Posts

ASKOFU MKUU TAG ACHANGIA MIL 10 UJENZI KANISA LA KCC

Image
  ASKOFU MKUU TAG ACHANGIA MIL 10 UJENZI KANISA LA KCC Na Allan Kitwe, Tabora ASKOFU Mkuu wa Kanisa la TAG Dkt Barnabas Mtokambali amechangia kiasi cha shilingi milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la Kitete Christian Centre (KCC) la Mjini Tabora ambalo ni Makao Makuu ya Jimbo jipya la Tabora Kati. Askofu Mkuu ameahidi kutoa mchango huo kwenye ibada maalumu ya uzinduzi wa Jimbo jipya la Tabora Kati lililopo Mjini Tabora baada ya kufurahishwa na kazi nzuri ya ujenzi wa kanisa hilo la kisasa linalojengwa na Kanisa la KCC. Ameeleza kuwa kanisa linalojengwa kwenye Makao Makuu hayo ya Jimbo jipya ni la kiwango cha juu, linavutia sana, hivyo akaahidi kuwaunga mkono ili kufanikisha maono hayo ya kujengwa kanisa la kisasa ambalo sasa limefikia asilimia 70. Dkt Mtokambali amebainisha kuwa jengo hilo litaleta heshima kwa TAG na kuheshimisha Makao Makuu wa Jimbo ambayo yamezinduliwa rasmi katika ibada hiyo iliyohudhuriwa na Viongozi wa serikali, Maaskofu, wachungaji na waumini. ...

RPC PWANI, AANGALIA ATHARI ZA ULISHAJI WA MIFUGO ENEO LA CHAURU.

Image
  RPC PWANI, AANGALIA ATHARI ZA ULISHAJI WA MIFUGO ENEO LA CHAURU. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Salim Morcase, amefanya ziara katika eneo linalolalamikiwa na Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU), kwa lengo la kujionea athari zilizosababishwa na ulishaji wa mifugo katika eneo hilo pamoja na uharibifu wa miundombinu ya umwagiliaji. Katika ziara hiyo, Kamanda Morcase amepita katika maeneo mbalimbali yanayolalamikiwa na wakulima na kujionea hali halisi ya uharibifu unaodaiwa kusababishwa na mifugo kuingia katika mashamba na maeneo ya umwagiliaji. Aidha, amesikiliza maelezo kutoka kwa viongozi wa Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) pamoja na wakulima kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo, ikiwemo uharibifu wa miundombinu na athari zinazotokana na mifugo kuingia katika maeneo ya kilimo. Kamanda Morcase amesisitiza umuhimu wa pande zote kuheshimu maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufu...

MBUNGE MARIAM IBRAHIM KUCHELE AWAPIGA JEKI YA MRADI WA PIKIPIKI WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI

Image
  MBUNGE MARIAM IBRAHIM KUCHELE AWAPIGA JEKI YA MRADI WA PIKIPIKI WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI Na mwandishi wetu ,Pwani    Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani ,Mhe Mariam Ibrahimu  katika  kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwakomboa wanawake kujikwamua  kiuchumi  ameamua kutoa pikipiki zipatazo 10 kwa umoja wa wanawake Tanzania  (UWT) Mkoa wa Pwani ikiwa ni moja ya mradi ambao utawasaidia kuondokana na wimbi la umasikini. Akikabidhi pikipiki hizo kwa uongozi wa UWT Mkoa wa Pwani wakati wa halfa ambayo imefanyika katika viwanja vya nje ya  Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha ambapo amebainisha kwamba wa pikipiki hizo zitakwenda kuwa ni mkombozi mkubwa na kuwaletea mabadiliko na mageuzi katika kuachana na dhana ya kuwa tegemezi  kila kukicha na badala yake  wajitegemee wao wenyewe. Aidha amebainisha kwamba  lengo lake kubwa sio kujinufaisha yeye mwenyewe bali ni kusaidia jamii ...

WAISLAMU SAADANI WAOMBA MSAADA KUJENGEWA MSIKITI.

Image
  WAISLAMU SAADANI WAOMBA MSAADA KUJENGEWA MSIKITI. Na Omary Mngindo, Saadani WAISLAMU Msikiti wa Masjid Bilal uliopo Kijiji cha Saadan National Park, Kata ya Mkange Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wanaomba msaada wa kuukarabati Msikiti wao ili waweze kufanya ibada kwa utulivu. Msikiti huo wa Kale ambao umejengwa na Wakoloni miaka 200 iliyopita kwa sasa umechakaa hivyo waumini hao wameanza kuukarabati kwa nguvu zao wenyewe. Imamu wa Msikiti huo Maalimu Kitoro Fundi Chande alisema kuwa Msikiti huo umedumu kwa miaka mingi, hatua ambayo inapaswa kufanyiwa ukarabati. "Huu Msikiti umejengwa na Wakoloni miaka 200 iliyopita tunaendelea na kuswali, lakini kwa sasa unastahili kufanyiwa ukarabati," alisema Imamu Kitoro. Aliongeza kuwa "Tunahitaji Mabati, Mbao, rangi, Vigae (Tiles sehemu za kuchukulia udhu) na vifaa mbalimbali vitakavyofanikisha kuboreshwa kwa Msikiti wetu," alisema Kitoro. Kwa upande wake Muumini msikitini hapo Ally Majimengi alisema ...

SOLA NA KOMPYUTA ZA GURUMO ZAMPA SOMO RIDHIWANI.

