RPC PWANI, AANGALIA ATHARI ZA ULISHAJI WA MIFUGO ENEO LA CHAURU.

 

RPC PWANI, AANGALIA ATHARI ZA ULISHAJI WA MIFUGO ENEO LA CHAURU.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Salim Morcase, amefanya ziara katika eneo linalolalamikiwa na Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU), kwa lengo la kujionea athari zilizosababishwa na ulishaji wa mifugo katika eneo hilo pamoja na uharibifu wa miundombinu ya umwagiliaji.


Katika ziara hiyo, Kamanda Morcase amepita katika maeneo mbalimbali yanayolalamikiwa na wakulima na kujionea hali halisi ya uharibifu unaodaiwa kusababishwa na mifugo kuingia katika mashamba na maeneo ya umwagiliaji.


Aidha, amesikiliza maelezo kutoka kwa viongozi wa Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) pamoja na wakulima kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo, ikiwemo uharibifu wa miundombinu na athari zinazotokana na mifugo kuingia katika maeneo ya kilimo.


Kamanda Morcase amesisitiza umuhimu wa pande zote kuheshimu maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji, huku akieleza kuwa Jeshi la Polisi 

litaendelea kushirikiana na viongozi wa Serikali na wadau mbalimbali katika kuhakikisha changamoto hizo zinapatiwa ufumbuzi kwa kuzingatia sheria za nchi.



Katika ziara hiyo aliambatana na Mkuu wa oparesheni Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi wa Polisi Boniface Mwakalagsye ikiwa ni mwendelezo na juhudi za Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani katika kusikiliza kero za wananchi, kuzuia migogoro na kuhakikisha usalama na utulivu unaendelea katika jamii.







Comments

Popular posts from this blog

CHALINZE KUPELEKA MILIONI 80, KUJENGA VYUMBA VYA MADARASA TALAWANDA.

WAZIRI MCHENGERWA NA MHE.MARIAM IBRAHIM WASHUSHA NEEMA KWA WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI

SOLA NA KOMPYUTA ZA GURUMO ZAMPA SOMO RIDHIWANI.

I-NEC YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA UCHAGUZI

TUWASA YABORESHA UTOAJI HUDUMA KWA WATEJA

VEDMA KUCHONGA BARABARA KIMANGE - PONGWE MNAZI

MATOKEA DARASA LA SABA 2018 HAYA HAPA.