SPIKA WA UINGEREZA AMPENDEKEZA ZUNGU KUWA RAIS WA MKUTANO WA 153 WA IPU

 

SPIKA WA UINGEREZA AMPENDEKEZA ZUNGU KUWA RAIS WA MKUTANO WA 153 WA IPU


Na Mwandishi wetu


Katika hali inayoonesha kuwa mataifa makubwa duniani yameendelea kuonesha imani kubwa kwa Tanzania, Spika wa Bunge la Wawakilishi la Uingereza (House of Commons) Mhe. Sir Lindsay Hoyle, amempendekeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Rais wa Mkutano wa 153 wa Umoja Mabunge Duniani (IPU).


Sir Lindsay amempendekeza Spika Zungu leo Oktoba 6, 2026 asubuhi wakati wa kikao ambapo awali, Rais wa IPU Mhe. Dkt. Tulia Ackson aliwaeleza wajumbe kuwa wanapaswa kumchagua Rais wa Mkutano huo wa 153 unaoendelea jijini Arusha.


Baada ya maelezo ya Dkt. Tulia kuhusu kumchagua Rais wa mkutano huo, Spika wa   Bunge Bunge la Wawakilishi la Uingereza Mhe. Sir Lindsay Hoyle alitoa hoja na kumpendekeza Spika Zungu.


“Ninayo furaha na heshima kubwa ninampendekeza Spika wa Tanzania achaguliwe kuwa Rais wa Mkutano wa 153. Ninapenda kusema kuwa urafiki huenda mbali, urafiki ni wa ndani na ndio maana ni heshima kubwa kuwa naweza kumpendekeza  Spika kutoka Tanzania”, alieleza Spika Lindsay na kutoa hoja.


Pendekezo hilo liliunggwa mkono na mjumbe kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na mjumbe kutoka Uganda na hatimaye kuunwa mkono na wajumbe wote wa kikao hicho.


Akionea baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Mkutano wa 153 wa IPU, Mheshimiwa Zungu aliwashukuru wajumbe kwa kumchagua na kueleza kwamba amekubali kushika nafasi hiyo kwa moyo mmoja.


“Mheshimiwa Rais wa IPU na wajumbe wote wa Mkutano huu, kwa moyo wa dhati, nawashukuru wajumbe wote, Tanzania inajivunia kuwakaribisha jijini Arusha na tutaendelea kuwa pamoja katika mkutano huu wa 153 wa IPU” amesema.


Kwa upande wake, Rais wa IPU na Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania alimpongeza Mhe. Zungu kuwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Mkutano huo wa 153 wa IPU.

Comments

Popular posts from this blog

RPC PWANI, AANGALIA ATHARI ZA ULISHAJI WA MIFUGO ENEO LA CHAURU.

WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA, CRDB BAGAMOYO WAKATA KEKI PAMOJA NA WATEJA WAO.

CHALINZE KUPELEKA MILIONI 80, KUJENGA VYUMBA VYA MADARASA TALAWANDA.

WAZEE WAASWA KUWA MBELE KATIKA KUHAMASISHA USHIRIKI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

MBUNGE MARIAM IBRAHIM KUCHELE AWAPIGA JEKI YA MRADI WA PIKIPIKI WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI

WAISLAMU SAADANI WAOMBA MSAADA KUJENGEWA MSIKITI.

WAZIRI MCHENGERWA NA MHE.MARIAM IBRAHIM WASHUSHA NEEMA KWA WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI

SOLA NA KOMPYUTA ZA GURUMO ZAMPA SOMO RIDHIWANI.

TUWASA YABORESHA UTOAJI HUDUMA KWA WATEJA

MATOKEA DARASA LA SABA 2018 HAYA HAPA.