Thursday, February 13, 2020

MASAUNI ATEMBELEA SHULE YA POLISI MOSHI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Polisi baada ya kuwasili  katika Shule ya Polisi Tanzania wakati wa ziara yake aliyoifanya hapo chuoni lengo kusisitiza ufundishaji makini ili jamii iweze kufaidika na huduma zinazotolewa na Jeshi la Polisi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akiangalia moja ya darasa linalotumika kufundishia wanafunzi katika Shule ya Polisi Tanzania wakati wa ziara yake aliyoifanya hapo chuoni lengo kusisitiza ufundishaji makini ili jamii iweze kufaidika na huduma zinazotolewa na Jeshi la Polisi,wapili kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Salum Hamduni.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akikagua dawati katika  moja ya darasa linalotumika kufundishia wanafunzi katika Shule ya Polisi Tanzania wakati wa ziara yake aliyoifanya hapo chuoni lengo kusisitiza ufundishaji makini ili jamii iweze kufaidika na huduma zinazotolewa na Jeshi la Polisi,wapili kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Salum Hamduni.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Salum Hamduni(kulia) baada ya kukagua moja ya chumba vinavyotumika kutoa huduma ya malazi kwa   wanafunzi katika Shule ya Polisi Tanzania wakati wa ziara yake aliyoifanya hapo chuoni lengo kusisitiza ufundishaji makini ili jamii iweze kufaidika na huduma zinazotolewa na Jeshi la Polisi.
................................................


Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni ameutaka uongozi wa Shule ya Polisi Tanzania kuwafundisha ueledi wapelelezi ili kuweza kupunguza msongamano wa mahabusu na kesi ambazo zinasababishwa na upelelezi usio na kiwango.


Masauni ameyasema hayo mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara ya kutembelea Shule ya Polisi Tanzania lengo ikiwa kusisitiza ufundishaji makini ili jamii iweze kufaidika na huduma za Jeshi la Polisi.


“Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli alipokua akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria aligusia suala la wapelelezi kuwa chanzo cha mlundikano wa mahabusu katika magereza yetu na mimi hii leo nimetoka gereza la Arusha nimeongea na wafungwa na mahabusu nao wanalalamikia upelelezi wa kesi zao kupindishwa na mbaya zaidi wengine wamehukumiwa vifungo kwa ajili ya upelelezi usio makini.


Ni tatizo kubwa haiwezekani Rais huyu alalamike kila siku sasa maagizo ya serikali kwa chuo hiki jitahidini kupika vizuri wapelelezi wenu vizuri,tumpumzishe Rais wetu ana mambo mengi,timizeni tu wajibu wenu”amesema Masauni.


Akizungumza katika ziara hiyo Kaimu Kamandanti Kamishna Msaidizi Omar Khamis Omar amesema wamechukua maelekezo ya serikali na wanaahidi kuyafanyia kazi ili yaweze kuleta tija huku akitaja idadi ya wanafunzi waliopo shuleni hapo wakisomea fani mbalimbali.


“Shule yetu kwa sasa ina wanafunzi 856 kati yao wanaume 725 na wanawake ni 131 ambao wako katika mafunzo mbalimbali na wote wanaendelea vizuri na masomo” amesema Kamishna Msaidizi Omar
Katika ziara hiyo ya Naibu Waziri Masauni alipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya shule hiyo ikiwemo sehemu za kulala,madarasa,uwanja wa paredi,vyumba vya komputa na ukarabati bwalo la chakula.

TIF YAKABIDHI MISAADA KILWA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO.

Image may contain: 2 people, beard and text
Mwenyekiti wa taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) Aref Nahdi akikabidhi msaada kwa waathirika wa mafuriko eneo la Njinjo wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
Image may contain: 4 people, people standing and outdoor 
Mwenyekiti wa taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) Aref Nahdi, akiwa na Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Musa Buluki, pamoja na viongozi waandamizi wa taasisi ya hiyo wakiwasili eneo la Njinjo wilayani Kilwa kwaajili kugawa misaada kwa wananchi walioathirika na mafuriko kutoka na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini.

