Popular posts from this blog
MAGAZETI YA TANZANIA LEO JUMATATU TAREHE 31 AGOSTI 2026
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
MWENGE WA UHURU, WAZINDUA NA KUTEMBELEA MIRADI YA MILIONI 900. BUKOBA
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
MWENGE WA UHURU, WAZINDUA NA KUTEMBELEA MIRADI YA MILIONI 900. BUKOBA Alodia Dominick, Bukoba Mwenge wa uhuru umezindua, kuweka mawe ya msingi na kutembelea miradi saba yenye thamani ya sh. milioni 900 katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera. Mwenge wa Uhuru umewasili Manispaa ya Bukoba Augosti 31, 2026 ukitokea katika wilaya ya Muleba. Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Wazo Mwang'onda akiwa Manispaa ya Bukoba amesisitiza wananchi kuilinda amani, umoja na mshikamano kwani pasipo amani hakuna miradi ya maendeleo inayoweza kutekelezwa. "Ni wajibu wetu wananchi wa Taifa hili kuilinda amani ya nchi yetu chini ya kauli mbiu isemayo Tanzania ni yetu sote tushikamane kuleta maendeleo sambamba na hiyo inatukumbushwa mapambano dhidi ya rushwa, madawa ya kulevya, mapambano dhidi ya virusi vya ukimwi na mapambano dhidi ya maralia" amesema Mwang'onda Ameeleza kuwa, ujumbe huo unawataka wananchi kuendelea kulinda amani na utulivu uliohasisiwa na viongozi wa nchi hi...
MAKAMU WA RAIS, ATEMBELEA OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
MAKAMU WA RAIS, ATEMBELEA OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA AWATAKA WATUMISHI KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amewataka watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira kuongeza bidii, uwajibikaji na kuachana na utendaji wa kazi kwa mazoea ili kuhakikisha majukumu ya Serikali yanatekelezwa kwa ufanisi na kwa wakati. Makamu wa Rais ametoa wito huo leo, alipofanya ziara yake ya kwanza katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), iliyopo Mtumba, jijini Dodoma, ambako alipokelewa na wafanyakazi pamoja na Menejimenti ya Wizara hiyo. Amesisitiza umuhimu wa watumishi kubadili mitazamo na namna ya kufanya kazi, akitaka kila mmoja kuwa mbunifu na kuweka mipango inayolenga kuleta matokeo yanayoonekana kwa wananchi na Taifa kwa ujumla. Makamu wa Rais amewasihi watumishi kutumia nafasi zao kutoa huduma yenye thamani kwa watanzania na kutambua dhaman...
TARURA YATENGA BIL. 1 KUKABILIANA NA EL NINO TABORA
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
TARURA YATENGA BIL. 1 KUKABILIANA NA EL NINO TABORA Na Allan Kitwe, Tabora WAKALA wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoani Tabora wametenga zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali ili kukabiliana na wingi wa mvua za el nino. Hayo yamebainishwa jana na Afisa wa Wakala huo, Mhandisi Nehemia Chacha kwa niaba ya Meneja wa TARURA Mkoa wa Tabora alipokuwa akitoa taarifa ya hali ya barabara kwenye kikao cha madiwani wa halmashauri ya manispaa. Ameeleza kuwa ili kuhakikisha miundombinu ya barabara katika manispaa hiyo inapitika wakati wote wamekamilisha ujenzi wa madaraja makubwa 2 ya kimkakati katika kata za Ndevelwa, Misha na Kabila. Mhandisi amefafanua kuwa daraja la Ndevelwa ambalo lilikuwa kero kubwa sana kwa wananchi limegharimu zaidi ya shilingi milioni 460 na limekamilika kwa asilimia 100 na sasawananchi wameanza kulitumia, kero imeisha Daraja la pili ni lile linalounganisha Kata za Misha na Kabila ambalo lil...
