Tuesday, April 9, 2024
Saturday, March 30, 2024
TUISOME KWA WINGI QURAN TUKUFU-DK.MWINYI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya kiislamu kuendelea kuisoma kwa wingi Quran Tukufu katika kipindi hiki cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika fainali za kwanza za Mashindano ya kuhifadhi Quran Tukufu Afrika Mashariki yanayosimamiwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar ikiwemo washiriki tisa kutoka nchi za Afrika Mashariki katika Uwanja wa New Amaan Complex, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 30 Machi 2024.
Aidha Rais Dk.Mwinyi ameiomba Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar kuzidisha juhudi za malezi ya vijana na kuwaongoza katika maadili na tabia njema ili wawe raia wema na wenye hofu ya Mungu.
Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuunga mkono mashindano hayo kufanyika kila mwaka.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amezipongeza Taasisi za Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar kwa kuandaa mashindano hayo makubwa ambayo yanaitangaza Zanzibar.
Mshindi wa kwanza wa Mashindano hayo ni Mahmoud Kassim Nassor wa Zanzibar aliyepata shilingi milioni 30 mshindi wa pili Abdourahamane Papa Said kutoka Comoro shilingi milioni 20 , na mshindi wa tatu Abdulrahman Mussa kutoka Kenya shilingi milioni 10.
Saturday, March 16, 2024
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI BAGAMOYO, AWAAPISHA MAKARANI WA UCHAGUZI MDOGO KATA YA FUKAYOSI.
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Bagamoyo Shauri Selenda, amewataka makarani waongozaji katika uchaguzi mdogo wa kata ya Fukayosi Halmashauri ya Bagamoyo, kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa mafunzo watakayopewa.
Selenda ameyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo kwa Makarani waongozaji wa uchaguzi mdogo kata ya Fukayosi Haashauri ya Bagamoyo ambapo alisema makarani wanapaswa kuzingatia kanuni na sheria za uchaguzi katika kutekeleza majukumu yao kama watakavyoelekezwa katika mafunzo hayo.
Alisema kazi ya ukarani wa uchaguzi inahitaji uvumilivyu, subira na busara katika utendaji wake kwani kazi hiyo inawakutanisha na watu tofauti ambao wanahitaji kusikilizwa, kuelekezwa na kuongozwa juu ya kile wanachopaswa kufanya katika kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi.
Makarani hao walikula kiapo cha kutekeleza majukumu hayo tayari kwaajili ya uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Machi 20, 2024.
Kiti cha udiwani kata ya Fukayosi kimebaki wazi baada ya aliyekuwa Diwani wa kata hiyo kufariki dunia kwa maradhi ya shinikizo la damu mnamo mwezi Novemba mwaka 2023.
Akizungumza kwa niaba ya Makarani wenzake, Athumani Hassan Fundi, amesema watahakikisha wanazingatia kile wanachofundishwa ili kutekeleza majukumu yao kwa weledi
Alisema nia wameipokea kazi hiyo kwa moyo mmoja na wapo tayari kufuata maelekezo kwa mujibu wa sheria za uchaguzi ili kufanikisha kazi hiyo muhimu.
Monday, February 19, 2024
MILIONI 800 KUWASAIDIA WAHANGA WA MAFURIKO MULEBA.
Na Alodia Babara
Bukoba,
Walengwa wapatao 482 walioathirika na mafuriko pamoja na upepo mkali katika wilaya za Muleba na Manispaa ya Bukoba mwaka jana wanatarajia kupata msaada wa kibinadamu wenye malengo mbalimbali utakaoghalimu zaidi ya sh. milioni 800 kutoka taasisi zisizo za kiserikali.
Msaada huo ambao unatolewa na Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi kwa ufadhili wa taasisis inayojihusisha na shughuli za kibinadamu kwa watu wenye majanga nchini Tanzania (TCRS) na taasisi ya Actalliance Tanzania Forum utakuwa wa mwaka mmoja utawezesha kutimiza malengo sita ambayo ni msaada wa chakula, uboreshaji wa makazi, msaada wa kisaikrojia, huduma za maji, elimu na Afya na usafi wa mazingira.
Akizindua mradi huo Februari 19, mwaka huu mkuu wa mkoa wa Kagera Fatuma Mwassa alisisitiza mambo matatu ikiwemo matumizi ya fedha za walengwa, usimamizi mzuri pamoja na elimu ya maafa kwa walengwa.