Akizungumza katika zoezi hilo, Aref alisema anawashukuru wananchi wote kwa ujumla walioungana na The Islamic Foundatio kufanikisha misaada hiyo ili kuwasaidia watanzania waliokumbwa na mafuriko.

Alisema taasisi hiyo iliweka makadirio ya kukusanya kiasi cha shilingi milioni 100 lakini kwa muitikio ulivyokuwa mkubwa makusanyo ya michango imefika zaidi ya milioni 110.

Aidha, alisema wanatekeleza hayo kwa mujibu wa mafundisho ya uislamu yanayotaka kusaidiana katika matatizo bila ya kujali dini, rangi, wala kabila.
Image may contain: one or more people
 Image may contain: 2 people, people standing and outdoor
Vijana wakujitolea wakiwa katika harakati za kugawa misaada iliyokusanywa na The Islamic Foundation kwa waathirika wa mafuriko huko Njinjo wilayani Kilwa.

Image may contain: 5 people, people sitting and text 
Sehemu ya wananchi walioathirika na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini, wakisubiri utaratibu wa kugaiwa misaada hiyo kutoka kwa taasisi ya The Islamic Foundation ambayo makao yake makuu ni mkoani Morogoro.
Image may contain: one or more people 
Image may contain: one or more people and outdoor
Sehemu ya misaada hiyo ikiwa imepangwa kwa utaratibu wa kugawa kwa wahusika.

Tuesday, February 11, 2020

WAHANGA WA MAFURIKO LINDI WAPOKEA MISAADA KUTOKA KWA MAHAKAMA NA SEDO.

 
Mkuu wa Mkoa huo Godfrey Zambi (kushoto akipokea msaada huo kutoka kwa Jaji Mfawidhi Mahakama kuu kanda ya Mtwara, Jaji Paul Gwembe.
..................................................

NA HADIJA HASSAN. LINDI

Mahakama kuu kanda ya Mtwara, Jamii ya watu wa kusini (SEDO) waungana na wadau wengine wa maendeleo kuwasaidia waathirika wa Mafuriko Mkoani Lindi kwa kutoa pesa taslimu na vitu mbali mbali vyenye thamani ya Shilingi milioni 8,637,000.

Misaada hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Godfrey Zambi ofisini kwake.

Misaada hiyo ni pesa taslimu shilingi milioni 3.1 kutoka Mahakama kuu kanda ya Mtwara, Nguo mifuko tisa,mabati 250 yenye thamani ya shilingi milioni 4, pamoja na unga viroba 15 vyenye ujazo wa kg 25 na sukari mifuko 8 ya kg 25 vyenye thamani ya shilingi lako 537,000 kutoka kwa jamii ya watu wa kusini (SEDO).

Akikabidhi msaada huo Jaji Mfawidhi Mahakama kuu kanda ya Mtwara, Jaji Paul Gwembe alisema kuwa fedha hizo walizokabidhi ni michango kutoka kwa watumishi wa Mahakama zote za Mikoa hiyo ya Lindi na Mtwara.

Nae mwenyekiti wa wanakusini forum (SEDO) Brigedia jeneral msaafu Aloyce Mwanjile pamoja na kutoa pole aliupongeza uongozi wa Mkoa huo kwa namna walivyoshughulika na maafa hayo pamoja na kuwaokoa wananchi.

Akipokea misaada hiyo Mkuu wa Mkoa huo Godfrey Zambi aliwashukuru wadau hao kwa misaada waliyoitoa kwa ajili ya waathirika huku akiwatoa hofu kuwa misaada hiyo ipo katika mikono salama na itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

WAANDIKISHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA WAAPISHWA RASMI CHALINZE


Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Chalinze Bi Amina Kiwanuka, amewaapisha rasmi, waandikishaji wasaidizi 319 na na watumiaji wa mashine za kuandikishia wapiga kura yaani "BVR" 319. Waandikishaji hao waliapishwa katika Ukumbi wa shule ya sekondari ya Lugoba baada ya kupata mafunzo ya namna ya uandikishaji wa wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura.


