Posts

ASKOFU PENGO AFARIKI DUNIA.

Image
 

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 20 FEBRUALI 2026.

Image
 

SERIKALI YASHUSHA ADA KWA WANABLOGU.

Image
SERIKALI YASHUSHA ADA KWA WANABLOGU. TCRA Yazindua Redio ya Kisasa 'DSB' SERIKALI imetangaza neema ya kihistoria kwa wanablogu, vijana wabunifu, na watoa maudhui mtandaoni nchini kwa kupunguza ada za leseni kwa kiwango kikubwa, hatua inayolenga kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali na kurasimisha shughuli za wahabarishaji wa mitandao. Hatua hiyo imekuja kufuatia utafiti wa kina na mikutano ya kimkakati ya takribani mwaka mzima kati ya mtandao wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ikielezea vikwazo vya gharama vilivyokuwa vikikwaza uandishi wa habari za kidijitali nchini. Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Watoa Huduma za Utangazaji (ABC 2026) jijini Dodoma leo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamisi Mwinjuma, amesema ada ya leseni kwa watoa maudhui mtandaoni imeshushwa kutoka Sh500,000 hadi Sh50,000 tu, huku ada ya maombi ikiwa ni Sh10,000 pekee. Mageuzi hayo pia yamegusa kundi la wakusanyaji w...

ITHIBATI YA WAANDISHI WA HABARI NI NGAO YA TAIFA KATIKA VITA.

Image
  Ithibati ya waandishi wa habari imeendelea kujidhihirisha kama nguzo muhimu ya ulinzi wa Taifa katika dunia ya sasa inayotawaliwa na vita ya taarifa.   Kupitia Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), inayotoa ithibati na vitambulisho vya uandishi wa habari kwa waandishi wenye vigezo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari, Taifa linapata waandishi wanaotambulika, wanaowajibika na wanaofanya kazi kwa kufuata misingi ya taaluma, weledi na maadili.  Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Greyson Msigwa, wakati akizungumza katika kikao kazi na waandishi wa habari kilichoratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) tarehe 18 Desemba 2025 jijini Dar es Salaam.  Amesema kuwa hatua hiyo inasaidia kudhibiti upotoshaji wa taarifa na kulinda taswira ya nchi ndani na nje ya mipaka yake kwani dunia ya sasa haipigani tena vita kwa silaha za kijeshi pekee, bali kwa taarifa zinazozalishwa ...

SERIKALI YAAHIDI ULINZI NA USHIRIKIANO KWA WAANDISHI WA MTANDAONI.

Image
  Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuonesha dhamira ya dhati ya kulea na kuwawezesha waandishi wa habari wa mitandaoni na mabloga, badala ya kuwashughulikia kwa mtazamo wa adhabu, ili kujenga tasnia imara na yenye tija ya habari nchini. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, aliipongeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa mwelekeo wake wa kulea wadau wa sekta ya habari badala ya kuchukua hatua kali za kinidhamu. Msigwa alisema mwelekeo huo unaendana na falsafa ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambayo inalenga kushirikiana na wadau mbalimbali kwa manufaa ya taifa. Aliitaja Tanzania Bloggers Network (TBN) na Jukwaa la Mitandao Tanzania (JUMIKITA) kuwa ni wadau wakubwa wa serikali katika tasnia ya habari, akisisitiza kuwa mchango wao ni muhimu katika kusambaza taarifa na kujenga mawasiliano kati ya serikali...

HALMASHAURI YA MJI BAGAMOYO YAKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA KWA WALIMU WAKUU.

Image
  Halmashauri ya mji wa Bagamoyo, imekabidhi vifaa vya TEHAMA kwa walimu wakuu wa shule za kata za Zinga, Dunda na Kata ya Yombo. Makabidhiano hayo yameongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bagamoyo Mhe Mohamedi Usinga  Desemba 17,2025. Katika makabidhiano hayo Mhe Mwenyekiti amekabidhi jumla ya komputa (Desktop)44 katika Shule ya Msingi Yombo wamepata Komputa 20,shule ya Msingi Kizuiani 12 na Shule ya Zinga 12 pamoja na Komputa Mpakato moja kwa kila shule na vifaa vyake kwa ujumla. Mhe Usinga ametoa wito kwa walimu hao kuhakikisha wanavitunza na kuvilinda vifaaa hivyo kwa ajili ya kujifunzia kwa wanafunzi mashuleni ili kuendana na kasi ya teknologia. Vilevile Mhe Mwenyekiti ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha anawezesha upatikanaji wa vifaa vya Tehama mashuleni lakini pia na kuwezesha miundombinu bora mashuleni. Nae Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Mji wa Bagamoyo Ndg Shauri Selenda amewasisitiza walim...