Thursday, November 7, 2019

VUVUZELA KUTUMIKA KURUDISHA WANYAMA HIFADHINI.

 Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abeli Mtui akizungumza na waandishi ofisini kwake ambao hawapo pichani waliotembelea hifadhi hiyo kuhusu vivutio vilivyopo kwenye hifadhi hiyo.

Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abeli Mtui akiwaonyesha waandishi wa habari bwawa la Dindira lililopo hifadhini humo ambalo linatumiwa na wanyama kwa ajili ya kunywa maji  ambao walitembelea.

Bwawa la Dindira lililopo hifadhini humo ambalo linatumiwa na wanyama kwa ajili ya kunywa maji.
.........................................

HIFADHI ya Taifa ya Mkomazi iliyopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro imeeleza kwamba watatumia mavuvuzela na tochi zenye mwanga mkali kuwafukuza wanyama wanaovamia makazi ya wananchi wakiwemo Tembo na kuwarudisha kwenye hifadhi.

Hayo yalisemwa na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, Abeli Mtui wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao walitembelea hifadhi hiyo.

Alisema kwamba watashirikiana pia na baadhi ya taasisi binafsi ambazo zimebuni mbinu za kuwafukuza wanyama hao ikiwemo la wakulima kufundishwa namna ya kuweka uzio wa mabati ambayo yanayopiga kelele na imesaidia kwa asilimia kubwa.


Kamishna huyo Msaidizi wa Uhifadhi alisema wamefanya jitihada zote huku akitoa wito kwa wananchi wazingatie na wanaona ufumbuzi mkubwa ni yale maeneo ambayo yalikuwa ni mapitio ya wanyama kufanya matumizi bora ya ardhi, rafiki  yanayoendana na yasiwe ya kilimo au yale ya kuchunga ili kupunguza mgongano wa kuharibu mazao.

“Kikubwa ni kutenga au kufanya matumizi bora ya ardhi kwenye vijiji yale maeneo yenye historia ya kupita wanyama watu wayapangie matumizi ambayo ni rafiki au matumizi yanayoendana na yasiwe ya kilimo au yawe ya kuchungia ili kupunguza mgogano wanyama kuharibu mazao”Alisema.

Aidha alisema kwamba wana matumaini makubwa na  kuna mikakati wanaoiweka ili wasaidiane na viongozi wa vijiji katika kukamilisha mipango bora ya matumizi ya ardhi ili maeneo yaliyo onekana ni mapito ya wanyama yaweza kufanyiwa matumizi mazuri yanayoendena na uhifadhi wa wanyama pori pia na matumizi ya mifugo kama malisho.


Alieleza pia kwamba hifadhi hiyo ni moja kati ya hifadhi ambayo inapakana na Hifadhi ya Tsavo West ya Kenya na katika mfumo wa ikolojia ya savo mkomazi kwa upande wa Kenya ndio eneo lenye idadi kubwa ya Tembo kwa mujibu wa sensa miaka iliyopita kwenye huo mfumo kulikuwa na tembo 23000.


Alisema na mwaka 2014 hesabu ilifanyika na walionekana tembo 60 na wao wamefanya sensa mwaka huu wakati wa kiangazi wamepata tembo zaidi ya 1000 ina maana idadi kubwa ya tembo wameongezeka na hao tembo ni kwa sababu hawana mipaka wanaotembea kwenye mfumo wa ikolojia na kipindi hicho wamekuwa na tembo wengi ambao wamekuwa wakipita kwenye makazi ya watu.


“Hili linatokana na kwamba mara nyingi tembo eneo ambalo amepita miaka ya zamana anatabia ya kupita tena kilichoonekana kwenye kipindi cha kiangazi mapito ambayo yalikuwa ya tembo wanapita watu wamevamia na kuweka makazi hata madhara makubwa yametokea”Alisema.


Hata hivyo alisema kwamba changamoto kubwa ni watu wamelima karibu na hifadhi huku wakiwa hawajaacha hata mita moja na ndio changamoto inapelekea kuwa rahisi tembo kuingia kwenye hayo maeneo na mashamba na kufanya uharibifu mkubwa.


Kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa Uhifadhi katika Idara ya Utalii hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Benard Mgina amesema hali ya utalii wageni wamezidi kuongezeka kwa sababu ukiangalia takwimu 2009 hadi 2010 wageni 854 wametembela hifadhi wageni wa nje walikuwa ni 419 na wa ndani 435.


Aliema utaona kuna utofauti mkubwa sana vile vile ulkiangalia hesabu kutoka mwaka 2009 /2010 kwenda 2018 hadi 2019 kuna tofauri kwa sababu 2009 /2010 ilikuwa wageni 854 lakini 2018/2019 wamepokea wageni 2930.


Afisa Mwandamizi huyo wa Uhifadhi wa Idara ya Utalii alisema kwamba wageni ambao wamepokelewa kwa mwaka 2018/2019 kati yao wageni 728 kutoka nje na 2200 walikuwa wageni wa ndani kuna utofauti mkubwa sana.

SERIKALI KUTEKELEZA MRADI WA GESI ZA MAGARI

Na Hadija Hassan.


SERIKALI kupitia Shirika la maendeleo ya Gesi na Mafuta Tanzania (TPDC) linakusudia kutekeleza mradi mkubwa wa Compressive nature Gas (CNG) wa kuongeza vituo vya Gesi iliyoshindiliwa kwa ajili ya matumizi ya kwenye Magari.


Hayo yameelezwa na Meneja utafiti wa mafuta na Gesi wa Shirika la Maendeleo ya gesi na mafuta Tanzania (TPDC) Aristudes Katto alipokuwa akitoa maelezo kuhusu shughuli za Mkondo wa chini wa Gesi na usambazaji kwa wateja, kwa Waandishi wa habari waliotembelea katika kituo cha kupokelea Gesi Kinyerezi jijini Dar es salaam.


Katto alisema mradi huo wa Compressive nature gas (CNG) unatarajiwa kuanza mwaka huu wa fedha wa 2019/2020 ukiwa na lengo la kuongeza vituo vingi vya kutolea huduma pamoja na kuchochea matumizi ya Gesi kwenye Magari.


Alifafanua kuwa tangu nchi imeanza kutumia Gesi asilia mwaka 2004 mpaka sasa kiasi kilichotumika ni futi za ujazo Bilioni 497 huku asilimia 82% ya gesi inayozalishwa ikitumika katika kuzalishia umeme, 17% ikitumika viwandani na 0.02 ikitumika kwa upande wa taasisi, majumbani pamoja na kwenye magari.


Aidha Katto pia aliongeza kuwa utekelezwaji wa Mradi huo pia utahusisha Wamiliki wa vituo vya mafuta ambao watakuwa tayari kuunganishwa katika huduma hiyo ambavyo vitakuwa vikitumika kama vituo vya kujaza ama kubadilisha mitungi hiyo ya Gesi.


"kwenye Mradi huu kutakuwa na vituo mama kwa maeneo ambayo yatakuwa yamepitiwa na miundombinu ya bomba la gesi ambavyo vitatumika kusaidia kushindilia gesi, na baadae kusafirishwa kwenye vituo vidogo ambapo hakuna miundombinu  ya mabomba ya gesi na watumiaji watafika hapo na kubadilisha mitungi yao ya gesi" alisema Katto


"Kwa kuanzia mradi huu utaanza Jijini Dar es salaam kwa maeneo ambayo hayajafikiwa na miundombinu ya mabomba ya gesi ikiwemo Kigamboni, Mjini kati na pembezoni mwa Dar chalinze na kibaha ambako pia kumeonekana kuwa na wateja wengi wenye mahitaji wa huduma hii" aliongeza Ngowi.


Kwa upande wake Mubarak kituya Mkazi wa Temeke Jijini Dar es salaam aliipongeza Serikali kupitia TPDC kwa kufikiria kuanzisha mradi huo huku akieleza kwamba wamiliki wengi wa magari walikuwa wanasita kubadilisha mifumo ya kutumia mafuta na kutumia Gesi kwenye magari yao kwa kuhofia umbali wa kwenda kubadilishia gesi hiyo hivyo kupitia mradi huo wanachi wengi watahamasika kutumia gesi katika magari yao

KITUO CHA AFYA CHALINZE CHAZIDIWA NA WAGONJWA

 
Mkurugenzi wa shule ya Chalinze Modern Islamic, Omari Swed, akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Dkt. Sud Msakamali,kiroba cha sabuni ya unga, kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
........................................
Na Omary Mngindo.


