WAZIRI MCHENGERWA NA MHE.MARIAM IBRAHIM WASHUSHA NEEMA KWA WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI
WAZIRI MCHENGERWA NA MHE.MARIAM IBRAHIM WASHUSHA NEEMA KWA WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI
Na Mwandishi wetu , Pwani
Waziri wa Afya Mohamed Mchengerwa katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassaan katika kuwakomboa wanawake na kuimarisha jumuiya zao ameamua kuchangia kiasi cha shilingi milioni 35 kwa ajili ya kuwasaidia umoja wa wanawake wa (UWT) Mkoa wa Pwani waweze kukamilisha malengo yao waliyojiwekea ikiwemo suala la ujenzi wa nyumba za makatibu wa Wilaya na ngazi ya Mkoa.
Mchengerwa ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (MNEC ) Taifa ameyabainisha hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kikao cha baraza la kawaida la UWT Mkoa wa Pwani ambalo limehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama pamoja na viongozi wa serikali akiwemo Mkuu mpya wa Mkoa wa Pwani.
Mchengerwa amebainisha kwamba lengo lake kubwa ni kuendelea kutoa sapoti kwa kuweza kuwasaidia kwa hali na mali wanawake wa jumuiya hiyo ya UWT ikiwemo kuwapatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya nyumba za makatibu kuanzia ngazi ya Mkoa pamoja na ngazi za Wilaya.
"Nimefarijika sana kualikwa katika kikao hiki cha baraza la kawaida la UWT Mkoa wa Pwani na nimechangia kiasi cha shilingi milioni 35 na laki moja kwa ajili ya kuwasaidia wanawake hao katika mambo mbali mbali ikiwemo miradi ya ujenzi wa nyumba za makatibu wa UWT ngazi za Wilaya na ngazi ya Mkoa na mimi nitapenda sana kuona wanawake mnajikomboa kiuchumi,"amebainisha Waziri Mchengerwa.
Aidha Mchengerwa amewahimiza wanawake wa Mkoa wa Pwani kuachana na tabia ya kuwa wanafiki na badala yake amewataka kuhakikisha kwamba wanaweka misingi imara ya kutunza amani ya nchi ikiwa sambamba na kushikamana kwa pamoja kwa lengo la kuweza kuimarisha jumuiya yao pamoja na chama kwa ujumla.
Naye Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani Mhe. Mariam Ibrahimu katika kuwakomboa wanawake hao kiuchumi ametoa pikipiki zipatazo kumi kwa ajili ya kuendeshea kama mradi ambazo kati ya hizo nane zitakwenda kusaidia katika ngazi za Wilaya zote za UWT pamoja na nyiingine mbili zitakwenda katika ofisi na UWT Mkoa na nyingine ofsini kwa wilaya zote za Mkoa wa Pwani
"Nimeamua kutumia fedha zangu za mshahara kwa ajili ya kusaidia wanawake wa Mkoa wa Pwani ambapo nimekabidhi pikipiki kumi zitakazosaidia jumuiya za wanawake katika Wilaya zote na kwamba ni mradi ambazo utaweza kuwakomboa katika kujikwamua kiuchumi na kuachana na kuwa tegemezi na vifaa vya ujenzi wa nyumba vyenye thamani ya shilingi milioni 20 ,"amebainisha Mh.Mariam
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Zainabu Vullu amesema kwamba mikakati ambayo wamejiwekea ni kuondokana na kuwa tegemezi na kwamba lengo kubwa ni kuwa na miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo itakuwa na tija zaidi katika kuwasaidia wanawake.
Naye Katibu wa UWT Mkoa wa Pwani Aziza Omary amesema kwamba kwa sasa wamejipanga na kuweka mipango madhubuti ya kuwa na miradi mbali mbali ikiwemo kuwepo na miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa ujenzi wa nyumba za makatibu kwa ngazi ya Wilaya na ngazi ya Mkoa.
Akitoa salama za serikali Mkuu wa Mkoa wa Pwani Stanslaus Nyongo amewahimiza wanawake kuchangamkia fursa za asilimia 10 ambazo zinatengwa na Halmashauri kwa lengo la kuweza kuwasaidia sana wanawake katika kujikwamua kiuchumi.
Katika kikao cha baraza la UWT Mkoa wa Pwani wameweza kujadili mambo mbali mbali yakiwemo suala la uanzishwaji wa miradi ya maendeleo ili kujikwamua kiuchumi, ujenzi wa nyumba za makatibu wa Wilaya pamoja na Mkoa, mikakati ya kuimarisha jumuiya na uhai wa wanachama, pamoja na jinsi watakavyoweza kutimia fursa za mradi wa pikipiki ambazo wamepatiwa kama ni moja ya kitega uchumi.


Comments
Post a Comment