Image
  SOLA NA KOMPYUTA ZA GURUMO ZAMPA SOMO RIDHIWANI. Na Omary Mngindo, Kimange TAA za Umeme wa Jua zilizopelekwa kwenye shule ya Sekondari Kimange, Kata ya Kimange Halmashauri ya Chalinze Bagamoyo Pwani, zimempa somo Waziri wa Utumishi Ridhiwani Kikwete. Taa hizo na Seti 10 za Kompyuta zilizopelekwa shuleni hapo na Diwani Juma Gurumo, zimekuwa msaada katika kuhakikisha Walimu wanafundisha na Wanafunzi wanapokea masomo. Ridhiwani alisema kuwa amepata somo zuri atakalokwenda kuliuza kwa viongozi mbalimbali, kuhusiana na matumizi ya Nishati hiyo inayosaidia kupunguza gharama za matumizi ya Umeme. "Hizi Kompyuta zingekuwa zinatumia Umeme gharama zingekuwa juu sana na sidhani kama tungeziweza, nakupongeza Diwani Gurumo kwa kazi kubwa naiona Kimange ikisonga mbele kwa kasi" alisema Waziri Kikwete. Aidha alipongeza ununuzi wa Kompyuta ambazo zinawapatia fursa Wanafunzi kusoma Sayansi kwa vitendo, huku akisisitiza kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia inapeleka fedha ...

WAZIRI MCHENGERWA NA MHE.MARIAM IBRAHIM WASHUSHA NEEMA KWA WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI

Image
  WAZIRI MCHENGERWA NA MHE.MARIAM IBRAHIM  WASHUSHA NEEMA KWA WANAWAKE WA UWT MKOA WA PWANI Na Mwandishi wetu , Pwani Waziri wa  Afya Mohamed  Mchengerwa  katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita  Dkt. Samia Suluhu Hassaan katika kuwakomboa wanawake na kuimarisha jumuiya zao  ameamua kuchangia kiasi cha shilingi milioni 35 kwa ajili ya kuwasaidia umoja wa wanawake wa (UWT) Mkoa wa Pwani waweze kukamilisha malengo yao waliyojiwekea ikiwemo suala la ujenzi  wa nyumba za makatibu wa Wilaya na ngazi ya Mkoa. Mchengerwa ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi  (MNEC )  Taifa ameyabainisha  hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika  kikao cha baraza la kawaida la UWT Mkoa wa Pwani ambalo limehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama pamoja na viongozi wa serikali akiwemo Mkuu mpya  wa Mkoa wa  Pwani.   Mchengerwa amebainisha  kwamba lengo lake kubwa ni kuendelea kutoa sapoti kwa k...

π™ˆπ˜Όπ™†π˜Όπ™ˆπ™ π™’π˜Ό π™π˜Όπ™„π™Ž π˜Όπ™Žπ™ƒπ™π™ƒπ™π˜Ώπ™„π˜Ό π™π™π™„π˜Όπ™…π™„ π™Žπ˜Όπ™„π™‰π™„, π™ˆπ™‹π˜Όπ™‰π™‚π™Š π™’π˜Ό π™π™Žπ™ƒπ™„π™π™„π™†π™„π˜Όπ™‰π™Š π™’π˜Ό π™π˜Όπ™‰π™€π™Žπ˜Ύπ™Š π™‰π˜Ό π˜Ύπ™π˜Ώπ˜½ π™†π™π™’π˜Όπ™’π™€π™•π™€π™Žπ™ƒπ˜Ό π™’π˜Όπ™‰π˜Όπ™‰π˜Ύπ™ƒπ™„ π™†π™π™‹π˜Όπ™π˜Ό π™π™ˆπ™€π™ˆπ™€.

Image
  π™ˆπ˜Όπ™†π˜Όπ™ˆπ™ π™’π˜Ό π™π˜Όπ™„π™Ž π˜Όπ™Žπ™ƒπ™π™ƒπ™π˜Ώπ™„π˜Ό π™π™π™„π˜Όπ™…π™„ π™Žπ˜Όπ™„π™‰π™„, π™ˆπ™‹π˜Όπ™‰π™‚π™Š π™’π˜Ό π™π™Žπ™ƒπ™„π™π™„π™†π™„π˜Όπ™‰π™Š π™’π˜Ό π™π˜Όπ™‰π™€π™Žπ˜Ύπ™Š π™‰π˜Ό π˜Ύπ™π˜Ώπ˜½ π™†π™π™’π˜Όπ™’π™€π™•π™€π™Žπ™ƒπ˜Ό π™’π˜Όπ™‰π˜Όπ™‰π˜Ύπ™ƒπ™„ π™†π™π™‹π˜Όπ™π˜Ό π™π™ˆπ™€π™ˆπ™€. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ametoa wito kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kushirikiana na wadau husika wa sekta binafsi kuandaa mpango utakaowawezesha wananchi kununua umeme kwa mkopo kama ilivyo mikopo katika mitandao ya simu ili kuwasaidia wananchi wanapokuwa na uhitaji wa umeme lakini hawana fedha.   Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati wa hafla ya utiaji Saini Mkataba wa Uzinduzi wa Mpango wa Ufadhili wa Uunganishaji Umeme kwa Wananchi, kati ya Benki ya CRDB na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Amesema hatua hiyo itaweza kusaidia wananchi kuendelea kutumia huduma ya umeme na kufanya uzalishaji mali au ma...