshuhudia katikati ni  Afisa Mkuu Mwendeshaji wa Property International Ltd. George Obado. 

  Afisa Mkuu Mwendeshaji wa Property International Ltd. George Obado, akimkabidhi hati ya kiwanja, Aisha Sfana mara baada ya kukamilisha mkopo wake Amana Bank, kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara Amana Bank, Munir Rajabu
 Mkuu wa Kitengo cha Biashara Amana Bank, Munir Rajabu, akizungumza na waandishi wa Habari katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Amana Bank Jijini Dar es Salaam, kulia ni Afisa Mkuu Mwendeshaji wa Property International Ltd. George Obado.
..................................... 

Amana Bank Ltd. kwa  kushirikiana na Property International Ltd (PIL) wanaadhimisha miaka mitatu ya ushirikiano wa kibiashara kati yao huku wakiwa wamefanikiwa kuwawezesha wateja wao zaidi ya 300 kumiliki viwanja kwa njia ya mikopo katika maeneo mbalimbali ambayo PIL imepima viwanja.

Wakizungumza katika Makao Makuu ya Amana Bank jijini Dar es Salaam, kwenye hafla fupi ya kuwakabidhi hati za viwanja wateja waliofanikiwa kukamilisha mikopo yao, Maafisa wa Amana Bank Ltd. na Property International Ltd, walisema wanayo furaha na wanajivunia ushirikiano wao ambao umewawezesha watanzania wa hali zote kumiliki viwanja.

Munir Rajabu ni Mkuu wa kitengo cha Biashara kutoka Amana Bank Ltd. amesema Amana Bank siku zote inabuni mbinu na njia rahisi za kuwawezesha wateja wao kumiliki vitu mbalimbali ikiwemo Biashara, Nyumba, Magari, Viwanja NK.

Munir alisema kuwa, katika huduma ya kuwakopesha viwanja wateja wao, Amana Bnak imekuwa ikishirikiana na Property International Ltd ambao ni wataalamu wa upimaji na umiliki wa viwanja na hivyo kurahisisha mikopo ya viwanja kupitia Benki hiyo.

Alisema wateja wanaokopeshwa viwanja bila ya riba sio tu wanafaidika na viwanja, bali wanafaidika kwa kumiliki viwanja vyenye hati ambavyo ni dhamana ya kukopa vitu vingine vitakavyowaletea maendeleo katika maisha yao.

Aliongeza kwa kusema kuwa, hiyo ni njia rahisi kwa watanzania kumiliki viwanja ikiwa ni daraja la kufikia malengo ya kibiashara na kimaendeleo kwa kujenga misngi ya uaminifu katika marejesho ya mikopo hiyo.

Aidha, aliendelea kusema kuwa, kwa namna ambavyo, Amana Bank inavyowajali wateja wake, imeamua kuongeza muda wa malipo kutoka mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu na kupunguza faida kutoka asilimia 14 hadi asilimia 12 kwa mwaka, jambo ambalo limewavutia wateja wengi na kujitokeza kuomba mikopo hiyo ya viwanja.

Munir Alifafanua kuwa, katika mkopo huo wa kumiliki viwanja, mteja anatakiwa kutanguliza asilimia ishirini ya thamani ya kiwanja alichochagua kama malipo ya awali na kuendelea kulipa kiasi kilichobaki katika kipindi kisichozidi miaka mitatu.

Alisisitiza kuwa, Amana Bank ni Benki pekee hapa nchini inayofuata sheria ya kiislamu hivyo mikopo hiyo ya viwanja pia inazingatia misingi ya sheria za kiislamu licha ya kuwa wakopaji ni wateja wa dini tofauti na hata wasiokuwa na dini.

Alisema katika sheria ya kiislamu imeruhusiwa kufanya biashara na imeharamishwa riba, kwa kulizingatia hilo Amana Bank tayari inavyo vitu inamiliki na kisha kuwakopesha wateja wake kwa kulipa kidogo kidogo kama inavyofanya kwenye viwanja kwa kushirikiana na (PIL) 

Mkuu huyo wa kitengo cha Biashara alitumia nafasi hiyo keleza kuwa, katika wiki ya huduma kwa wateja, wateja wa Amana Bank, watapata fursa ya kununua viwanja kwa punguzo maalum la bei ambapo atakuwepo mwakilishi wa (PIL) katika kipindi chote cha wiki ya huduma kwa wateja katika matawi yote ya Dar es Salaam.