Kituo cha afya Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, kinakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa majengo sanjali na msongamano wa wagonjwa.


Kituo hicho kilichoanza kama zahanati mwaka 1982 kabla ya kupandishwa hadhi mwaka 1996 kuwa kituo cha afya, majengo yake yamekuwa chakavu huku baadhi yake hayana linta hatua ambayo ni hatari kwa usalama.


Hayo yamebainishwa na Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Dkt. Sud Msakamali, akizungumza na Waandishi muda mfupi baada ya shule ya Chalinze Modern Islamic kufanya usafi pamoja na kukabidhi sabuni kwa uongozi wa Kituo.


Mbele ya Mkurugenzi wa shule ya Chalinze Modern Islamic, Omari Swed na Mbunge wa Jimbo hilo Ridhiwani Rikwete, Msakamali alisema kuwa kituo hicho kinapokea wagonjwa 300 kwa siku, huku kikizalisha watoto kati 130 mpaka 150 kwa mwezi.


"Kubwa la kwanza ni kuboreshwa miundombinu ya majengo, sababu wateja wanaokuja ni wengi, idadi ya majengo ni ndogo hivyo kusababisha foleni na msongamano, pia kutokwepo uzio ni changamoto kubwa watu wanapita muda wote," alisema Dkt. Msakamali.


Akizungumzia changamoto hiyo, Ridhiwani aliipongeza shule ya Chalinze Modern Islamic, kwa namna wanavyojitoa katika kufanikisha maendeleo, huku akishukuru msaada wa mifuko kumi ya saruji na karatasi za mitihani rimu 15 kwenye shule ya msingi ya Kibiki.


Aidha amewapongeza madaktari na watumishi wa Kituo hicho, huku akisema kuwa serikali imeshaanza kuzitafutia ufumbuzi, na kwamba TACAIDS imeshaanza ujenzi wa maabara itayojihusisha na upimaji wa vipimo vyote ikiwemo ya damu.


"Kama mnavyotambua, vipimo vya binadamu kwa magonjwa yote yanategemea upimaji wa damu, hilo limepewa kipaumbele, pia tunajenga chumba cha dharula kitakachosaidia wagonjwa watakaokuwa wanafika kwa ajili ya matibabu," alisema Ridhiwani.


Awali Mkurugenzi wa shule ya Chalinze Modern Islamic, Omari Swed akizungumza baada ya zoezi la usafi na kukabidhi sabuni za maji chupa 10, miche 15 ya sabuni ya kufulia na kiroba cha sabuni ya unga, alisema kuwa shule imejitoa kwa hali na mali kusaidia shighuli za kimaendeleo.


"Shule yetu ya Chalinze imekuwa mstari wa mbele kusaidia shughuli za kimaendeleo katika nyanja tofaiti, juzi tulikwenda shule ya msingi ya Kibiki tumesaidia mifuko kumi ya saruji na rimu 15 za karatasi kwa ajili ya mitihani," alisema Swed.

Monday, November 4, 2019

TAASISI ya Action for change (ACHA) kwa kushirikiana na The Right way (TRW) wamefanya uzinduzi rasmi programu endelevu ya uelimishaji jamii na uangalizi wa uchaguzi







TAASISI  ya Action for change  (ACHA) kwa kushirikiana na The Right way (TRW) wamefanya uzinduzi rasmi programu endelevu ya uelimishaji jamii na uangalizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika nchini Novemba 24 mwaka huu.

Programu hiyo imejenga taswira  kubwa ya kuona na wapiga kura wanapata elimu ya upigaji wa kura na uwepo wa mazingira rafiki kwa wazee na walemavu pamoja na kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru ,salama na haki  kwa vyama vyote vya kisiasa.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam, mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Action for change (ACHA) Bi Martina Kabisama alisema wao kama taasisi  za kiraia wanatekeza wajibu wa kusimamia uchaguzi huo kwa kufuata misingi maalumu ya kisheria iliyomo kwenye katiba ya nchi kwa kupatiwa kibali husika.

