Saturday, July 6, 2019

Hakikisheni mnaandaa bidhaa kwa ubora wa hali ya juu, acheni udanganyifu




MKURUNGEZI wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Edwin  Rutageluka amewaonya  wafanyabiashara wa viungo waache udanganyifu wanapotayarisha bidhaa ili viwe katika ubora unaofaa kuweza kupata soko mpaka nje ya nchi.

Akizungumza leo katika Maonesho ya 43 ya kimataifa na biashara Rutageluka amesma, baadhi ya  wafanyabiashara hasa wa kiungo cha pilipili manga wamekuwa na tabia ya  kuchanganya mbegu za mapapai ili kuzidisha ujazo katika kiungo hicho

Magogo ya kukatia nyama yanazalisha wadudu, atakayekutwa anatumia baada ya Septemba 30 kukiona







Ofisa Usajili wa bodi ya nyama nchini,  Sosthenes akifafanua jambo kww wananchi waliotembelea banda la bodi hii katika maonesho ya 43 ya sababa  yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini  Dar es Salaam.


Na Selemani Magali; Dar es salaam

Imeelezwa kuwa  mwisho wa kutumia magogo ya kukatia nyama ni Septemba 30, 2019, yeyote atakayekutwa anatumia baada ya tarehe hiyo kukiona.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Mtaalamu kutoka bodi ya Nyama Tanzania amesema hatua imekuja kwa sababu magogo hayo yanamadhara kiafya, ambayo yanatengeneza mazingira ya kuzaliana kwa wadudu  au vimelea vya magonjwa.

Aidha, amesema magogo hayo pia yanasababisha hasara ya upotevu wa nyama, kitaalamu katika kilo 100 inapotea kilo moja, ambapo kwa mwaka muuzaji anapoteza Sh milioni 3.8 ambayo inatosha kununua machine ya kisasa  ya kukatia nyama.

Ofisa msajili kutoka bodi hiyo Bw. Geofrey Sosthenes amesema hayo Julai 5, 2019 katika maonesho ya 43 ya sababa  yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini  Dar es Salaam.
Mtaalamu huyo amewataka wananchi hususani wanaoshughulika na uuzaji wa nyama kutembelea banda hilo ili waweze kupatiwa elimu.

Amesema watakao kaidi agizo hilo watachukuliwa hatua na Msajili wa bodi hiyo, kwa sababu tayari amekwisha ziandikia mamlaka za Serikali za Mitaa tangu  Februari, mwaka huu kwa maana ya wakurugenzi wa idara zote kuhakikisha wanaboresha maeneo yote yanayozalisha nyama ukiwa pamoja na machinjio, makalo na mabucha.

Ofisa huyo, ameongeza kuwa, hawapendi kuyatumia magogo kwa sababu yanamdhara kutokana na kwamba hayasafishiki, ukiwa unakata nyama baada ya mwezi yanakuwa ni mabaki ya muda mrefu na yanatengeneza vimelea vya magongwa ambavyo vinaweza kuleta madhara kwa walaji.

Aidha, amesema, utumiaji wa magogo pia husababisha hasara kwani mtu akitumia gogo, Kumbuka anatumia na shoka, kinachotokea nyama inagawanyika.

"Kama una bucha inauza kilo 200 kwa siku unaona ni kiasi gani unapoteza, ukipiga hesabu yako kwa mwaka unapoteza sh milioni 3.8 ambayo inatosha kununua mashine ya kisasa ya kukatia nyama, tunawasihi kuacha kuyatumia magogo kwa sababu si salama kwa afya za watumiaji," alisema Sosthens.

Tutahakikisha tunawashauri wamiliki wa mabucha kuhakikisha wanakuwa na mabucha ya viwango ambayo yapo kwenye sheria, viwango hivyo ni pamoja na kuacha kutumia magogo jambo ambalo tumeisha lisisitiza".

Ofisa huyo pia ametoa ombi kwa wadau wote wanaojishughulisha na mnyororo wa thamani wa nyama au anayefanya biashara hiyo au msafirishaji au mfugaji ahakikishe amesajiliwa na kumiliki cheti kutoka katika bodi hiyo.

