Saturday, July 13, 2019

TIC WAKUSANYA MAMIA YA WAWEKEZAJI KUJADILI SEKTA YA KOROSHO

Na Bakari Chijumba

Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba amesema Tanzania inakusudia kuwa mzalishaji mkubwa wa zao la korosho Duniani ambapo imeweka mkakati wa kufikia uzalishaji wa tani milioni moja ifikapo mwaka 2023/2024 kutoka tani laki tatu na kumi na tatu kwa sasa.

Akizungumza  Ijumaa July 12, 2018 katika kongamano la kimataifa la uwekezaji kwenye sekta ya korosho lililoandaliwa na kituo cha uwekezaji nchini Tanzania (TIC) na kufanyika katika ukumbi wa Benki Kuu tawi la Mtwara, amesema vipo viwanda zaidi ya kumi ambavyo vimekuwepo tangu serikali ya awamu ya kwanza ambavyo teknolojia yake imepitwa na wakati na vingine havifanyi kazi kabisa.

“Mwalimu Nyerere mwaka 1978 hadi mwaka 1980 alijenga viwanda zaidi ya 12 ambavyo kwa sasa teknolojia yake imepitwa na wakati. Baadhi vimekufa na vilivyobaki vimepunguza uzalishaji,tumaeamua kuwaita wawekezaji ili kuviendeleza na kuanzisha vingine ili kuongeza uzalishaji” amesema Mgumba.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji nchini Tanzania (TIC) Geofrey Mwambe amesema Serikali imekuwa na matarajio makubwa ya kuwapo kwa ongezeko la uwekezaji katika zao la korosho ambapo wataanzisha viwanda kutokana na mwamko uliooneshwa na wawekezaji hao kwa kuwa wametambua fursa kwenye zao hilo.

Mwambe amesema wameamua kuandaa kongamoano hilo ili kushawishi wawekezaji wazawa na wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani ili wawekeze katika viwanda vya kubangua korosho katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

“Tulitarajia kupata wageni 100 mpaka 150 lakini tumepata wawekezaji zaidi ya 300, Kwa idadi hii tumevuka lengo la kongamano letu na tunaimani watakuwa tayari kuwekeza kwenye viwanda vikiwemo viwanda vya korosho, nashukuru Wakuu wa Mikoa walioshiriki wote wametenga maeneo ya uwekezaji jambo ambalo linarahisisha kazi hii na kuifanya kuwa nyepesi" amesema Mwambe.

Mmoja ya wawekezaji kwenye kongamano hilo Mahamoud Sinani ameishukuru Serikali kwa kuwakutanisha pamoja na kuwawezesha kuzitambua fursa mbalimbali zilizopo katika kilimo cha zao korosho hapa nchini.

Sagini aitaka VETA kupeka mashine Simiyu

 
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini akizungumza na waandishi habari kuhusiana vitu alivyoona katika banda la VETA katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini amesema bidhaa zinazozalishwa na VETA wapeleke kwa wakulima ili kuweza kutatua changamoto zao ikiwa pamoja na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

Sagini aliyasema hayo wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.amesema wakulima wanahitaji mashine mbalimbali ambazo VETA mnazalisha hivyo zisiishie katika Maonesho.

Amewataka VETA kwenda na mashine hizo na kuziuza kwa wakulima wa Simiyu katika Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika mkoani humo.
Sagini amesema kuwa VETA wanafanya ugunduzi katika nyanja mbalimbali ambazo zikitumiwa vizuri kutarahisha wakulima kukua kiuchumi kutokana na vitendea kazi kutoka VETA.
Aidha amesema kuwa mashine za VETA zisimbazwe kwani gharama itakuwa rahisi kwa wakulima kumudu kuliko mashine za nje.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini akipata maelezo kutoka VETA kwa mwanafunzi wenye mahitaji Maalum vitu wanavyotengeneza wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini akipata maelezo kuhusiana na mashine ya kuchakata majani kwa ajili ya Mifugo wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mashine iliyundwa na Watu Wenye mahitaji Maalum kwa kushirikiana na Mwalimu wao wa VETA Chang'ombe.