"Jamii inapaswa kujua haki zao za msingi katika kuwachagua viongozi bora wenye sifa na uwezo wa kuongoza wananchi hivyo ni fursa pekee ya wao kuelishwa umuhimu wa chaguzi hizi  sisi kama taasisi tutajikita katika kutoa elimu kwa wapiga kura na kusimamia zoezi la uhesabuji wa kura katika misingi ya haki," alisema Kabisama

Kabisama alisema kuwa programu hiyo ni endelevu yenye lengo la kuwafikia makundi mbalimbali ya wananchi waliopo mijini na vijijini ambao ndio wapiga kura wakuu katika chaguzi zijazo hivyo kuwapa elimu ni haki yao ya msingi.

Alisema sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa inawapa fursa makundi mbalimbali ya taasisi za kiraia kuungana kwa pamoja na serikali kwa kushirikiana na vyombo vingine kuweza kusimamia chaguzi , kutoa elimu na kuhakikisha demokrasia inatawala.

Alifafanua kwa kuvitaja baadhi ya vyombo watakavyo shirikiana navyo katika uendeshaji zoezi la uchaguzi  huo kuwa ni TAKUKURU, Tume ya uchaguzi, vyombo vya usalama ikiwemo jeshi la polisi pamoja na viongozi wa dini kuhakikisha amani na utulivu vinakuwepo.

Kwa upande wake Katibu wa The Right way (TRW) Gideon Mazara alisema kuwa mchalato wa utoaji elimu kwa jamii kupitia muungano huo utawashirisha vyombo mbalimbali vya habari ili kuhakikisha ujumbe kusudiwa unawafikia walengwa.

Alisema kuwa wao kama taasisi wamejipanga na kudhamilia kutembelea mikoa yote 24 ya Tanzania ili kuweza kuliendesha zoezi la hilo la mpiga kura ikiwemo utoaji elimu, uendeshaji sambamba na uangalizi wa uhesabuji wa kura.


Sunday, November 3, 2019

NECTA yaonya wadanganyifu wa mitihani, Kundi la kwanza elimu bure kufanya mitihani kesho




BARAZA la mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza kuanza kwa mitihani ya kidado cha nne kwa mwaka 2019 hapo kesho huku ikisisitiza kuwa wamechukua hatua zote muhimu kuhakikisha vitendo vya udanganyifu vinadhibitiwa.

Idadi ya wanafunzi ambao wamejiandikisha kufanya mtihani huo imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka na kwa mwaka huu jumla ya watahiniwa 585,866 wamesajiliwa kufanya mtihani huo. Kati yao watahiniwa wa shule ni 433,052 na watahiniwa wa kujitegemea ni 52,814

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt Charles Msonde amesema vitendo vya udanganyifu katika mitihani imeendelea kushuka mwaka hadi mwaka na mwaka huu wamejipanga kuvidhibiti.

Akitoa Takwimu ya kupungua kwa vitendo hivyo, Dkt Msonde alisema, toka Mwaka 2011 ambapo vitendo hivyo vilikuwa vikubwa na kupelekea kufuta matokeo, vitendo hivyo vilianza kushuka.

Alisema mwaka 2011, upande wa elimu ya msingi Barazalilirekodi vitendo vya udanganyifu 9,736 na baada ya hapo viliendelea kupungua mwaka hadi mwaka na ilipofika mwaka 2018 vitendo hivyo vilifikia 200+.

Kwa upande wa sekondari pia vitendo hivyo kwa mwaka 2011 baraza lilirekodi jumla ya vietendo vya udanganyifu 3303, idadi iliendelea kupungua hadi kufikia 200+ mwaka jana

“Napenda kuchukua nafasi hii kuzipongeza kamati zetu za mikoa, halmashauri kwa juhudi ambazo wanazichukua kukabiliana na udanganyifu wa mitihani, kwa kweli tumevipunguza sana na mwelekeo wetu ndio huo, kukabiliana na vitendo hivyo.” Alisema Dkt Msonde

Aidha Msonde aliongeza kuwa kufuatia mafanikio hayo, jumla ya Nchi 10 za SADC ziliweza kuja Tanzania kujifunza namna Taasisi hiyo ilivyoweza kukomesha udanganyifu.

