Thursday, July 11, 2019

KILWA YATENGA MILIONI 12 KUPIMA MIPAKA YA ARDHI.

Na Hadija Hassan, Lindi.

Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi imetenga julma ya Tsh. 12,000,000. Kwa ajili ya kumaliza migogoro yote ya mipaka ya Aridhi iliyonayo hivi sasa katika vijiji vinne ifikapo 2020.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Renatus Mchau hivi karibuni alipokuwa akizungumza na Bagamoyo kwanza blog ofisini kwake.

Alisema fedha hizo walizotenga ni kwa ajili ya kuwawezesha wataalamu wa Aridhi wa Halmashauri hiyo kupima upya mipaka ya Aridhi katika vijiji hivyo.


Mchau alivitaja Vijiji vinavyokabiliwa na Migogoro hiyo ya mipaka ya Aridhi kuwa ni Namayuni, Mingumbi , Liwiti na likawage Alisema kuanzia mwezi January mpaka kufikia mwezi machi kiasi cha Tsh.1,500,000. zimeshatumika katika kazi hiyo ya upimaji upya wa mipaka ya Aridhi.

Pamoja na mambo mengine aliiambia Bagamoyo kwanza blog kuwa licha ya kudhamiria kutatua migogoro ya mipaka ya Aridhi pia Halmashauri hiyo inatarajia kufanya upimaji wa stendi kuu ya Mabasi katika eneo la Nangurukulu na Mihani.

Aliongeza kuwa upimaji huo wa Stendi kumbwa ya mabasi utawezesha upatikanaji wa ramani na hati za Stendi mwaka 2020 ambao umeghalimu Tsh. 4,500,00

HALMASHAURI YA KILWA YATUMIA ZAIDI YA MILIONI 4 KUREJESHA MAZALIA YA SAMAKI BAHARINI.

Na Hadija Hassan, Lindi.


Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi imetumia kiasi cha Tsh.4,350,000 kwa kwa ajili ya kurejesha mazalia na makalia ya Samaki yaliyoharibika kutokana na shughuli mbali mbali za kibinaadamu.


Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo jana alipokuwa akizungumza na Bagamoyo kwanza blog ofisini kwake.


Alisema kuwa fedha hizo zimetumika kwa kipindi cha miezi mitatu January hadi march mwaka 2019 Huku akieleza kuwa katika kiasi hicho cha fedha sh.350,000 zilitumika kwa ajili ya uimarishaji na uanzishwaji wa vikundi vya ushirika wa Uvuvi na wafugaji wa samaki 650,000. kurejesha mazalia na makalia ya samaki yaliyohalibika kutokana na mabadiliko ya Tabia Nchi na uharibifu wa mazingira kwa kuweka Matumbawe bandia pamoja na kupanda Mikoko katika Bahari.


Mchau alisema Mpaka sasa tayari Miamba Mitano ya Chocha ndogo, chocha kubwa, pera, nyuni na mpovi imefungwa kwa ajili ya kurejesha mazalia ya samaki kwenye kata za Somanga, Kivinje, Songo songo na Singino.


Aidha, Mchau aliongeza kuwa, Tsh. 950,0000,00 zilitumika kwa ajili ya kuendeleza Mapambano dhidi ya Uvuvi haramu pamoja na kuufanya Uvuvi halali kuwa endelevu na wenye tija ambapo doria tatu(3) za kupambana na uvuvi haramu zilifanyika.


Alisema katika Dolia hizo tatu zilizofanyika mbili zilifanikiwa kukamata nyavu haramu za tamba 4, saratonga2, kokoro 18 nyavu chini ya 8mm.