Kiwanuka katika hotuba yake ya uzinduzi wa mafunzo ya uandikishaji aliwataka wote walioteuliwa kufanya zoezi hili muhimu la kitaifa kwa umakini,uadilifu na weledi wa hali ya Juu,kwani wameaniwa hivyo wazingatie sheria, taratibu na kanuni zinazotumika katika zoezi hili.


Aidha Afisa Mwandikishaji wa Jimbo amewataka kuzingatia muda wa kufungua vituo na kufunga."Mnatakiwa kuutumia vizuri muda wa uandikishaji kwani zoezi hili litafanyika kwa muda wa siku Saba tu kuanzia tarehe 14/02/2020 hadi tarehe 20/02/2020." Kiwanuka alisisitiza.


Bi Kiwanuka katika hotuba yake alitoa wito kwa wananchi wote katika halmashauri ya Chalinze na Jimbo la Chalinze kujitokeza kwa wingi ili kuja kujiandikisha lakini pia kurekebisha taarifa zao endapo Pana uhitaji wa kufanya hivyo,amewaagiza watendaji wa kata,watendaji wa vijiji,wenyeviti wa vijiji,wenyeviti wa vitongoji na vyombo vya Habari kuwahamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kujiandikisha.


Hata hivyo aliwataka wananchi kutoa taarifa sahihi kuhusu ndugu na jamaa waliofariki au kufungwa ili waweze kuondolewa katika daftari la wapiga kura na hatimaye kuwa na watu sahihi katika daftari hilo.


IMETAYARISHWA NA KITENGO CHA HABARI,MAWASILIANO NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHALINZE


Sunday, February 9, 2020

Wiki ya uhasibu kufanyika feb 9, 2020, wajasilimali, wavuvi, wafugaji kupewa ushauri: TAA




Na mwandishi wetu


Chama cha wahasibu Tanzania (TAA) kwa kushirikiana na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) pamoja na chama cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA) wameandaa wiki ya uhasibu, hamira ikiwa kuwaleta karibu wahasibu na jamii.


Kwa miaka mingi wahasibu walikuwa wanakaa nyuma ya kompya zao wakifanya kazi zao, hawakuweza kuwa karibu najamii,wengine walionekana kuwa kikwazo cha kupata fedha zao, lakini wameamua kujitokeza hadharani na kuwaambia watu kuwa wao sio kama wanavyowafikilia.


Akizungumza na waandishi wa habari jana, mwenyekiti wa chama chawaasibu Tanzania (TAA) alisema wafanyabiashara, wajasiliamali, wafugaji, wavui na taasii mbalimbali watapata fursa ya kupata ushauri.


Kwa mara ya kwanza wiki ya Uhasibu itaadhimishwa kwa siku 6 kuanzia March 9 hadi March 14, Wiki ya Uhasibu inafanyika kwa ajili ya kuifahamisha jamii umuhimu wa taalum ya uhasibu kwa ajili ya uchumi wa viwanda na maendeleo ya jamii.


Hii itakuwa inawaleta pamoja wadau mbalimbali kushiriki na kutambua kazi ya Uhasibu na Wahasibu wanaofanya kazi katika taasisi mbalimbali kwenye ngazi mbalimbali za majukumu ya taaluma hiyo, ambapo kutakuwa na huduma ya kushauri  na kuwawezesha wahasibu kusonga mbele kitaaluma.


Kwa Wahasibu ambao wana malengo ya kufungua kampuni zao binafsi au taasisi zozote za Uhasibu hiyo itakuwa ni fursa nzuri kwao kukutana na wenye makampuni wabobemzi na itakuwa ni fursa nzuri kushea nao mawazo.