Kuhusu watahiniwa wenye mahitaji maalum, Dkt Msonde alisema kwa mwaka huu kuna Jumla ya wanafunzi 842 ambao kati yao 450 ni wenye uoni hafifu, 42 wasion kabisa, 200 wwenye ulemavu wa kusikia na 150 wenye ulemavu wa viungo vya mwili.

Ametoa wito kwa kamati za mitihani za mikoa, halmashauri,Manispaa, Jiji kuhakikisha kuwa taratibu zote za mitihani ya Taifa zinazingatiwa ipasavyo, pia amewataka wasimamizi wote wa mitihani kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu.

Aidha watahiniwa wote wenye mahitaji maalum, wasimamizi wanatakiwa kulinda haki zao ikiwamo kuwapa mitihani yenye maandishi makubwa kwa wale wenye uono hafifu na mitihani yenye maandishi ya nukta nundu kwa watahiniwa wasioona.

Na wale wenye mahitaji maalum waongeze muda wa dakika 20 kwa kila saa kwa somo la hisababti na dakika 10 kwa kila saa kwa masomo mengine kama mwongozo wa baraza unavyoelekeza.

Hilo ni kundi la kwanza la wanafunzi wa kidato cha nne walionufaika na mpango wa elimu bila malipo

Kwa upande wake Waziri wa Tamisemi Suleiman Jaffo amesema hiyo ni hatua kubwa kwa serikali ambayo inatekeleza mpango huo ambao umesaidia kuongeza idadi ya wanafunzi walioendelea na sekondari.

Waziri Jafo amewataka watahiniwa kujiepusha na vitendo vya udanganyifu na kuhakikisha wanadumisha amani na utulivu wakati wote wa mitihani.

 “Hili ni jambo kubwa kwa kuwa hawa  ni watahiniwa wa kwanza walianza shule mwaka 2016 tuna kila sababu ya kumshukuru Rais Magufuli kwa utashi wake wa kisiasa na kuja na mpango huu.”

 “Niwaombe wanafunzi na wote wanaohusika katika usimamizi wa mitihani wajiepushe na vitendo vya udanganyifu, najua baraza la mitihani haliwezi kuvumilia na msije kulilaumu kwa kuonyesha makali yake,” amesema Jafo.

Ofisi 127 za serikali za mitaa sasa kupokea malipo kupitia Vodacom M-Pesa



WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo akizungumza na Waandishi wa habari katika zoezi la uzinduzi wa kampeni ya Malipo ya Serikali kupitia M-Pesa.


 WAZIRI Jafo akifafanua jambo
  • Zaidi ya wateja milioni 14 kunufaika na matumizi ya M-Pesa katika malipo ya halmashauri na manispaa kote nchini, hayo yamebainika leo Novemba 3, 2019. Dar es Salaam.
Na Selemani Magali

Wateja zaidi ya milioni 14 wa Vodacom watanufaika na huduma ya malipo kwa M-Pesa kwenda halmashauri na manispaa mbali mbali nchini. Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na ofisi ya TAMISEMI wamefanikisha kuimarisha mfumo wa malipo ya kifedha

kwa kusogeza huduma ya malipo kwa M-Pesa kwa ofisi zaidi ya 127 za serikali za mitaa nchini. Uzinduzi wa huduma hiyo, ulifanyika ofisi za Makao Makuu ya Vodacom, Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa

(TAMISEMI), Mheshimiwa. Suleiman Jaffo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mh Jaffo alisitiza umuhimu wa kutumia njia za kidigitali kama M-pesa kufanya malipo na kukusanya mapato kwani itaboresha uwekaji wa kumbukumbu, utoaji wa taarifa, kupunguza uvujaji na ubadhirifu wa pesa za umma pamoja na zkuongeza mapato kwa idara mbali mbali za Serikali ndogo.

“Malipo kutumia njia hizi za kidigitali yanapunguza muda mwingi tuliokuwa tunatumia kupanga foleni kufanya malipo. Sasa tuna M-Pesa naamini muda huu tukaupeleka moja kwa moja kwenye kujenga taifa na shughuli za maendeleo. Napenda kuwapongeza Vodacom kwa kutukumbuka na sisi huku TAMISEMI.

