Meneja wa Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Kagera Castro John
Afisa elimu kwa umma TRA Kagera Ruekaza Rwegoshola akitoa elimu ya kodi kwa waandishi wa habari
..............................
Na Alodia Babara,
Bukoba.
Mamlaka ya mapato nchini TRA mkoa wa Kagera imevuka lengo la ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha Januari hadi Machi 2024 na kufikia asilimia 107.
Meneja wa mamlaka hayo mkoa wa Kagera Castro John akizumgumza na waandishi wa habari Aprili 25, 2024 katika kikao kilicholenga kuhamasisha ulipaji kodi wa hiari pamoja na kueleza mafanikio ya ukusanyaji wa kodi kipindi cha Januari hadi Machi, 2024.
"Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Kagera tulipanga kukusanya shilingi bilioni 28.24 lakini tulikusanya shilingi bilioni 30.2 na hivyo kuvuka lengo na kufikia asilimia 107" amesema John.
John ametolea ufafanuzi wa kodi mpya ya bodaboda ambayo inapaswa kulipwa kwa mwaka elfu 65,000 ambapo kila robo mwaka zinapaswa kilipwa shilingi 16,200 na zinalipwa kwa awamu nne hivyo akawaomba wamiliki wa pikipiki za biashara kulipa kodi hiyo.
Aidha katika mkutano huo amewaomba waandishi wa habari kuendelea kuhamasisha walipakodi kulipa kwa wakati ili kuongeza mapato ya nchi.
Afisa elimu kwa umma Ruekaza Rwegoshola ameeleza kuwa, kupitia ulipaji kodi serikali imekuwa ikitoa huduma mbalimbali kwa wananchi wake zikiwemo huduma za Afya, maji, ujenzi wa miundombinu ya barabara na vyumba vya madarasa.
Amesema, asilimia 70 ya mapato ya serikali yanatokana na ukusanyaji kodi na kwa mwaka 2023/2024 serikali ilipitisha bajeti ya trioni 44.39 na TRA ilipewa lengo la kukusanya trioni 26.75 hivyo TRA inayo kazi kubwa kuhakikisha inakusanya kodi.
No comments:
Post a Comment