Rais Magufuli Afurahishwa na Ujio wa Rais Kenyatta Nchini

Na: Frank Shija – MAELEZO, Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kuwa Rais wa kwanza wa nje kutembelea Wilaya ya Chato.

Amesema kuwa ukiachilia mbali ujirani uliopo baina ya Tanzania na Kenya, pia kuna undugu kwa kuwa tunazungumza lugha moja, tunamuingiliano wa kijamii ikiwemo kuoana na kuwa na utamaduni unaofanana.

“Kufika kwako umeudhihirishia umma wa dunia kuwa sisi ni majirani, na marafiki wa kweli siku zote tutatembea pamoja kamwe tusikubali kulaghaiwa na watu,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema kuwa kutokana na ushirikiano huo wafanyabiasha wa Kenya na Tanzania wamekuwa wakishirikiana katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kijamii ikiwemo kuwekeza katika nchi zetu.

Kwa ujibu wa takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Kenya imewekeza miradi 504 yenye thamani ya dola 1.7 biloni ikiwa na idadi ya watu 50,956 huku wawekezaji wa Tanzania nchini Kenya wakiwa wakekezaji 24.

Aidha katika Sekta ya Utalii, Tanzania ni nchi ya pili kwa watu wake kutembela nchini Kenya ikitanguliwa na nchi ya Marekani ambapo kwa mujibu ya takwimu za Bodi ya utalii ya Kenya ya Mwaka 2018 Watanzania 222,216 walitembelea Kenya ambayo ni zaidi ya 10% ya watu wote waliotembelea Kenya.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli ameitaja miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kwa ushirikiano wan chi hizi mbili ikiwemo barabara ya Holili- Arusha hadi Namanga pamoja na maandalizi ya ujenzi wa Barabara kutoka Mombasa hadi Bagamoyo.

Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania ipo katika hatua mbalimbali za kujenga meli tano ambapo itaanzisha safari za kutoka Bukoba – Mwanza – Kisumu na Jinja.

Vile vile Rais Dkt. Magufuli ametoa wito kwa wawekezaji kutoka Kenya kuja kuwekeza nchini hapa kwa kuwa milango ipo wazi kwa mwekezaji yeyote na Watanzania waendelee kuwekeza Kenya ili kuendeleza ushirikiano uliopo kwa mustakabari wa maendeleo ya nchi zote mbili.

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyata amesema anayofuraha kuwa Rais wa kwanza wa nje kukanyaga ardhi ya Chato.

Ameongeza kwamba uwepo wake Chato Mkoani Geita ni udhibitisho kuwa nchi hizi ni ndugu na wapo kwa ajili ya kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Kenya.

“Hakuna mtu anayeweza kututenganisha kamwe, sisi kama watu wa Afrika Mashariki yatupasa kuhakikisha tunaondoa vikwazo vyote vitakavyozuia kutembeleana, kufanyabiashara pamoja na pengine hata kuoana.” Alisema Kenyatta.

Apongeza Ujenzi Uwanja wa Ndege Chato
Rais Kenyatta ameipongeza Serikali kwa kujenga uwanja wa ndege wa Chato kwa kuwa ni utaimarisha na kukuza ukuaji wa biashara na shughuli nyingine za kimaendelea katika ukanda huo jambo ambalo halipaswi kubezwa.

Amesema anashangazwa na baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakipuuza jitihada hizo za kujenga uwanja huo kwani ni muhimu na yeye kama Rais wa Kenya angependa kuona Afrika ya Mashariki inakuwa kitu kimoja.

Amechukizwa na kauli za baadhi ya wanasiasa na kusema haiwezekani kumzuia Mtanzania kufanya biashara au kuoa nchini Kenya vivyo hivyo kwa Wakenya nchini Tanzania.

Rais Kenyatta yupo hapa nchini ikiwa ni ziara yake binafsi kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 05 Julai hadi siku ya kesho Jumamosi ya tarehe 06 Julai 2019.

LG electronics calls citizen to visit its pavilion to see washing machine that create smarter washing solutions





The LG electronics has made a call to Tanzanian who visit sabsaba trade fair to take their time to visit its pavilion and see good products that deliver ultimate convenience to consumer.
Also the company has introduced TWIN wash, styler and commercial washers that assures Tanzania home owners the latest smart washing solutions.