Wednesday, July 10, 2019

Tacaids kushirikiana na Wasafi kutoa elimu ya VVU





Anna Potinus – Dar es Saaam
Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), wametangaza kushirikiana na kampuni ya Wasafi Ltd katika kupeleka ujumbe kwa jamii kuhusiana na suala la afya kupitia tamasha la Wasafi festival ambapo wasanii watapata fursa ya kutoa elimu kwa vijana juu ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Julai 10, katika ofisi za Tacaids zilizopo Posta jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa kampuni ya Wasafi na mwanamuziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul maarufu ‘Diamond Platnumz’, amesema lengo kuu la ushirikiano huo ni kuangalia ni namna gani wasanii wanaweza kutumia vipaji vyao kuelimisha jamii.
“Tuliona tuandae tamasha la Wasafi festival ambalo litatukutanisha na kutumia sanaa yetu katika njia zilizo sahihi hivyo tukaona sasa imefikia muda kutumia ushawishi tulionao na katika kulifanikisha hilo tukasema tukishirikiana na Tacaids pengine tutafikisha ujumbe mzuri zaidi,” amesema.
“Hauwezi kutimiza ndoto zako kama hauna afya bora hivyo tukiwa kama wasanii ambao Mungu ametupa Baraka za ushawishi tunaweza tukafikisha ujumbe kwa wenzetu wakatuelewa hivyo tumeshirikiana na Tacaids katika kuwaelimisha vijana namna ya kutumianafasi tulizonazo katika njia chanya zitakazoleta maendeleo katika nchi yetu,” amesema.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Tacaids, Jumanne Issango, amesema vijana ndio kipaumbele katika katika mapambano dhidi ya ukimwi na kwamba ndio kundi lenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya virusi vya ukimwi
“Utafiti uliofanyika 2016/17 unaonyesha kwamba maambukizi ya virusi vya ukimwi katika kundi la vijana kati ya miaka 15-24 wanachangia asilimi 40 ya maambukizi mapya kati ya maambukizi ya idadi ya watu 72,000 kitaifa kwa mwaka hivyo baada ya kuzindua utafiti huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa agizo kwa Tume kutumia wasanii kufikisha ujumbe na elimu ya VVU na Ukimwi na kuhamasisha suala la upimaji kwa vijana,” amesema Issango.
“Majukwaa ya wasanii ni mengi lakini mwaka huu tumebahatika kushirikiana na Wasafi tumeambiwa takribani wasanii 20 wana ushawishi hivyo tumeona ni fursa nzuri katika kuwafikishia ujumbe vijana juu ya maambuziki ya virusi vya ukimwi, eneo muhimu ambalo tutaliwekea msisitizo ni pamoja na matumizi ya Condom, upimaji na sasa hivi vijana wako katika mtandao kwahiyo tutahakikisha tunatumia akaunti za wasanii hawa kupitishia jumbe,” amesema Issango.
Aidha Issango amesema kupitia tamasha hilo wanatarajia kuwafikia vijana milioni 15 na kutakuwa na utoaji wa elimu, ugawaji wa condom na vipeperushi vitakavyokuwa na maelezo juu ya maambukizi hayo ambapo ametoa wito kwa wasanii wengine kufuata mfano wa wasafi wa kutoa elimu juu ya maambikizi ya ukimwi.

Familia ya askofu yamwangukia Rais Magufuli





Na KENNETH NGELESI-MBOZI
FAMILIA ya Askofu Mulilege Mkombo Ambindwile Kameka wa Kanisa la ‘House of  Preyer Shield of  Faith Christian Church’  imemuomba Rais Dk.John Magufuli kuingilia kati na tatizo na kiongozi huyo ambaye kwa sasa inadaiwa yupo mahabusu tangu Januari mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana,  baba mzazi wa askofu huyo, Ambilikile Kameka, alisema anaiomba Serikali ya Rais Magufuli imnusuru kiongozi huyo wa kiroho.
Mchungaji Mwaipungu alisema askofu wao alikamatwa Jenuari 17,  mwaka huu Jijini Dar es Salaam, kwa hutuma za mashaka na urai wake na kufunguliwa kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Machi 17, mwaka huu.
“Awali alikamatwa kwa madai kuwa si raia lakini Mahakama Kuu ikadhibitisha kuwa ni raia halali lakini tangu wakati huo bado anashilikwa sasa sisi hatuelewi hadi sasa. Tunamuomba Rais wetu Dk.John Magufuli na serikali yake watusaidie suala hili,” alisema Mwaipungu
Kutokana na madai hayo mwandishi alimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mmabosasa, ambapo alimtaka mwandishi wa habari hawe na subira wa suala hili kwani yupo nje ya ofisi.