Mwenyekiti wa zamani wa UWT kizimbani kwa kughusi cheti cha ndoa

ERICK MUGISHA (DSJ) – DAR ES SALAAM
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Ilala Norah Waziri (52), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa shtaka la  kughushi cheti cha ndoa.
Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Benson Mwaitenda, akimsomea shtaka lake mbele ya Hakimu, Anifa Mwingira, alidai Februari 4 mwaka 1995 jijini  Dar es Salaam, kwa nia ya kudanganya mtuhumiwa alighushi cheti cha ndoa chenye namba za usajili 00040078  kikionyesha ameolewa na Silvanus Mzeru katika Kanisa Katoliki la Mburahati.
Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo ambapo mwendesha mashitaka alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
Hakimu Mwingira alisema dhamana ipo wazi kwa mashariti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu wenye barua zinazo watambulisha wanapotokea, vitambulisho vya Taifa na kusaini bondi ya Sh milioni moja.
Mshitakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza mashariti na kesi hiyo itatajwa tena Julai 17.
Wakati huo huo watu wawili amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa shtaka la mauaji.
Waliofikishwa Mahakamani ni Juma Malumbi (34) mkazi wa Kinondoni Hananasif na Amri Mazangu (40) mkazi wa Mbagala Kirulugwa.
akiwasomea mashtaka yao mbele ya Hakimu Joyce Mushi, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, ASP Hamisi, alidai Octoba 20 mwaka 2018 maeneo ya Bonde la Mchicha Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam, watuhumiwa walimuua Zurufa Oda.
Hakimu Mushi alisema washitakiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.
ASP Hamisi alidai upelelezi hauja kamilika na kuomba tarehe nyingine kwa kesi hiyo kutajwa

RAIS WA UGANDA MUSEVENI AWASILI CHATO MKOANI GEITA NA KUPOKEWA NA RAIS DKT. MAGUFULI


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati wakipita kwenye Gadi ya Heshma iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati wakiangalia vikundi mbalimbali vya Ngoma na Kwaya mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.
 Rais wa Uganda Yoweri Museveni akizungumza na Wananchi wa Chato mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati akiwapungia mkono wananchi waliofika katika uwanja wa ndege wa Chato.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati waliupokuwa wakiwasalimia wananchi wa Njiapanda Chato mkoani Geita. 
Baadhi ya Wananchi wa Chato waliojitokeza katika mapokezi ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni Chato mkoani Geita. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU

MAGAZETI YA LEO JULAI 13, 2019.

CHALIWASA YAWAPIGA MSASA WATUMISHI WAKE

Na Omary Mngindo, Chalinze.

WATUMISHI wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Chalinze (CHALIWASA) wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wametakiwa kuwatuliza wateja na kuwapa lugha nzuri, hasa pale wanapokuja kwenye ofisi wakiwa na jazba.


Kauli ya Mhandisi Raymond imefuatia malalamiko kutoka kwa Abdallah Kipolelo, aliyelalamikia kuwepo kwa baadhi ya viongozi wa CHALIWASA kutokuwa na lugha nzuri, mara baada ya kupokea taarifa za utendaji wa kazi kutoka kwa wateja.


Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Mhandisi Honest Raymond, alipozungumza na watumishi katika kikao cha kukumbushana majukimu ya kazi, huku suala la nidhamu likisisitizwa katika kikao hicho.


"Sisi tunafundishwa namna ya kuwahudumia wateja, wao hawana somo kama hilo hivyo unapokutana na mteja anakuwa mkali, wewe jukumu lako ni kumtuliza, kwani wakati mwingine anaweza kufikia hatua ya kukupiga ngumi," alisema Mhandisi Raymond.


Kwa upande wake Kipolelo alisema kuwa kuna wakati mtumishi anapokea simu ya upole kutoka kwa mteja akimjulisha kuwepo kwa uvujaji maji eneo alilopo, lakini utakuta kiongozi anapiga simu kwa ukali, hatua aliyodai kama ya udhalilishaji.


"Mteja anakupigia simu kwa upole akikuelezea kuwepo kwa tatizo eneo moja, wakati huohuo unapigiwa simu kwa lugha ya ukali kutoka kwa kiongozi, wee Kipolelo uko wapi, nenda eneo fulani kuna tatizo, lugha ambayo ni ya udhalilishaji," alisema Kipolelo.


Akitoa mada katika kikao hicho, Elizabeth Eusebius ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii aliwaambia watumishi hao kuwa wameamua kutoa mafunzo hayo kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa taasisi.


"Tumekuwa tukijikita katika utoaji wa elimu kwa watumiaji wa maji, kwetu tumejisahau warsha tunayopeana leo inalenga kufahamishana masuala mbalimbali ili wote tukafanyekazi za Mamlaka," alisema Elizabeth.