Speaking at sabasaba trade fair LG electronics country manager Tanzania Mr Keewook Song, said the company is re-positioning its expansive products portfolio as an integrated service that offers premium solutions for enhanced living.

The manager said, the TWIN wash washing machine employs the true steam feature penetrate fabrics with steam to eliminate 99.9% of household allergens as well as wrinkles and odors while softening and refreshing clothing.

He added, the machines comes with turbo wash to minimize washing time by using powerful jet spray and filtration to disperse concentrated detergent directly onto the clothes inside.

Furthermore, the TWIN wash significantly reduces washing time by allowing for two loads to be cleaned simultaneously –completing both wash cycles in just 49 minutes.

In addition to the powerful main front load washer and convenient mini washer, the washing machine comes with LG’s efficient echo-hybrid dryer function which provides consumers with the ultimate all –in-one solution as well as a washer/ dryer that meets their everyday laundry needs

According to Song said, the styler promises functionality and elegance to Tanzanian homes with its refined, modern design and ability to keep clothes hygienically clean and looking their very best. It features a sleek mirrored door that exudes sophistication and complements the interior décor.

He noted that the stylers’ core technology is its True steam technology, which eliminates over 99.9% of bacteria and germs found in the clothing to keep users’ wardrobes hygienically clean. With its rack moving system, styler shakes out wrinkles and unpleasant odors, while dampness is quickly and effectively removed by the gentle dry feature.

He elaborated that heat pump drying reduces energy consumption by recycling heat from the hot, moist air from the styler, and pants crease care ensures a neat, tidy look by eliminating wrinkles and creating a crisp crease-line, saving users from the time-consuming task of ironing

Also concern the LG’s commercial washers feature the inverter direct drive technology assuring the customers of its superior durability and liability who desire quiet and low vibration performance.

Commercial washers also comes with the minimal parts which means customers do not need to worry about repairs, the commercial dryers on the other hands incorporate a durable heavy-duty motor that results in better drying performance and increased drying capacity.

The stackable design for washers and dryers allows more customers and more machines in limited space, suitable for businesses of all size

LG’s electronic is also a part of other company that show case its products at sabasaba trade fair. It shows its pioneering products and innovative technologies that deliver ultimate convenience to consumers.

According to country manager, all products they display are energy star qualified to meet industries standards in energy efficiency and also in line with their global corporate sustainability strategy to reduce the environmental impact of a products development, production and circulation. The customers are guaranteed to save on electricity bills with their products.








CHAI BORA YAELEZA KILIMO CHA CHAI KILIVYO NA TIJA KWA WAKULIMA






Selemani Magali

Kampuni ya chai bora imeelezea kufurahishwa kwake na kushiriki maonyesho ya sabasaba, wakisema maonyesho hayo yamewasaidia kuwakutanisha na wakulima moja kwa moja kuwaeleza namna wanavyoweza kufanya kazi kwa pamoja.

Wakulima wadogowadogo walikuwa wanaogopa kampuni ya chai bora wakizani ni kwa ajili ya wakulima wakubwa, lakini kupitia maonyesho ya sabasaba wameweza kuondoa dhana hiyo potofu kwa wakulima.

Katika upande mwingine wakulima wa zao la Chai wametakiwa kuendelea kulima Chai kwa wingi katika kuhakikisha Soko lake linakuwa ndani na nje ya nchi.

Pia wametakiwa kulima aina mbali mbali ya Chai na kuacha mazoea ya kulima aina moja ya Chai nyeusi badala yake walime aina mbali mbali ikiwemo Chai ya maua.

Akizungumza Jana Jijini Dar as Salaam  maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ,Awatif Bushiri alisema kwa sasa wakulima wamekuwa wakilima aina moja ya Chai hali inayowafanya watu watengenezaji wa majani ya Chai kukosa kuweka aina nyingine ya Chai na kutumia aina moja ya Chai nyeusi.

