WAZIRI CHONGOLO: BEI YA PEMBEJEO ISIUMIZE WAKULIMA

 


WAZIRI CHONGOLO: BEI YA PEMBEJEO ISIUMIZE WAKULIMA


Na Allan Kitwe, Tabora


WAZIRI wa Kilimo Daniel Chongolo ameeleza kuwa malalamiko ya wakulima wa tumbaku ya kuuziwa pembejeo kwa bei ya juu ikilinganishwa na bei halisi ya zao hilo inapaswa kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo ili isiwaumize.


Waziri ametoa kauli hiyo hivi karibuni alipokuwa akiongea na Viongozi wa Ushirika, wadau wa kilimo na wakulima wa tumbaku kutoka Wilaya za Sikonge, Uyui, Nzega na Manispaa Tabora katika ukumbi wa Themi Hill Sekondari Mjini hapa.


Ameeleza kuwa dhamana aliyopewa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo ni kuhakikisha changamoto zozote zinazogusa maisha ya wakulima zinatatuliwa haraka iwezekanavyo.


Waziri Chongolo amesisitiza kuwa kilio cha wakulima wa tumbaku juu ya pembejeo kuwa juu kinapaswa kufanyiwa kazi, msimu uliopita wakulima wengi waliuza kwa bei ya hasara hali iliyopelekea sintofahamu kubwa miongoni mwao.


‘Najua, mbolea za pembejeo zimeshaanza kusambazwa katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya msimu mpya, ila nimeambiwa bei bado ni ile ile, nataka ipungue ili isimuumize mkulima, Bodi ya Tumbaku na TCJE lifanyieni kazi’, ameeleza.


Mheshimiwa Waziri amebainisha kuwa mikataba ya ununuzi na uuzaji wa zao hilo nayo haiko wazi, haielezi jinsi pande zote zinavyoweza kuwajibika punde mmoja anapoenda kinyume na mkataba wake, na kudokeza kuwa anataka haki itendeke.  


‘Nataka mikataba yote ya ununuzi wa zao hili iwe wazi na ilinde haki ya pande zote mbili, kinyume na hapo mkulima ataendelea kuibiwa haki yake, na mimi siko tayari kuona mkulima anaonewa, haki na wajibu vinaenda sambamba’, ameongeza.


Kuhusu madeni ya wakulima, Waziri ameeleza kuwa tayari walishakubaliana, kila kampuni kulipa fedha za wakulima kabla msimu mpya haujaanza, na kuonya kuwa hakuna mnunuzi anayedaiwa atakayeruhusiwa kununua msimu huu.


Aidha amebainisha kuwa yupo tayari kutenga bajeti kwa ajili ya kueneza teknolojia mpya ya ukaushaji tumbaku itakayoleta tija kwenye kilimo cha zao hilo huku akisisitiza kuwa kupanda mti sio mbadala wa kukata mti, bali kulinda na kuhifadhi misitu.


Waziri Chongolo ameonya Maafisa wa Wizara hiyo na Watendaji wa Bodi ya Tumbaku wanaotumia lugha zisizofaa kwa wakulima pale wanapolalamikiwa kutotatua kero zao, huku akiahidi kuchukua hatua stahiki kwa watakaobainika kwenda kinyume.


Comments

Popular posts from this blog

RPC PWANI, AANGALIA ATHARI ZA ULISHAJI WA MIFUGO ENEO LA CHAURU.

WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA, CRDB BAGAMOYO WAKATA KEKI PAMOJA NA WATEJA WAO.

CHALINZE KUPELEKA MILIONI 80, KUJENGA VYUMBA VYA MADARASA TALAWANDA.

WAZEE WAASWA KUWA MBELE KATIKA KUHAMASISHA USHIRIKI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

MBUNGE MARIAM IBRAHIM KUCHELE AWAPIGA JEKI YA MRADI WA PIKIPIKI WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI

WAISLAMU SAADANI WAOMBA MSAADA KUJENGEWA MSIKITI.

WAZIRI MCHENGERWA NA MHE.MARIAM IBRAHIM WASHUSHA NEEMA KWA WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI

SOLA NA KOMPYUTA ZA GURUMO ZAMPA SOMO RIDHIWANI.

TUWASA YABORESHA UTOAJI HUDUMA KWA WATEJA

MATOKEA DARASA LA SABA 2018 HAYA HAPA.