Sunday, July 7, 2019

WANANCHI WAVUTIWA NA PIKIPIKI INAYOGUNDUA KILEVI, HAIWAKI KAMA UMELEWA, HUJAA KOFIA NGUMU AU MWENDO KASI


Katika kukabiliana na changamoto za madhara ya ajali za pikipiki yanayosababishwa na madereva kutovaa kofiangumu (helmet), Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imebuni teknolojia ya kukabiliana na hilo. 

Mwalimu wa fani ya elektroniki kutoka VETA Kipawa, AnethMganga, amebuni mfumo wa kielektroniki unaozuia pikipiki kuwa kampaka dereva awe amevaa kofiangumu (helmet). 

Akizungumza na katika viwanja vya maonesho ya sabasaba,  mwalimu Aneth amesema mfumo huo ukianza kutumika na madereva wa pikipiki utapunguza madhara endapo kunatokea ajali kwa kuwa bila ya kuvaa kofiangumu pikipiki haiwaki na hata ukiwa katika mwendo ikitokea ukavua kofiangumu pikipiki itazimika. 

Aidha, katika usalama barabarani inasaidia kuzuia wizi wa pikipiki kwani mwizi hatoweza kuiwasha bila kofiangumu ambayo imeunganishwa kieletroniki. 

Aneth amesema anaendelea kufanya utafiti nakuboresha zaidi ubunifu huo, lakini ameomba serikali na wadau mbalimbali kuunga mkono ili uweze kuenea, kukubalikana kutumika na waendesha pikipiki katika maeneo mbalimbali nchini

VETA WAJA NA MASHINE YA KUBANGUA KOROSHO





Na Selemani Magali; Daresalaam


ADHA ya kubangua korosho kwa kukoka moto sasa huenda ikabaki historia baada ya mamlaka  ya Ufundi  Stadi (VETA) Songea  kubuni  mashine  ndogo  ya kubangulia  korosho  yenye uwezo wa kubangua debe tatu kwa siku, huku ikiwa na uwezo wa kutenganisha ubora wa bidhaa hiyo. 

Mwalimu kutoka VETA Songea,  Susack Mbulu, amesema hayo katika banda la VETA, lililopo katika  maonesho  ya 43 ya biashara ya Kimataifa (DITF),  yanayoendelea katika viwanja  vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. 

Amesema mashine  hiyo inatumia nguvu  za binadamu  na itawasaidia  wazalishaji  wadogo  kuondokana na mfumo  wa  kukoka  moto  na kukaanga korosho  na kisha kuanza  kuzipasua kwa  mkono, badala yake sasa watatumia  mashine  hiyo. 

"Ukitumia mashine hii, unaweza kutenganisha korosho  kwa ubora, yaani kama ni daraja la kwanza hadi la tatu. Na  iwapo mtumiaji wa  mashine  hii ataanza  kubangua bila kukausha  korosho hizo vyema  zitavunjika na iwapo zitakauka  hazitovunjika bali  zitatoka  sawa," amesema.

Ameongeza kuwa mashine hiyo inauwezo wa kuanza kubangua  korosho  ndogondogo  ama zilizo kubwa kwa kuwa ina meno ya aina mbili ambayo kwa pamoja yanaweza kubangua zao  hilo na kumrahisishia mkulima mdogo. 