"Wakati mwingine tunapata shida ya kutengeneza Chai aina nyingine Kutokana na wakulima wengi kulima Chai aina moja na wakati mwingine uwa tunaamua kuagiza nje ya nchi Chai za maua ambazo zinakuwa na harufu za matunda mbali mbali," alisema

Bushiri alisema zao la Chai linasoko kubwa ndani na nje ya nchi hivyo wakulima wakiongeza jitihada tutaweza kuzidisha kupiga hatua katika kufanya biashara na kujitangaza zaidi kwa nchi za nje.

"Sisi Chai Bora tumekuwa tukiuza bidhaa zetu hadi nje ya nchi na sasa tumefikia katika nchi tano ambazo tumekuwa tunauza Chai yetu,ikiwemo Ghana,Saudi Arabia,South Africa,Rwanda na Kenya ," alisema Bushiri

Kwa Mwaka huu Banda la Chai Bora limeshika nafasi ya kwanza katika kipengele cha Chakula,Dawa na Vinywaji katika maonyesho hayo.


Friday, July 5, 2019

WAFANYAKAZI WAOMBWA KUTEMBELEA BANDA WCF SABASABA ILI KUPATA ELIMU NA KUJUA HAKI ZA MFANYAKAZI NA MWAJIRI


Mkurugenzi wa Huduma na Tathimini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF),Dkt. Abdulsalaam Omar, akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam amesema mfanyakazi aliyeumia kutokana na kazi aifanyayo au maradhi yaliyosababishwa na kazi ifanyayo.
Mfuko utagharimia matibabu kwa ujumla baada ya kufanyiwa tathmini na madaktari ambao tayari wamepatiwa mafunzo ya namna ya kufanya tathmini kwa Mfanyakazi aliyeumia au kupata maradhi kutokana na kazi anayoifanya.
Naye Mkuu wa kitengo cha Mahusiano kwa Umma wa (WCF),Bi. Laura Kunenge, aliwahimiza waajiri na wafanyakazi kutembelea banda hilo ili kupata elimu lakini pia kujua haki za mfanyakazi na mwajiri.
“Mfulo huu unatoa nafuu sio tu unasaidia Mfanyakazi kulipwa Fidia Stahili bali pia unatoa nafuu kwa mwajiri kwani ghara hizo zitasimamiwa na WCF na sio Mwajiri. “Ndio maana tunawahizimiza waajiri kote nchini kutoka sekta binafsi na umma, kutoa michango ya kila mwezi kama sheria inavyotaka.”Amesema Bi. Laura.

 Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCD), Dkt. Abdulsalaam Omar,(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua ambazo mfanyakazi anapaswa kuchukua baada ya kupata maradhi au kuumia wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kabla ya kupatiwa Fidia na WCF katika  banda la mfuko huo  kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa leo Dar es Salaam 2019, barabara ya Kilwa.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
  Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano kwa Umma wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCD),Bi. Laura Kunenge akizungumza na waandishi wa habari ambapo amewaomba  wananchi wafike katika banda la mfuko huo ili kujua haki za mfanyakazi na mwajiri kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya barabara ya Kilwa Dar es Salaam 2019.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Sebera Fulgencealie (wapili kulia) akiwapatia maelezo waandishi wa habari (kushoto) kuhusu shughuli zifanywazo na WCF.

Watumishi wa WCF (kulia) wakiwahudumia mwananchi waliofika kwenye kwenye banda            hilo kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya barabara ya Kilwa Dar es Salaam2019.

VETA WAJA NA TAA ZA MANUAL KUMSAIDIA ASKARI BARABARANI






MAMLAKA ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), imebuni mfumo  maalumu kwa ajili ya kumsaidia trafiki kuongoza magari bila ya kusimama katikati ya barabara.

Hapa kama mnavyoona tunalo mfano wa daraja la juu na la chini, hizi taa mnazoziona sio za kawaida kama zile ambazo mmezizoea, hizi za kwetu askari anaweza kuziendesha anavyotaka, dhamira ni kumsaidia askari asigongwe lakini pia kuondoa msongamano wa magari.

Akizungumza katika maonesho ya 43 ya kimataifa ya biashara Mwalimu wa magari Makubwa kutoka Veta kihonda Morogoro Mwalimu Willium Emanuel Munuo amesema lengo la mfumo huo ni kumsaidia trafiki kuepuka kero mbalimbali asimamapo barabarani ikiwemo kugongwa na magari.