Katika kipindi hicho cha wiki ya huduma kwa wateja, Munir alitoa wito kwa wateja wa Amana Bank Ltd. na watanzania kwa ujumla kutembelea matawi ya Amana Bank ili kupata fursa ya kununua viwanja kwa bei ya punguzo.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu Mwendeshaji wa Property International Ltd. George Obado alisema anafurahia ushirikiano kati yao na Amana Bank kwakuwa wameweza kuanzisha huduma hiyo rafiki kwa wateja.
"Mpango huo wa mikopo unaotekelezwa na Amana Bank ni mpango ambao una msaada mkubwa kwa mwenye kutaka kumiliki kiwanja". Alisema Obado.
Akielezea kapuni ya PIL, Obado, alisema imeanzishwa Mwezi January 2014 ikiwa inajishughulisha na upimaji wa viwanja katika maeneo mbalimbali ya Tanzania ili kuwawezesha wanunuzi wa viwanja kununua viwanja vilivyopimwa.

Alisema katika upimaji wao wa viwanja wanazingztia kanuni na sheria za mipango miji ikiwa ni pamoja kuainisha Barabara ili kurahisisha kufika kwenye makazi husika.

Alisema wananchi wengi wamekuwa wakinunua viwanja ambavyo havina hati hivyo PIL imekuja na suluhisho la kupata hati miliki ya Ardhi kwa kusimamia na kushughulikia mpaka mteja anakuwa na kiwanja chenye hati.

Aidha, Bwana Obado alitaja maeneo ambayo tayari PIL imeshapima viwanja ni Kimbiji Sea View Kigamboni, Magodani Mkuranga, Mapinduzi residence, Chekeni Farm Mwasongfa Tundwi, Fukayosi Residence Bagamoyo, The Dar es Salaam Automobile Zone, (DAZ) Riverside Residence, Coco Palms, Royal Palm Estate Mwasonga, African Palm Estate na Dege Residence. 
 
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Amana Bank, Munir Rajabu akimkabidhi zawadi Mteja wao Stephano mara baada ya kukabidhiwa hati yake ya kiwanja baada kukamilisha mkopo wake Amana Bank
anaeshuhudia katikati ni  Afisa Mkuu Mwendeshaji wa Property International Ltd. George Obado.
     Mkuu wa Kitengo cha Biashara Amana Bank, Munir Rajabu akimkabidhi zawadi Mteja wao Nora Laizer, mara baada ya kukabidhiwa hati yake ya kiwanja baada kukamilisha mkopo wake Amana Bank
anaeshuhudia katikati ni  Afisa Mkuu Mwendeshaji wa Property International Ltd. George Obado.


 Hafla hiyo ilipambwa na keki inayoonyesha miaka mitatu ya ushirikiano wa kibiashara kati ya Amana Bank Ltd. na Property International Ltd.
 Wateja wa Amana Bank na PIL wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kukamilisha mikopo yao na kukabidhiwa rasmi hati za viwanja vyao, hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Amana Bank Jijini Dar es Salaam, katika picha hizo anaeonekana upande wa kulia ni Afisa Mkuu Mwendeshaji wa Property International Ltd. George Obado. 
    Afisa Mkuu Mwendeshaji wa Property International Ltd. (PIL) George Obado, akionyesha kipeperushi kinachoelezea huduma zinazotolewa na PIL.
 
Meneja Mkuu wa Biashara wa Amana Bank, Dasu Musa, (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja wa Tawi la Tandamti, Juma Yamlinga, kushoto, mara baada ya kumaliza hafla hiyo fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Amana Bank.
 Picha ya pamoja kati ya Maafisa wa Amana Bank Ltd, na wale wa Property International Ltd. (PIL) pamoja na wateja wao watatu waliokabidhiwa hati za viwanja vyao Novemba 12, 2018. Shughuli iliyofanyika Makao Makuu ya Amana Bank Jijini Dar es Salaam.

 Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya Habari wakichukua kumbukumbu ya tukio hilo.

RC SONGWE ATOA SULUHU MGOGORO WA UCHIMBAJI MADINI

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus E. Mwangela akikagua shughuli za wachimbaji wadogo wa madini Wilayani Songwe ambapo ameagiza Ofisi ya Madini kuwatembelea wachimbaji na kuwapa elimu kuhusu sheria na taratibu za uchimbaji wa madini.
...................................

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus E. Mwangela akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wamesuluhisha mgogoro baina ya wakazi wawili wa kijiji cha Saza Wilaya ya Songwe kuhusu eneo la uchimbaji wa madini.

Brig. Jen. Mwangela amesema Suzan Karan amebainika kisheria kuwa ni mmiliki halali wa eneo lililokuwa likigombewa kwa kuwa ana leseni halali huku Elimbotwa Naftari ambaye hana leseni na amekuwa akidai umiliki wa eneo hilo amebainika kuendesha shughuli za uchimbali kinyume na sheria.

“Sheria inamtambua Suzan kama mmliki halaki kwakuwa anayo leseni na amefuata taratibu na sheria za uchimbaji madini, tunashauri Elimbotwa kama atataka kuendelea kuchimba madini katika eneo hilo basi akubaliane na Suzan kufanya naye kazi”, amesisitiza.

