TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 41 ZA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI
Tanzania kupata dola milioni 41 za uhifadhi wa bioanuwai, kuhimili mabadiliko ya tabianchi Tanzania inatarajiwa kunufaika na takribani Dola za Marekani milioni 41 kupitia madirisha mbalimbali ya ufadhili wa Global Environment Facility (GEF), kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi wa bioanuwai, urejeshwaji wa mifumo ikolojia na kujenga ustahimilivu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi. Hayo yamebainika katika mazungumzo kati ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi na Mratibu wa Bioanuwai wa GEF kwa Afrika, Bw. Jurgis Sapijanskas, yaliyofanyika Nairobi, Kenya, pembezoni mwa mikutano ya SBSTTA-28 na SBI-7 mwishoni mwa wiki. Katika mazungumzo hayo, imeelezwa kuwa takribani Dola za Marekani milioni 16 zimetengwa kupitia dirisha ya GEF – Trust Fund katika Mzunguko wa 9 (GEF-9), huku fursa nyingine zikijumuisha Dola milioni 20 kupitia Mfuko wa Least Developed Countries Fund (LDCF) kwa ajili ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, pamoja na Dola milioni...