Mwalimu Munuo amesema tayari mfumo huo umeshapelekwa costech tayari kwa kusajilia ubunifu huu, tayari kwa mfumo huu kutumika.

Amesema wazo la kutengeneza mfumo huo liliwajia kutokana na kuona kero iliyokuwepo katika barabara na kuona matrafiki wamekuwa wakipata shida na kuatarisha maisha yao pindi wanapokuwa barabarani.

Amesema mfumo utamsaidia trafiki kufanya kazi bila ya kutumia nguvu wala kusimama katikati ya barabara hivyo kumpa urahisi zaidi wa kuangalia ni sehemu gani ambapo pamezidiwa na foleni na kuponyeza mfumo huo kisha taa zitawaka.

"Teknolojia hii bado haijaanza kufanya kazi tumepeleka wazo katika Ofisi husika ili waweze kuungalia kama unaweza kusaidia kupunguza adha ya foleni," amesema Swanga.

Ameongeza kuwa mfumo huo utafungwa pembeni ya barabara na kuunganishwa katika taa za barabarani ambapo trafiki atakuwa akibadilisha ni sehemu gani ambapo magari yameonekana kukaa kwa muda mrefu.

Aidha Mwalimu huyo amesema taa hizo zinatumia umeme wa kawaida na wajua. Taa hizo zinadaiwa kuwa suluhu ya kumsaidia askari wa barabarani.


KIJANA AMLAWITI MAMA YAKE MZAZI...TAYARI KADAKWA NA POLISI


Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Mazengo Chati kwa kumlawiti mama yake mzazi akiwa hajitambui, katika Kijiji cha Manchali wilayani Chamwino, jambo ambalo ni kinyume kwa mujibu wa sheria za Tanzania.

Kamanda Muroto ametoa taarifa hiyo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alieleza kijana Mazengo Chati mwenye umri wa miaka 28, amembaka mama yake mzazi mwenye miaka 56 na ametenda kosa hilo kwa madai ya ulevi pamoja na imani za kishirikina.

Kamanda Muroto amesema kuwa "tukio la kijana Mazengo limetokea katika Kijiji cha Manchali ambapo kijana huyo alimlawiti mama yake mzazi akiwa hajitambui, na kwa sasa tunamshikilia kwa ajili ya kumfikisha mahakamani"

Aidha Kamanda huyo amesema kuwa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia watu wengine wawili, kwa makosa ya ulawiti na ubakaji wa watoto na wazee huku mtuhumiwa mmoja akiuawa na wananchi wenye hasira kali, baada ya kukutwa akiwa anambaka mwanafunzi wa miaka nane.
Chanzo - EATV

TTCL Yavuna Wateja Wapya 215,000 Na Kuitikia Wito Wa Rais Magufuli

SHIRIKA la Mawasiliano Nchini (TTCL) katika kipindi cha siku 30 limeweza kusajili wateja wapya 215,000, ikiwa ni Mpango Mkakati wa Shirika hilo katika kujiinua kibiashara na kuongeza wigo huduma ya Mawasiliano kwa Watanzania ikiwa ni utekezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli.

Akizungumza Alhamisi (Julai 4, 2019) katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere, Meneja Mawasiliano wa TTCL Nicodemus Mushi alisema Shirika hilo limetekeleza kwa vitendo agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilolitoa kwa Shirika hilo tarehe 21 Mei, mwaka huu.

Mushi alisema hadi sasa huduma za Mawasiliano za Kampuni hiyo katika Mfumo wa 4G zinapatikana katika Mikoa 16 nchini na mpango uliopo ni kuhakikisha kuwa maeneo yaliyobaki yanapata huduma za Shirika kupitia  Mpango Mkakati wa Shirika hilo uliojiwekea na hivyo kuweza kuleta ushindani wa huduma ya mawasiliano na makampuni mengine nchini.

“Mwaka uliopita tulijiwekea Mpango Mkakati wetu ambao utahakikisha kuwa tunaweza kuleta ushindani na makampuni mengine na hivi sasa kama unavyoona tumeweza kupata wateja wapya 215,000 na kupitia maonesho hayo tutaweza kuongeza wateja wengi zaidi ” alisema Mushi.