Ninatumaini kwamba huduma hii itawarahisishia malipo, si tu kwa wananchi bali hata nyinyi viongozi katika kutunza hesabu zenu,usalama wa fedha pamoja na ukusanyaji fedha kwa ujumla,” aliongeza Jaffo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa huduma ya M-Pesa, Bwana Epimack Mbeteni alisema kupitia M-Pesa, Vodacom inategemea kufikia taasisi nyingi za serikali na

binafsi ili kuwezesha mfumo wa malipo kuwa rahisi,fanisi na salama zaidi. “Asilimia kubwa ya

watanzania wanatumia M-Pesa kufanya miamala mbali mbali kama Luku, bili za maji, faini za barabarani, ndio maana tukaona fursa kubwa ya kurahisisha malipo kwa serikali za mitaa kutumia M-Pesa,” aliongeza Mbeteni.

Ushirikiano huu baina ya TAMISEMI na M-Pesa utawawezesha wateja wa mtandao wa Vodacom kufanya zaidi ya malipo 205 ya serikali za mitaa kwa urahisi na usalama zaidi.Malipo kama vile leseni za biashara, vibali vya ujenzi, malipo ya maegesho na nyinginezo.

“Wote tunashuhudia jinsi M-Pesa inavoendelea kubadilisha mfumo wa malipo nchini, ni tegemeo letu kwamba, malipo katika serikali za mitaa hizi yatakuwa rahisi na salama zadi.

Ili kulipa kupitia M-Pesa unapiga *150*00# anachagua lipa kwa M-Pesa, alafu malipo kwa serikali kisha anaweka namba ya kumbukumbu ambayo utapatiwa na ofisi za serikali za mtaa au unaweza kutumia APP ya M-Pesa kufanya malipo wakati wowote,” alifafanua Mbeteni.

Waziri Dkt. Kigwangala ahitimisha Tamasha la Urithi wetu



Mgeni Rasmi Waziri wa Mali asili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala akifurahia jambo wakati wa kufunga Tamasha la Urithi Wetu kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.

Mgeni Rasmi ambaye pia ni Waziri wa Mali asili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala (katikati) akimkabidhi Mwenyekiti wa kwaya ya Mt. Benedict kutoka Parokia ya Bugando jijini Mwanza Leonidas Kabagambi (aliyevaa shati jeupe) mfano wa ufunguo wa gari inayojulikana kama “Kirikuu”mara baada ya kuibuka washindi wakati wa kufunga Tamasha la Urithi Wetu kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.


Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi (wa pili kulia) akiruhusu mashindano ya mbio za baiskeli yaliyofanyika leo jijini Mwanza. wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mali Asili na Utalii Prof. Adolf Mkenda

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akitoa neno wakati wa kufunga Tamasha la Urithi Wetu leo jijini Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela (kushoto) akiteta jamboa na Waziri wa Mali asili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala (katikati)wakati wa kufunga Tamasha la Urithi Wetu leo jijini Mwanza. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe




Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Mwanza.

Serikali imewataka waandaaji wa Tamasha la Urithi Wetu kuwa wabunifu kwa kuongeza michezo mbalimbali ya jadi ambayo itasaidia kukuza kazi za sanaa na utamaduni wa Mtanzania ili kukuza fursa za utalii na kuwaongezea wananchi kipato.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mali Asili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala leo jijini Mwanza wakati wa kufunga Tamasha la Urithi Wetu kwa naiaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.

“Nimepita kila mabanda, wananchi wamepata fursa ya kutangaza kazi zao mbalimbali za kiuchumi zinazowasaidia kukuza kipato chao na uchumi wa taifa kwa ujumla. Rais Dkt. John Pombe Magufuli yupo mstari wa mbele katika kuinua na kusimamia utamaduni wetu” alisema Dkt. Hamis Kigwangala.

Dkt. Kigwangala amesisistiza kuwa Tanzania inafursa nyingi za kiutamaduni ambapo amebainisha kuwa ni nchi pekee barani Afrika inayojumuisha zaidi ya makabila 128 ambayo yapo kwenye makundi makuu manne ya makabila yanayopatikana Afrika yanayojulikana kama Wakushi, Khoisan, Wabantu na Waniloti.

