MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KUANZA JANUARI 2027
Na Alodia Dominick, Bukoba, Mradi wa bomba la mafuta ambao utekelezaji wake wa jumla umefikia asilimia 87.7 unatarajia kukamilika na kuanza rasmi Januari 15,2027. Mradi huo ambao mkataba wake ulisainiwa mwaka 2021 unatarajiwa kuanza rasmi ifikapo Januari 15, 2027 na kutokana na mkataba mradi utadumu takribani miaka 25. Mratibu wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kusafirisha mafuta ghafi Afrika Mashariki (EACOP) Jumanne Saidi akitoa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari mkoani Kagera juu ya mradi wa bomba la mafuta na maendeleo yake ameeleza kuwa, mradi huo utaanza rasmi Januari 15,2027. Amesema sh.bilioni 35.6 zimetumika kulipa fidia kwa wananchi wapatao 10,144 maeneo yote yanayopitiwa na bomba la mafuta na nyumba zilizoguswa ni 340, kwa Kagera ni nyumba 119 ambapo waguswa kwa Kagera wako 118. "Mikoa inayopitiwa na bomba la mafuta ni nane ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Manyara, Dodoma na Tanga na katika mkoa wa Kagera unapita katika wilay...