Mwassa alieleza kuwa, anazo taarifa kuwa mradi huo utahusisha maswala ya fedha, akaelekeza maafisa wanaohusika na maafa upande wa Serikali kama maafisa maendeleo ya jamii, watendaji wa kata, madiwani na viongozi hadi ngazi ya wilaya kushirikiana na uongozi wa kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania dayosisi ya Kaskazini Mgharibi katika uhakiki wa walengwa ambao ni harisia ili mradi usije kunufaisha ambao siyo walengwa.
“Viongozi kuanzia ngazi ya kitongoji hadi wilaya ni lazima kushiriki kikamilifu wakati wa uhakiki na kutoa huduma kwa walengwa wanaostahili na ndiyo maana nyinyi viongozi mmehudhuria uzinduzi huu” amesema Mwassa.
Amesisitiza hilo baada ya kukumbana na changamoto wakati wa kugawa chakula kwa waathirika hao kilicholetwa na kamati ya maafa kutoka ofisi ya Waziri mkuu kwani ziliingizwa siasa na likaibuka vuguvugu wakitaka watu wote wapewe msaada huo na watu waliokuwa kwenye kata zilizokumbwa na maafa wakajitokeza wakidai wote wana shida.
Amesema tathimini ilishafanyika wenye uhitaji walishatambuliwa na kuwa viongozi wasiende kuzua la kuzua kwa kulazimisha wengine kuingia kwenye hiyo risti, kaya ambazo zitahusika baada ya uchunguzi ni 482 inajullikana na ndiyo bajeti iliyopo.
“Nitumie nafasi hii kusisitiza kuwa fedha zitakazotolewa zitumike kwa matumizi yaliyokusudiwa zisiwe chanzo cha ndoa kuvunjika na kusababisha ukatili wa kijinsia katika familia za walengwa” amesema Mwassa
Aidha aliongeza kuwa, mradi ujikite sana kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujifunza namna ya kukabiliana na maafa, mfano wananchi waelimishwe kutojenga sehemu hatarishi zinazoweza kuhatarisha maisha yao na familia zao serikali inaposema maeneo haya hayafai kujengwa makazi basi watu wote wakubaliane na waache maeneo hayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi inayojihusisha na shughuli za kibinadamu kwa watu wenye majanga nchini Tanzania TCRS Samwel Mlay amesema kuwa, mradi utakuwa wa mwaka mmoja ulianza kutekelezwa Desemba mwaka jana na utakamilika Desemba mwaka huuu, utawezesha kutimiza malengo sita ambayo ni msaada wa chakula, uboreshaji wa makazi, msaada wa kisaikrojia, huduma za maji, elimu na afya na usafi wa mazingira.
Mlay amesema, mradi utaghalimu zaidi ya shl milioni 800 walengwa wapatao 482 walioathirika na mafuriko pamoja na upepo mkali katika wilaya za Muleba na Manispaa ya Bukoba mwaka jana watanufaika na mradi huo ambapo katika wilaya ya Muleba ni kata mbili za Kashalunga na Kalambi na Manispaa ya Bukoba ni kata nne za Rwamishenyi, Hamugembe, Bilele na Kashai zinatarajia kupata msaada wa kibinadamu katika nyanja mbalimbali kutoka katika taasisi zisizo za kiserikali
Diwani wa kata ya Kashai Ramadhan Kambuga amesema kuwa, kutolewa kwa misaada hiyo kutasaidia kupunguza maumivu kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko na upepo mkali.
Amesema wananchi waliokumbwa na athari za mafuriko na upepo walishatambuliwa hivyo hawatakwenda kinyume na wale waliotambuliwa kikubwa viongozi wa Serikali walishawatembelea na kuwabaini na mahitaji ya kila mmoja, hawataongeza wala kupunguza mlengwa kila mmoja alishawekwa kwenye utaratibu hivyo uadilifu, busara na hekima vitaendelea kutumika.
DIVISHENI YA ELIMU SEKONDARI YAFANYA KIKAO KAZI CHALINZE.
Divisheni ya Elimu Sekondari katika Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo, imefanya kikao kazi kufanya tathmini ya utendaji kazi ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya matokeo ya kidato cha pili na cha nne kwa mwaka 2023 ili kuweka mikakati mbalimbali katika kuboresha utendaji kazi ili kufikia Malengo ya utendaji kazi (Key Performance Indicators).
Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 19 Februali 2024 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete uliopo katika Halmashauri hiyo na kuhusisha Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali na binafsi na walimu wa Taaluma katika Shule zote za Sekondari katika Halmashauri ya Chalinze.
Akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi Afisa Elimu wilaya ya Chalinze, Bi Salama Ndyetabura alieleza mafanikio na Changamoto mbalimbali zinazoikabili Divisheni ya Elimu Sekondari, huku akiishukuru Halmashauri ya Chalinze kwa kuweza kujenga maabara kwa baadhi ya Shule za Sekondari katika Halmashauri hiyo
Afisa Elimu Sekondari, ametoa pongezi kwa wakuu wa Shule kwa usimamizi bora wa miradi kwa kumpongeza Mkuu wa Shule Changalikwa Mwl Benasian Ituja kwa Kusimamia ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Mbwewe kwa kuisimamia kwa weledi na maarifa hata kutotengeneza hoja yoyote ya ukaguzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Bwana Ramadhani Possi ametoa pongezi za dhati kwa walimu wote wa Sekondari, Maafisa Elimu na Maafisa kata kwa jinsi wanavyofanya kazi kwa weledi na uadilifu katika kutoa maarifa kwa watoto wa Taifa hili.
Possi aliwapongeza kwa kukuza taaluma na kupata matokeo mazuri ya kidato cha nne na cha pili kwa mwaka 2023.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri amewasisitiza watendaji wa kata kushirikiana na walimu ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza kuripoti kwa wakati na kuweza kuendelea na masomo.
Saturday, February 10, 2024
MIZIGO YAONGEZEKA BANDARI YA MTWARA
Na Albert Kawogo, Mtwara
BANDARI ya Mtwara imeongeza kiasi cha mizigo inayohudumiwa hapo kutoka kiasi cha tani laki nne hadi tani milioni 1.6 katika kipindi cha mwaka 2022/2023.
Chachu ya ongezeko hilo linatokana na hatua kubwa ya kimkakati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA kufanya maboresho yenya thamani ya shilingi bilioni 157.8 kwenye eneo la gati ya bandari hiyo sambamba na ununuzi wa mtambo wa kupakia na kushusha mizigo.
Ferdinand Nyathi meneja wa Bandari ya Mtwara amewaeleza wahariri wa habari kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) waliotembelea bandari hiyo kuwa, jitihada kubwa zinazofanywa na TPA kwenye uwekezaji wa miundombinu ya bandari ndio zinaongeza ufanisi katika utendaji.
"Uwekezaji umeimarishaji mifumo ya bandari na matunda ya kazi hii ni kwamba msimu wa korosho ambao sasa uko mwishoni tumeweza kuhudumia meli kubwa 28" Alisema Nyathi
Nyathi aliendelea kufafanua kuwa Bandari hiyo imekuwa ikisafirisha makaa ya mawe, saruji ya kiwanda Cha Dangote Cement ambapo saruji hiyo husafirishwa kupelekwa Zanzibar na Comoro.
Naye Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Dk George Fasha alisema Bandari ya Mtwara ni Bandari ya kimkakati kwa ushoroba wa kusini.
Dk Fasha alisema mpango wa sasa ni kuanza usafirishaji wa madini ya graphite kutoka Wilaya Ruangwa Lindi,huku akisisitiza kuwa ili kuimarisha ushoroba huo TPA inaendelea kuboresha Bandari za MbambaBay ili iweze kusaidia bandari ya Mtwara kuhudumia mizigo ya Malawi na Msumbiji.
Thursday, February 8, 2024
RAIS SAMIA ASIKITISHWA NA MAUAJI YA PALESTINA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania inasikitishwa na vita vinavyoendelea Palestina vinavyosababisha mauaji ya watoto na raia wasio na hatia.
Rais Samia ameyasema hayo Tarehe 07 february 2024 katika sherehe za mwaka mpya 2024 (Diplomatic Sherry Party) kwa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya kimataifa zilizofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.
Aidha, amesema Tanzania inaunga mkono usuluhishi kati ya Palestina na Israeli kwa kutoa wito wa kusitisha mapigano na kupatiwa misaada ya kibinadamu.
Wakati huohuo Rais Samia amesema Haki, Demokrasia, Sheria na Utawala bora vitadumishwa kwa watu wote wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Amesema ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki, kikosi kazi huru cha kupitia na kushauri mageuzi muhimu katika mfumo wa siasa kiliundwa ambapo kiliwasilisha ripoti yake mwaka 2023
Rais Samia pia amesema mapendekezo mengi ya kikosi kazi yaliyopokelewa na serikali na wadau wote yalihusu kuongeza uwazi katika michakato ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi.






















































