WAISLAMU SAADANI WAOMBA MSAADA KUJENGEWA MSIKITI.

 

WAISLAMU SAADANI WAOMBA MSAADA KUJENGEWA MSIKITI.


Na Omary Mngindo, Saadani



WAISLAMU Msikiti wa Masjid Bilal uliopo Kijiji cha Saadan National Park, Kata ya Mkange Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wanaomba msaada wa kuukarabati Msikiti wao ili waweze kufanya ibada kwa utulivu.


Msikiti huo wa Kale ambao umejengwa na Wakoloni miaka 200 iliyopita kwa sasa umechakaa hivyo waumini hao wameanza kuukarabati kwa nguvu zao wenyewe.


Imamu wa Msikiti huo Maalimu Kitoro Fundi Chande alisema kuwa Msikiti huo umedumu kwa miaka mingi, hatua ambayo inapaswa kufanyiwa ukarabati.


"Huu Msikiti umejengwa na Wakoloni miaka 200 iliyopita tunaendelea na kuswali, lakini kwa sasa unastahili kufanyiwa ukarabati," alisema Imamu Kitoro.


Aliongeza kuwa "Tunahitaji Mabati, Mbao, rangi, Vigae (Tiles sehemu za kuchukulia udhu) na vifaa mbalimbali vitakavyofanikisha kuboreshwa kwa Msikiti wetu," alisema Kitoro.


Kwa upande wake Muumini msikitini hapo Ally Majimengi alisema kuwa ukarabati wa Msikiti huo kuna umuhimu kutokana na uchakavu wake.


"Kama unavyouona Msikiti wetu una miaka mingi, ambao umejengwa na Wakoloni miaka hiyo tunawashukuru sana kwani tunaendelea na Ibada," alisema Majimengi.


Nae fundi anayejenga Msikiti huo Juma Katelema Maarufu Fundi Ngosha alisema kuwa ujenzi unaendelea huku akigusia uhitaji wa vifaa.


"Kama alivyozungumza Imamu Kitoro ujenzi unaendelea lakini kuna upungufu wa baadhi ya vifaa ikiwemo bati, mbao, saruji na vifaa vingine," alisema Ngosha.





Comments

Popular posts from this blog

RPC PWANI, AANGALIA ATHARI ZA ULISHAJI WA MIFUGO ENEO LA CHAURU.

CHALINZE KUPELEKA MILIONI 80, KUJENGA VYUMBA VYA MADARASA TALAWANDA.

WAZIRI MCHENGERWA NA MHE.MARIAM IBRAHIM WASHUSHA NEEMA KWA WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI

SOLA NA KOMPYUTA ZA GURUMO ZAMPA SOMO RIDHIWANI.

I-NEC YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA UCHAGUZI

TUWASA YABORESHA UTOAJI HUDUMA KWA WATEJA

VEDMA KUCHONGA BARABARA KIMANGE - PONGWE MNAZI

MATOKEA DARASA LA SABA 2018 HAYA HAPA.