Hata hivyo, Mbulu ameushukuru  uongozi wa VETA makao  makuu  kwa ushirikiano  wao  na kuwezesha  kutekeleza  wazo  hilo, ambalo  linaunga  mkono  dhana ya  serikali  ya kufikia  uchumi  wa  kati  ambao  ni  wa  viwanda. 

Amesema katika  kufikia uchumi  wa  viwanda  VETA inaunga mkono  jitihada  hizo ambapo  wataweza  kuwafikia na  kuwasaidia wajasiriamali  wadogo. Lakini pia kusaidia korosho  kuingia  sokoni  katika  hali  ya  ubora.

"Lengo  letu ni kuhakikisha mashine hii inafikia kiwango  cha kutumia umeme au mota ambayo itafikisha hatua ya  kubangua  hata gunia moja  kwa  siku  la  korosho," amesema.

Aidha amewashauri  wafanyabiashara  wa  korosho kuwasiliana na VETA ili kuweza  kupata  mashine  hiyo na kuahidi kuwa  wanaweza  kuifikisha  serikali  katika  uchumi  wa viwanda.

MAGAZETI YA LEO JULAI 07, 2019.

TAKUKURU LINDI WACHUNGUZA UPOTEVU WA ZAIDI YA MILIONI 200.

NA HADIJA HASSAN, LINDI.

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa Lindi imeanza uchunguzi ili kubaini matumizi ya fedha Tsh. 221,000,000, zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya Ukarabati wa Baadhi ya Majengo katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa huo Sokoine.


Hayo yameelezwa na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Lindi Stephen chami jana alipokuwa anatoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli zao katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Aprili hadi juni mwaka 2019.


Chami alisema kupitia dawati lao la utafiti na udhibiti limebaini mapungufu makubwa kwenye ukarabati wa Hospitali hiyo ambapo marekebisho hayo yalihusisha ujenzi wa Wodi ya Watoto, Choo cha wagonjwa pamoja na matenk mawili ya maji ya Lita 50,000 na lita 150,000.


Alisema kupitia Dawati hilo TAKUKURU ilibaini kuwa fedha za ukarabati huo zimekwisha wakati ukarabati huo haujakamilika na baadhi ya vifaa vilivyonunuliwa kwa ajili ya ukarabati huo pamoja na kutokuwepo na maelezo yoyote juu ya upotevu huo.


Chami aliongeza kuwa kufuatia hali hiyo TAKUKURU Mkoa wa Lindi kupitia Dawati lake la Uchunguzi na mashtaka limeshaanza uchunguzi wa kina ili kubaini waliohujumu ukarabati huo ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani.


Nae Ofisa Uchunguzi na Ukaguzi wa Miradi , TAKUKURU Mkoa wa Lindi Michael Manento alidai kuwa Kwenye bajeti ya 2017/2018 hospitali hiyo iliomba fedha sh. 300,000,000. Kwa ajili ya ukarabati wa jingo la utawala, chumba cha X-ray, pamoja na wodi ambapo hata hivyo walipatiwa kiasi cha Tsh. 221,000,000,.


“kwa sababu pesa ilikuja pungufu wao kama menejiment ya Hospitali waliamua kufanya kazi tatu kujenga wodi ya watoto, Vyoo vya Wagonjwa wa nje pamoja na Matank mawili ya maji, hivyo wakati tunakagua kazi ile kulingana na BOQ zao pamoja na manunuzi ya vifaa walivyoandika tukabaini kwamba bajeti iliyowekwa na fedha iliyokuja fedha imeisha kabla ya kazi kukamilika” alifafanua.


Hata hivyo Manento Alizitaja kazi ambazo hazijakamilika katika ukarabaiti huo ni pamoja na ujenzi wa Wodi ambao umefikia hatua ya kupauwa pamoja na vifaa ambayo vinaonekana vimenunuliwa lakini havionekani vilipo