DKT. TULIA: WANAWAKE WASHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA MAAMUZI.

 

DKT. TULIA: WANAWAKE WASHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA MAAMUZI.



Na Mwandishi Wetu - MAELEZO, ARUSHA, 


Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson, amezitaka nchi wanachama kuhakikisha usawa wa kijinsia hauishii katika kuongeza idadi ya wanawake, bali uwape ushawishi na madaraka katika ngazi za maamuzi.


Akizungumza katika Mkutano wa 153 wa IPU - Jukwaa la Wanawake katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), Dkt. Tulia amesema katika kipindi chake cha uongozi IPU imefanya marekebisho ya Katiba na Kanuni zake kwa lengo la kuimarisha usawa wa kijinsia katika ngazi mbalimbali.


Amesema IPU pia imepitisha kwa mara ya kwanza Sera ya Kupinga Unyanyasaji katika Mikutano na Matukio, inayokataza aina zote za unyanyasaji, ikiwemo wa kingono, pamoja na kuweka mifumo ya kuripoti na kushughulikia vitendo hivyo.


Dkt. Tulia amesisitiza kuwa wanawake wanapaswa kuwa na nafasi ya kushiriki kikamilifu katika kufanya maamuzi, akisema, “Tunapaswa kuhakikisha kwamba usawa wa kijinsia unaenda sambamba na uwakilishi, ushiriki na fursa sawa za uongozi na kufanya maamuzi,” amesema Dkt. Tulia.


Aidha, amewataka washiriki wa mkutano huo kurejea katika nchi zao na kupeleka maazimio, mipango ya utekelezaji na mikakati ya usawa katika mabunge yao, huku wanaume wakishirikishwa kama wadau muhimu katika kufanikisha usawa huo.


Amesisitiza pia umuhimu wa kuwapa nafasi wanawake vijana, wanawake kutoka jamii zilizotengwa na wanawake wenye ulemavu kushiriki katika uongozi na kufanya maamuzi.






Comments

Popular posts from this blog

RPC PWANI, AANGALIA ATHARI ZA ULISHAJI WA MIFUGO ENEO LA CHAURU.

WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA, CRDB BAGAMOYO WAKATA KEKI PAMOJA NA WATEJA WAO.

CHALINZE KUPELEKA MILIONI 80, KUJENGA VYUMBA VYA MADARASA TALAWANDA.

WAZEE WAASWA KUWA MBELE KATIKA KUHAMASISHA USHIRIKI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

MBUNGE MARIAM IBRAHIM KUCHELE AWAPIGA JEKI YA MRADI WA PIKIPIKI WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI

WAISLAMU SAADANI WAOMBA MSAADA KUJENGEWA MSIKITI.

WAZIRI MCHENGERWA NA MHE.MARIAM IBRAHIM WASHUSHA NEEMA KWA WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI

SOLA NA KOMPYUTA ZA GURUMO ZAMPA SOMO RIDHIWANI.

TUWASA YABORESHA UTOAJI HUDUMA KWA WATEJA

MATOKEA DARASA LA SABA 2018 HAYA HAPA.