Monday, June 17, 2019

DKT. ABBASI AIPONGEZA PSSSF.

 Msemaji Mkuu wa serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbasi, (kushoto), akipeana mikono na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF bw. Abdul Njaidi.
 
Dkt. Abassi (kulia), akijadiliana jambo na Bi. Eunice Chiume, (katikati), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi ,mara baada ya mazungumzo yao.

 ............................................

MSEMAJI Mkuu wa serikali, Dkt. Hassan Abbasi ameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kuanza vizuri kutekeleza majukumu yake katika kipindi kifupi tangu kuunganishwa kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.


Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Jumamosi Juni 15, 2019 ofisini kwake jijini Dar es Salaam wakati alipotembelewa na Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, aliyefuatana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi.


Kwa takriban wiki nzima, Meneja huyo amekuwa kwenye ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii ili kujenga mahusiano ikiwa ni pamoja na kueleza malengo ya Mfuko huo ambao ni mpya baada ya serikali kuunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF, LAPF, PPF na GEPF kwa lengo la kuboresha utoaji huduma.


“Tunaposikia kuwa watu wameanza kupata mafao yao tena kwa wakati kwakweli ni jambo la faraja kwa serikali kwa hiyo mpeleke salamu zangu kwa watendaji wote, akiwemo mtendaji mkuu wa Mfuko, tunafarijika sana tunapoona kwamba yale malengo ya serikali kuu kuunganisha hii mifuko ili kutoa huduma bora yametimia.” Alisema.


Dkt, Abbasi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Malezeo, pia amempongeza Meneja huyo kwa uamuzi wa kuvitembelea vyombo vya habari kwa lengo la kuelimisha umma na kueleza shughuli za Mfuko kwani hii itasaidia wanachama kujua kinachoendelea kwenye Mfuko wao.



“Huu ni Mfuko mpya, yako maswali mengi yanayozua tashtiti na tashwishwi ambavyo kwa pamoja vinafanya kitu kinaitwa jakamoyo ambayo ni vile mtu anaumia moyoni kumbe anakuwa tu hana taarifa sahihi, hili nalo niwapongeze baada ya kukamilisha zile taratibu za ndani na kuhakikisha wale wastaafu wanapata kile kilicho chao sasa kazi kubwa ni kutoa elimu.” Amefafanua Dkt, Abassi


Aidha Dkt. Abbasi alitoa wito kwa wastaafu na wale wastaafu watarajiwa kutambua kuwa msingi wa pensheni ni kumuhudumia mfanyakazi anapokosa nguvu ya kufanya kazi, ama uzeeni au kutokana na kupata madhara mengine ambayo yatafanya akose nguvu ya kufanya kazi.


“Niwakumbushe watanzia kuwa tuweke pesa benki zile tunazohitaji kutumia leo, kesho au katika kipindi kifupi, lakini mafao ni kwa ajili ya kukusaidia katika maisha ya baadaye, si vema umetumikia nchi, jamii halafu baada ya kustaafu ukaishi maisha ya mashaka.” Aliasa.


Awali Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma wa PSSSF, Bi. Eunice Chiume alimweleza Dkt. Abassi kuwa amepata fursa ya kutembelea vyombo vya habari ili kujenga na kuendeleza mahusiano ikiwa ni pamoja na kuutambulisha Mfuko huo mpya kwa wadau wa sekta ya habari.


Alisema Mfuko ulianza kutekelez amajukumu yake Agosti 1, 2018 na ndani ya miezi 6 tangu Mfuko uanze kutekeleza majukumu hayo umeweza kulipa malimbikizo ya pensheni ya mkupuo na ile ya kila mwezi kiasi cha shilingi bilioni 880, lakini pia Mfuko unaendelea na zoezi la kuhakiki taarifa za wanachama (wastaafu) ambapo kati ya wastaafu 120,000, elfu 10,000 bado hawajahakikiwa.


