MBUNGE MARIAM IBRAHIM KUCHELE AWAPIGA JEKI YA MRADI WA PIKIPIKI WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI

 



MBUNGE MARIAM IBRAHIM KUCHELE AWAPIGA JEKI YA MRADI WA PIKIPIKI WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI


Na mwandishi wetu ,Pwani 

 

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani ,Mhe Mariam Ibrahimu  katika  kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwakomboa wanawake kujikwamua  kiuchumi  ameamua kutoa pikipiki zipatazo 10 kwa umoja wa wanawake Tanzania  (UWT) Mkoa wa Pwani ikiwa ni moja ya mradi ambao utawasaidia kuondokana na wimbi la umasikini.


Akikabidhi pikipiki hizo kwa uongozi wa UWT Mkoa wa Pwani wakati wa halfa ambayo imefanyika katika viwanja vya nje ya  Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha ambapo amebainisha kwamba wa pikipiki hizo zitakwenda kuwa ni mkombozi mkubwa na kuwaletea mabadiliko na mageuzi katika kuachana na dhana ya kuwa tegemezi  kila kukicha na badala yake  wajitegemee wao wenyewe.


Aidha amebainisha kwamba  lengo lake kubwa sio kujinufaisha yeye mwenyewe bali ni kusaidia jamii na jumuiya mbali mbali ambapo katika kutimiza ahadi zake  pia ametoa vifaa vyenye thamani ya milioni 20  kwa ajili ya   kumalizia mradi wa ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa UWT ngazi ya Mkoa wa Pwani.


"Nimeamua kutumia  fedha zangu za mshahara  kwa ajili ya kusaidia  wanawake  wa Mkoa wa Pwani ambapo nimekabidhi pikipiki  kumi ambazo zitasaidia jumuiya za wanawake katika Wilaya zote na kwamba ni mradi ambazo  utaweza  kuwakomboa  katika kujikwamua kiuchumi na kuachana na kuwa  tegemezi na vifaa  vya ujenzi wa nyumba   vyenye thamani ya shilingi  milioni 20  ,"amebainisha Mh.Mariam  


Kwa upande  wake Mwenyekiti  wa  UWT  Mkoa  wa  Pwani  Zainabu  Vullu  amesema  kwamba mikakati  ambayo wamejiwekea ni kuondokana na kuwa tegemezi na kwamba lengo kubwa  ni  kuwa na miradi mbali mbali ya  maendeleo ambayo  itakuwa na tija zaidi katika kuwasaidia wanawake.


Naye Katibu wa UWT Mkoa wa Pwani  Aziza  Omary amempongeza kwa dhati Mbunge huyo wa viti maalumu ambaye pia ni mjumbe wa baraza kuu la  UWT Taifa amempongeza kwa kwa dhati kwa kutoa mradi wa pikipiki hizo  kumi pamoja na vifaa vya ujenzi wa nyumba ya mtumishi  wa UWT ngazi ya Mkoa  vyenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 20.


Mradi wa pikipiki hizo kumi ambazo zitakwenda kuwa mkombozi katika  jumuiya zote za UWT   ngazi ya Wilaya  pamoja na ngazi ya Mkoa   zitakwenda kuwa chachu na  kuleta matokeo chanya katika kuwakwamua kiuchumi  wananawake  wa Mkoa wa Pwani.


                                       

Comments

Popular posts from this blog

RPC PWANI, AANGALIA ATHARI ZA ULISHAJI WA MIFUGO ENEO LA CHAURU.

CHALINZE KUPELEKA MILIONI 80, KUJENGA VYUMBA VYA MADARASA TALAWANDA.

WAZIRI MCHENGERWA NA MHE.MARIAM IBRAHIM WASHUSHA NEEMA KWA WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI

SOLA NA KOMPYUTA ZA GURUMO ZAMPA SOMO RIDHIWANI.

VEDMA KUCHONGA BARABARA KIMANGE - PONGWE MNAZI

I-NEC YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA UCHAGUZI

MATOKEA DARASA LA SABA 2018 HAYA HAPA.

TUWASA YABORESHA UTOAJI HUDUMA KWA WATEJA