WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA, CRDB BAGAMOYO WAKATA KEKI PAMOJA NA WATEJA WAO.

 

WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA, CRDB BAGAMOYO WAKATA KEKI PAMOJA NA WATEJA WAO.


Benki ya CRDB tawi la Bagamoyo imesherehekea wiki ya huduma kwa pamoja na wateja wake waliofika kupata huduma siku ya leo jumatano tarehe 07 Oktoba 2026.


Akizungumza wakati wa kuwakaribisha wateja katika hafla hiyo fupi Kiongozi wa timu ya mauzo na huduma, Sigsbert Mapunda, amesema CRDB inaungana na watoa huduma kote nchini kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja.


Amesema wanayo furaha kushiriki sherehe hiyo pamoja wateja wao waliowahi kufika asubui na mapema huku wateja wote wataoendelea kuja watapata keki na vinywaji ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha sherehe hiyo.


Akizungumza kwa niaba ya wateja walioshuhudia hafla hiyo, mfanyabiashara maarufu mjini Bagamoyo Mama Diha amesema wao kama wateja wa CRDB wamefurahi kwa kuthaminiwa na kupewa nafasi ya kushiriki pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB Bagamoyo.


Mama Diha amesema wamekuwa wakifika katika Benki hiyo kupata huduma za kutoa na kuweka lakini tofauti leo imekuwa ni siku ya kufurahi, kula na kunywa jambo ambalo limewavutia wateja wengi waliofika kupata huduma katika Benki hiyo.



Wateja waliofika katika Benki ya CRDB Tawi la Bagamoyo siku ya leo jumatano tarehe 07 Oktoba 2026 kwa nyakati tofauti wameweza kukaribishwa na kujipatia keki, soda pamoja na maji huku wale waliowahi kufika waliweza kufungua  shampeni na kuinywa pia.


Wiki ya Huduma kwa Wateja ni tukio linaloangazia umuhimu wa utoaji wa huduma bora kwa wateja na nafasi ya watoa huduma katika kujenga uhusiano mzuri na wateja.


Maadhimisho hayo yanatoa fursa kwa taasisi na mashirika mbalimbali kutafakari namna ya kuboresha huduma zao, kuongeza ubunifu na kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakidhi matarajio ya wateja.



Benki ya CRDB inaadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kauli mbiu ya “The Extra Mile”, inayoakisi falsafa ya Benki hiyo ya kwenda hatua moja zaidi katika kuwahudumia Wateja wake.






Comments

Popular posts from this blog

RPC PWANI, AANGALIA ATHARI ZA ULISHAJI WA MIFUGO ENEO LA CHAURU.

CHALINZE KUPELEKA MILIONI 80, KUJENGA VYUMBA VYA MADARASA TALAWANDA.

WAZEE WAASWA KUWA MBELE KATIKA KUHAMASISHA USHIRIKI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

MBUNGE MARIAM IBRAHIM KUCHELE AWAPIGA JEKI YA MRADI WA PIKIPIKI WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI

WAISLAMU SAADANI WAOMBA MSAADA KUJENGEWA MSIKITI.

WAZIRI MCHENGERWA NA MHE.MARIAM IBRAHIM WASHUSHA NEEMA KWA WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI

SOLA NA KOMPYUTA ZA GURUMO ZAMPA SOMO RIDHIWANI.

TUWASA YABORESHA UTOAJI HUDUMA KWA WATEJA

MATOKEA DARASA LA SABA 2018 HAYA HAPA.