Aidha, Dkt. Kigwangala alibainisha kuwa tamasha la urithi wetu lina lengo la kuendeleza falsafa ya nchi yetu ambayo Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kulinda utamaduni wa Mtanzania.

Ili kulifaya tamasha la urithi liwe endelevu, Dkt. Kigwangala amesema kuwa ni lazima wananchi wawe na furaha ambapo tamasha hilo linaongeza hamasa katika michezo, sanaa na utamaduni hatua itakayowapelekea wananchi wawe wabunifu, wenye furaha na wenye mawazo mazuri yanayowashirikisha wadau wote wa maendeleo ikiwemo sekta binafsi.

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa Watanzania wanahaki ya kumshukuru Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere ambapo mara baada ya kupata uhuru Desemba 9, 1961 alikuwa mstari wa mbele katika kusimamia utamaduni wa Mtanzania.

Akinukuu maneno ya Baba wa Taifa Mwl. Nyerere Waziri Dkt. Mwakyembe alisema “‘Taifa lisilo na utamaduni wake, ni taifa mfu.’ Watanzania tumeamka, tamasha hili linatukumbusha tujitambue sisi ni akina nani. Namshukuru Mungu tumejitambua ndio maana nawashukuru wana Mwanza, wizara zetu za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Mali Asili na Utalii kwa kurejesha na kusimamia tamasha hili linalotukumbusha sisi ni ni Watanzania, tujivunie Uafrika wetu.”

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amesisitiza kuwa Mwanza ndio kitovu cha nchi za maziwa makuu ambapo kuna mfanano wa mambo ya kijiografia yanayoifanya Mwanza kuwa katikati ya nchi za Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki. Hii ni sifa inayoifanya mkoa huo kuendelea kuwa mwenyeji wa tamasha la utithi wetu.

Jiografia hiyo inaipa mwanza nafasi kubwa zaidi ambayo itatoa fursa kwa nchi zote za Afrika mashariki kushiriki katika tamasha hili kwa ufanisi zaidi ambapo Mkuu huyo wa mkoa amewahakikishia washiriki wote ulinzi na usalama wakati wa tamashaha hilo mwakani 2020 ambalo litafanyikia tena jijini Mwanza.

Tamasha la Urithi wetu lilianza Oktoba 31 na kuhitimishwa Novemba 02 ambapo liliongozwa na kauli mbiu “Urithi wetu, Fahari yetu. Tamasha hilo lilpambwa na kushereheshwa kwa michezo mbalimbali ikiwemo ngoma za asili, kwaya, mbio za baiskeli, mbio za mitumbwi pamoja na mchezo wa bao.    


OSHA: tumetekeleza maagizo ya blue print kwa asilimia 100, sasa kuwafikia wateja walioko katika sekta isiyo rasmi hivi karibuni



 Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda, (katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja juu ya usalama na afya kwa wahariri na waandishi wa habari Dar es salaam. 
 Washiriki wa semina ya siku moja juu ya usalama na afya sehemu za kazi.

Na Mwandishi wetu, Dar es salaam

Imeelezwa kuwa usajili wa maeneo ya kazi unaofanywa OSHA,umeongezeka zaidi ya mara 6 toka utekelezaji wa Blue Print uanze, hayo yamesemwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda, wakati akifungua mafunzo  maalaumu ya usalama na Afya kwa waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam.

Mwenda amesema,OSHA imetekeleza maagizo ya Mhe. Rais kwa kuondoa urasimu katika utoaji wa huduma, ikiwemo kuondoa tozo na ada mbalimbali ambazo zilikuwa mzigo kwa wawekezaji nchini.

Kaimu Mtendaji huyo wa OSHA amesema tangu utekelezaji huo Blue Print uanze zaidi ya maaeneo ya kazi elfu kumi na sita yamesajiliwa na OSHA  mpaka kufikia Juni 2019 ukilinganisha na maeneo 3354 yaliyosajiliwa mwaka 2015/2016.

naye kwa upande wake washiriki wa mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yamewasaidia kujifunza mambo mengi ambayo walikuwa hawayafahamu, na hivyo yatawasaidia katika utendaji kazi wao wa kila siku.