Posts

MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA.

Image
  MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya utoaji wa tuzo za 19 za Rais za Wazalishaji Bora Viwandani, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam.   Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu wa Rais ametoa wito kwa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na wazalishaji wa saruji nchini, kuhakikisha wanatafuta suluhu ya haraka ili kurejesha bei ya kawaida ya saruji kwa wananchi. Amesema maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona wananchi wanaweza kununua mfuko wa saruji kwa gharama nafuu hivyo ni lazima kuoanisha uzalishaji wa malighafi zote zinazochangia katika uzalishaji wa saruji ili bidhaa hiyo ipatikane kwa urahisi.   Halikadhalika, Makamu wa Rais amesema ni muhimu kufanya tathimini ya ukuaji wa viwanda hapa ...

MBEYA DC YAPOKEA MRADI KUHIFADHI MAZINGIRA BONDE LA MTO SONGWE

Image
  MBEYA DC YAPOKEA MRADI KUHIFADHI MAZINGIRA BONDE LA MTO SONGWE Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya leo tarehe 03 Septemba,2026 imepokea Mradi wa Uhifadhi wa Mazingira (Sustainably Manage the Basin Natural Resources) kutoka Tume ya Pamoja Kati ya Nchi ya Tanzania na Malawi inayoshughulikia Uhifadhi wa Bonde la Mto Songwe (SONGWECOM) unaomwaga maji yake katika Ziwa Nyasa pamoja na uendelezaji wake. Akisoma taarifa hiyo mbele ya ugeni kutoka Wizara ya Maji Makao Makuu Dodoma, Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Mbeya, Aidan Mlawa amesema kuwa mradi huo ulifanyika katika Tarafa ya Isangati kwenye Kata za Izyra na Iwiji ndani ya vijiji vinne (4) ambavyo ni: Izyra; Isende; Masewe na Izumbwe II.  Amesema mradi huo umelenga kuwajengea uwezo wa kiuchumi wananchi ambao wanafanya shughuli za kiuchumi na kijamii katika vyanzo na kingo za mito inayomwaga maji yake katika Mto Songwe unaopeleka maji katika Ziwa Nyasa ili ziweze kuachana na uharibifu wa mazingira katika maeneo hayo. Mkurugenzi Msaidi...

SHULE YA MSINGI IPULI YAPEWA TUZO YA UFANISI

Image
  SHULE YA MSINGI IPULI YAPEWA TUZO YA UFANISI Na Allan Kitwe, Tabora HALMASHAURI ya Manispaa Tabora imetoa tuzo maalumu ya pongezi kwa Uongozi wa Shule ya Msingi Ipuli iliyopo katika Kata ya Ipuli Mjini Tabora kwa usimamizi mzuri wa fedha za maendeleo zilizopelekwa shuleni hapo. Akikabidhi tuzo hiyo (Cheti cha Pongezi) leo, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Ghullam-Hussein Dewj amempongeza Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Chiku Mwaka na Kamati yake kwa kusimamia vizuri maboresho ya miundombinu. Amesema kuwa Uongozi wa shule hiyo umeonesha weledi mkubwa kwa kusimamia kwa dhati mradi wa uboresha elimu (GPE) uliotekelezwa na serikali shuleni hapo kwa mwaka wa fedha uliopita kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 60. ‘Chini ya usimamizi wa Mwalimu Mkuu na Kamati ya Shule, Mradi umetekelezwa kwa ufanisi wa hali ya juu hali iliyopelekea mazingira ya shule hiyo kubadilika kwa kiasi kikubwa na kufanya watoto na wazazi kupenda shule yao’, ameeleza.     ‘Tunakupongeza sana Mwalimu M...

WATAALAMU WA HALMASHAURI BAGAMOYO, WAKAGUA MIRADI

Image
  WATAALAMU WA HALMASHAURI BAGAMOYO, WAKAGUA MIRADI. Timu ya Wataalam Halmashauri ya Mji Bagamoyo  imefanya Ziara ya ukaguzi wa Miradi Maendeleo katika Halmashauri hiyo. Timu hiyo ya Wataalamu imefanya ukaguzi wa Ujenzi wa fremu za kibiashara eneo la soko jipya ambapo Mradi huo upo katika hatua za mwishoni kukamilika kufikia tarehe 30 September 2026. Aidha Kamati imekagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa manne yanayojegwa kwa nguvu ya wananchi Kata ya Kisutu na kupongeza wananchi hao kWa Jitihada kubwa walizofanya za kuanza ujenzi wa shule Mpya katika eneo hilo. Pia Kamati imekagua ujenzi wa Matundu 12 ya vyoo shule ya Msingi Bigilo Kata ya Makurunge kamati hiyo imeshauri Mradi kuendelea kusimamiwa kwa karibu zaidi ili kujegwa kwa ubora unaotakiwa kurekebisha mapungufu ambayo yanatakiwa kurekebishwa. Vilevile kamati imetoa pongezi kwa Wasimamizi wa ujenzi Kamati ya ujenzi katika shule hiyo kwa usimamizi nzuri pamoja na kutoa Hamasa kWa wananchi kutoa ushirikiano kwa kipindi chote...

MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KUANZA JANUARI 2027

Image
  Na Alodia Dominick,  Bukoba, Mradi wa bomba la mafuta ambao utekelezaji wake wa jumla umefikia asilimia 87.7 unatarajia kukamilika na kuanza rasmi Januari 15,2027. Mradi huo ambao mkataba wake ulisainiwa mwaka 2021 unatarajiwa kuanza rasmi ifikapo Januari 15, 2027 na kutokana na mkataba mradi utadumu takribani miaka 25. Mratibu wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kusafirisha mafuta ghafi Afrika Mashariki (EACOP) Jumanne Saidi akitoa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari mkoani Kagera juu ya mradi wa bomba la mafuta na maendeleo yake ameeleza kuwa, mradi huo utaanza rasmi Januari 15,2027. Amesema sh.bilioni 35.6 zimetumika kulipa fidia kwa wananchi wapatao 10,144 maeneo yote yanayopitiwa na bomba la mafuta na nyumba zilizoguswa ni 340, kwa Kagera ni nyumba 119 ambapo waguswa kwa Kagera wako 118.  "Mikoa inayopitiwa na bomba la mafuta ni nane ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Manyara, Dodoma na Tanga na katika mkoa wa Kagera unapita katika wilay...

MIL 360 ZA BAKAA KUTEKELEZA MIRADI VIPORO MANISPAA TABORA

Image
  MIL 360 ZA BAKAA KUTEKELEZA MIRADI VIPORO MANISPAA TABORA Na Allan Kitwe, Tabora MADIWANI wa halmashauri ya manispaa ya Tabora wameazimia fedha zote zilizotengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha ulioishia Juni 2026 na hazikutumika (bakaa) zisirudishwe TAMISEMI bali zitumike kukamilisha miradi viporo. Hayo yamebainishwa na Katibu wa Madiwani wa CCM Bahati Adam Ntiruhungwa (diwani wa Kata ya Ng’ambo) alipokuwa akitoa maazimio yao kwenye kikao cha robo ya nne ya baraza kilichoketi leo Mjini hapa. Ameeleza kuwa madiwani ndio wawakilishi wa wananchi katika Kata zao, hivyo wana dhamana ya kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao inakamilika kwa wakati kwa manufaa ya wananchi. ‘Madiwani wa CCM tumeazimia miradi viporo yote ikamilishwe, na fedha za bakaa, zaidi ya shilingi milioni 364 ziombewe kibali ili zitumike kumalizia miradi iliyoanza kutekelezwa katika msimu uliopita’, amebainisha. Ntiruhungwa ameitaka Ofisi ya Mkurugenzi kuhakikisha wakazi wa kata zote wananufaika n...

SUBIRA MGALU AULIZA HATUA YA FIDIA KWA WANANCHI WA BARABARA YA MAKOFIA–MLANDIZI

Image
  SUBIRA MGALU AULIZA HATUA YA FIDIA KWA WANANCHI WA BARABARA YA MAKOFIA–MLANDIZI Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Mhe. CPA Subira Khamis Mgalu, ameuliza Serikali kuhusu hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya kuwalipa fidia wananchi wanaopitiwa na mradi wa Barabara ya Makofia–Mlandizi katika Kata ya Yombo. Akitoa swali la nyongeza, Mhe. Subira amesema barabara hiyo imefungamanishwa na mpango wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo pamoja na eneo la viwanda la Kwara, hivyo umuhimu wake unaendelea kuongezeka. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema kuwa Wizara tayari imekamilisha tathmini ya fidia na imewasilisha mahitaji hayo katika Wizara ya Fedha. Amesema Serikali inaendelea na taratibu za kupata fedha, na mara fedha zitakapopatikana, wananchi waliostahili watalipwa fidia ili hatua za ujenzi wa barabara hiyo ziweze kuendelea.