Aliongeza kuwa kwa sasa Shirika hilo limeweza kupata wateja wengi zaidi wakiwemo watumishi wa serikali, ambapo kwa kutambua umuhimu huo, TTCL imeanzisha kifurushi maalum cha ‘watumishi pack’ ambacho kinaweza kutumiwa na wafanyakazi wote wa serikali kwa kuweza kukamilisha taratibu mbalimbali ikiwemo vitambulisho vya kazi.

Akifafanua zaidi Mushi, alisema kauli zinatolewa na watu mbalimbali kuhusu kauli ya Rais Dkt. John Magufuli kuwataka wafanyakazi wa serikali kutumia huduma za mawasiliano za shirika hilo, ni kuwa zitawahusu watumishi wa umma ambao wanalipiwa huduma za mawasiliano ya simu na serikali na si kinyume na maelekezo hayo.

Aliongeza kuwa malengo ya Taasisi hiyo ni kuweza kujipanga ili kuendelea kutoa huduma bora na zenye viwango ili kuweza kuongoza na kuwa kampuni bora ya mawasiliano inayotoa huduma bora kwa wateja wake nchini.

“Sisi kwa upande wetu tumeendelea kuwalipa vizuri mawakala wetu ikiwemo kutoa kamisheni nzuri kwao ili kuhakikisha kuwa huduma zetu zinazotolewa zinakuwa zinakidhi matakwa ya wateja na soko la mawasiliano kwa ujumla” alisema Mushi

Tume Ya Madini Yatoa Mafunzo Kwa Wachimbaji Wadogo 350

Selemani Magali, Ddaresalaam 

SERIKALI kupitia Tume ya Madini imetoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini 350 katika mikoa ya Arusha na Katavi yaliyolenga kuwajengea uwezo wa kutumia njia bora na za kisasa ili kuwawezesha kuachana na matumizi ya matumizi ya Zebaki yanayoathiri mazingira.

Akizungumza  Alhamisi (Julai 4, 2019) katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere , Mkaguzi wa Madini na Mazingira wa Tume hiyo, John  Mataro alisema Tume hiyo imekusudia kuhakikisha kuwa suala la uhifadhi na utunzaji wa mazingira linapewa na kila mchimbaji wa madini nchini.

Mataro alisema Ofisi hiyo imekuwa ikiotoa miongozo mbalimbali kupitia sheria zilizopo kwa ajili ya kuwaelimisha wachimbaji wadogo, na kampeni hiyo itakuwa endelevu ili kuhakikisha kuwa maeneo yote yanayotumiwa na wachimbaji madini hususani wachimbaji wadogo yanazingatia maelezo hayo ili kuweza kuwa na uchimbaji endelevu na salama.

“Malengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wachimbaji wetu wanaweza kupata kipato cha kutosha ili kuweza kujikwamua kiuchumi, na hili litafanyika kwa kuhakikisha kuwa tunajenga mazingira yenye usalama wa hali ya juu katkika maeneo yote ya uchimbaji yaliyopo nchini” alisema Mataro.

Aidha Mataro aliongeza kuwa Tume hiyo kwa kutambua mchango wa wachimbaji wadogo nchini imekuwa ikiwajengea uwezo wachimbaji hao kwa kujenga mazingira wezeshi ikiwemo kupata mikopo nafuu kupitia taasisi za kifedha ikiwemo Benki, hatua inayolenga kuwapa morali na uwezo wa kumiliki vifaa bora na vya kisasa kwa ajili ya uchimbaji wa madini.

Akifafanua zaidi Mataro alisema mara kwa mara Tume hiyo imekuwa ikifanya ziara katika migodi mbalimbali iliyopo nchini yenye lengo la kuwakumbusha wachimbaji wote hususani wachimbaji wadogo kuzingatia miongozo mbalimbali ikiwemo kuwepo matangazo mbalimbali ya tahadhari katika maeneo ya uchimbaji ili kuweza kutoa taarifa kwa wahusika wanaofika katika maeneo hayo kwa mara ya kwanza.