Ameongeza kuwa serikali za vijiji hazina mamlaka ya kuwapa vibali vya uchimbaji wawekezaji wa madini bali leseni na vibali vyote vya uchimbaji wa madini hutolewa na ofisi za madini Wilaya, mkoa au kanda, hii inatokana na kuwa serikali ya kijiji ilimtambua Elimbotwa kama mmiliki wa eneo la uchimbaji kinyume na sheria.

Kwa upande wake Elimbotwa amesema anamtambua Suzan kama mmliki halali wa eneo walilokuwa wakiligombania isipokuwa sasa anadai fidia ya zaidi ya shilingi milioni 190 ikiwa ni gharama ya vitu alivyowekeza kabla ya Suzan kupewa leseni ya eneo hilo.

Naye Suzan ameupongeza uongozi wa Mkoa kwa kutoa suluhu ya mgogoro huo kutokana na kuwa ulipelekea kusimama kwa shughuli za uchimbaji na hivyo kuathiri uchumi wake.

Aidha Brig. Jen. Mwangela ameagiza Takukuru, TRA na taasisi zinazoweza kufanya ukaguzi, zihakiki madai ya Elimbotwa kama ni halisi ili Suzan aweze kuyalipa.

Imeelezwa kuwa baadhi ya migogoro ya haki ya kumiliki maeneo ya uchimbaji wa madini mkoani Songwe inasababishwa na ukiukwaji wa taratibu na sheria za madini unaofanywa na baadhi ya watendaji na wachimbaji.

MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI MKUBWA WA MAJI WA MWANGA, SAME NA KOROGWE.

Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) akitoa maelezo kuhusu mradi mkubwa wa maji wa Mwanga, Same na Korogwe kwa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.Mradi huo utanufaisha zaidi ya wananchi 438,000.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Mwanga, Same na Korogwe. Kulia ni Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa, akifuatiwa na Mhe. Mathayo David na Mhe. Jumanne Magembe (Mb) Mbunge wa Mwanga.
........................................
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) leo wameshiriki hafla ya kuweka jiwe la msingi wa mradi mkubwa wa maji wa Mwanga, Same na Korogwe. Hafla hiyo imefanyika katika chanzo cha mradi huo wilayani Mwanga, katika mkoa wa Kilimanjaro.

Mhe. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiongea kabla ya kuweka jiwe la msingi amewataka wananchi kuwa walinzi wa miradi ya maji kwasababu miradi hiyo inajengwa kwa ajili yao, hivyo wanawajibu wa kuitunza ili iwe indelevu.  Makamu wa Rais amefafanua kuwa vyanzo vya maji vinatakiwa kulindwa na kutunzwa ili miradi ya maji inayojengwa iwe indelevu na kutoa huduma ya uhakika kwa wananchi.

Awali, akimkaribisha Makamu wa Rais, Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wananchi wa vijiji 38 vinavyopitiwa na mradi huo kupata huduma ya majisafi na salama.

Waziri Mbarawa amesema kuwa mradi huo umegawanyika katika awamu mbili, ambapo hivi sasa utekelezaji upo awamu ya kwanza iliyogawanyika katika maeneno matatu na utagharimu kiasi cha shilingi milioni 336.4 na katika hatua ya kwanza mkandarasi  ameshalipwa kiasi cha Dola za Marekani milioni 20 na ujenzi umefika asilimia 76 ikihusisha ujenzi wa miundombinu ya kuzalisha maji, ikiwamo dakio la maji, 
mfumo wa kutibu maji pamoja na tanki. 

Ameongeza kuwa awamu ya pili yenye gharama ya kiasi cha Shilingi milioni 80.6 inahusu usambazaji maji kwenda Same kwa ujenzi wa bomba kubwa,  matanki mawili moja likiwa na uwezo wa lita za ujazo milioni 9 na jingine lita za ujazo milioni 7, na matanki madogo. Kazi hii hadi sasa imetekelezwa kwa asilimia 50 na mkandarasi ameshalipwa kiasi cha Dola za Marekani milioni 18.

Waziri Mbarawa amesema awamu ya tatu ni usambazaji wa maji Mwanga  kwa gharama ya Shilingi milioni 106.89 na kuainisha kuwa awamu hii imechelewa kwasababu mkandarasi aliyepatikana awali hakuwa na viwango vinavyostahili.

Mradi wa maji wa Mwanga, Same na Korogwe unatekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na taasisi za kifedha kutoka nchi za Kiarabu ikiwemo Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Uchumi wa Afrika( BADEA), Mfuko wa Maendeleo wa Opec (OFID), Mfuko wa Maendelo wa Saudia (SFD), na Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (KFD).

MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 13, 2018.