SHULE YA MSINGI IPULI YAPEWA TUZO YA UFANISI
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
SHULE YA MSINGI IPULI YAPEWA TUZO YA UFANISI Na Allan Kitwe, Tabora HALMASHAURI ya Manispaa Tabora imetoa tuzo maalumu ya pongezi kwa Uongozi wa Shule ya Msingi Ipuli iliyopo katika Kata ya Ipuli Mjini Tabora kwa usimamizi mzuri wa fedha za maendeleo zilizopelekwa shuleni hapo. Akikabidhi tuzo hiyo (Cheti cha Pongezi) leo, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Ghullam-Hussein Dewj amempongeza Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Chiku Mwaka na Kamati yake kwa kusimamia vizuri maboresho ya miundombinu. Amesema kuwa Uongozi wa shule hiyo umeonesha weledi mkubwa kwa kusimamia kwa dhati mradi wa uboresha elimu (GPE) uliotekelezwa na serikali shuleni hapo kwa mwaka wa fedha uliopita kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 60. ‘Chini ya usimamizi wa Mwalimu Mkuu na Kamati ya Shule, Mradi umetekelezwa kwa ufanisi wa hali ya juu hali iliyopelekea mazingira ya shule hiyo kubadilika kwa kiasi kikubwa na kufanya watoto na wazazi kupenda shule yao’, ameeleza. ‘Tunakupongeza sana Mwalimu M...
MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KUANZA JANUARI 2027
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
Na Alodia Dominick, Bukoba, Mradi wa bomba la mafuta ambao utekelezaji wake wa jumla umefikia asilimia 87.7 unatarajia kukamilika na kuanza rasmi Januari 15,2027. Mradi huo ambao mkataba wake ulisainiwa mwaka 2021 unatarajiwa kuanza rasmi ifikapo Januari 15, 2027 na kutokana na mkataba mradi utadumu takribani miaka 25. Mratibu wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kusafirisha mafuta ghafi Afrika Mashariki (EACOP) Jumanne Saidi akitoa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari mkoani Kagera juu ya mradi wa bomba la mafuta na maendeleo yake ameeleza kuwa, mradi huo utaanza rasmi Januari 15,2027. Amesema sh.bilioni 35.6 zimetumika kulipa fidia kwa wananchi wapatao 10,144 maeneo yote yanayopitiwa na bomba la mafuta na nyumba zilizoguswa ni 340, kwa Kagera ni nyumba 119 ambapo waguswa kwa Kagera wako 118. "Mikoa inayopitiwa na bomba la mafuta ni nane ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Manyara, Dodoma na Tanga na katika mkoa wa Kagera unapita katika wilay...
WMA: KILO NA LITA YA TANZANIA NI KILO NA LITA YA DUNIA
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
WMA: KILO NA LITA YA TANZANIA NI KILO NA LITA YA DUNIA Na WMA - MWANZA Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Geita, Bi. Eva Ikula amesema usimamizi wa matumizi sahihi ya vipimo unaofanywa na WMA umewezesha bidhaa za Tanzania kuaminiwa na kukubalika zaidi katika soko la kimataifa. Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 31, 2026 katika banda la WMA wakati wa Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayoendelea katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, Bi. Ikula amesema mojawapo ya sababu kubwa ya bidhaa za Tanzania kukubalika katika soko la kimataifa ni uhakika wa vipimo. "Kilo yetu ni kilo ya Kenya, ya India, na ya Ujerumani pia. Hiyo ndiyo nguvu ya matumizi ya vipimo sahihi." Amesema WMA inaendelea kutoa elimu kupitia kampeni mbalimbali ili kujenga uelewa kuwa "Kipimo sahihi ni pasipoti ya bidhaa yako kuingia soko lolote duniani." Amebainisha kuwa wanunuzi wa kimataifa wanaiamini Tanzania kwa sababu WMA inatumia mfumo mmoja wa kimataifa wa vipimo ...
MAGAZETI YA TANZANIA LEO JUMAPILI TAREHE 16 AGOSTI 2026
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
BAKWATA YATANGAZA SIKUKUU YA MAULIDI NI TAREHE 25 AGOSTI 2026
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
Baraza Kuu la waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limetangaza sikukuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammadi Swala Allahu Alayhi Wasalam, kuwa ni siku ya jumanne ya tarehe 25 Agosti 2026. Katika Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Katibu Mkuu BAKWATA, Alhaji, Nuhu Jabiri Mruma, imesema Maulidi itasomwa usiku wa siku ya jumatatu ya tarehe 24 Agosti 2026 katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.



























Comments
Post a Comment