“Kwa hiyo tumeeleza kuwa Mfuko umefungua ofisi nchi nzima bara na visiwani na kwa kila mstaafu ambaye bado hajahakiki taarifa zake afike kwenye ofisi ya PSSSF iliyo karibu naye ili atekeleze wajibu huo wa kisheria.” Alifafanua Bi. Chiume.


Msemaji Mkuu wa serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbasi, (kushoto), akipeana mikono na Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume baada ya mazungumzo yao ofisini kwa Dkt. Abassi jijini Dar es Salaam Bi. Chiume ambaye alikuwa katika ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii jijini Dar es Salaam, amehitimisha ziara hiyo kwa kufanya mazungumzo na Dkt. Abassi.

RAIS WA ZAMANI WA MISRI AFARIKI DUNIA.

Image may contain: 1 person, beard
Aliyekuwa rais wa Misri, Mohammed Morsi, ambae aliondolewa madarakani na jeshi mwaka 2013 amefariki dunia ghafla akiwa mahakamani.


Taarifa za kifo cha kiongozi huyo zimetangazwa na televisheni ya taifa hilo mara baada ya kifo hicho kutokea.


Mahakama nchini Misri ilibatilisha hukumu ya kifo mwaka 2016 dhidi ya rais huyo aliyepinduliwa.


Morsi alihukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na kutoroka kwa wafungwa wengi wakati wa mapinduzi ya mwaka 2011 nchini humo.


Alichaguliwa kuwa rais mwaka 2012 lakini akaondolewa katika mapinduzi ya kijeshi mwaka mmoja baadaye, kufuatia maandamano makubwa ya kupinga utawala wake.


Morsi alishahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mashtaka yanayohusu ugaidi.


Umauti umemkuta alipokuwa mahakamani akisikiliza mashtaka dhidi yake ya kujihusisha kijasusi na kundi la Hamas la nchini Palestina.


Kwa muda wote, Morsi na wafuasi wake wamekuwa wakishikilia msimamo kuwa mashtaka dhidi yake yamechochewa na uhasama wa kisiasa baina yake na uongozi uliopo kwa sasa.


Mtoto wa kiume wa Morsi, Abdullah hivi karibuni alilalamikia juu ya baba yake kunyimwa huduma muhimu za kiafya akiwa gerezani.


Aliliambia shirika la kimataifa la habari la AP mwezi Oktoba mwaka jana kuwa baba yake amekuwa akifungiwa muda mwingi kwenye selo ya peke yake na kunyimwa matibabu ya magonjwa yanayomsumbua ambayo ni shinikizo la damu na kisukari.

Sunday, June 16, 2019

WAKULIMA WA UFUTA LINDI WAONYWA.

Baadhi ya wakulima wa zao la Ufuta katika kijiji cha Namangale Halmashauri ya wilaya ya Lindi Mkoani Lindi wakishuhudia uendeshaji wa mnada wa zao hilo.
Mrajisi msaidizi wa Vyama vya Ushirika wa Mkoa Huo Robert Nsunza, akizungumza wakati wa mnada huo.
.................................
NA HADIJA HASSAN, LINDI.


SERIKALI mkoani Lindi imesema haitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa kiongozi yeyote wa Chama Cha Msingi (AMCOS) atakaehujumu Mfumo wa uuzwaji wa zao la ufuta kwa Njia ya Mnada kwa kuchanganya zao hilo pamoja na Mchanga.


Hayo yamesema na Mrajisi msaidizi wa Vyama vya Ushirika wa Mkoa Huo Robert Nsunza June 15, 2019 katika Mnada wa zao hilo uliofanyika Ghara la Chama cha Msingi Namangale AMCOS katika kijiji cha Namangale Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Mkoani humo.


Nsunza alisema ili wakulima waendelee kupata bei mzuri katika zao hilo ni muhimu kwa watendaji katika Vyama vya Ushirika kuwa makikini katika Ufuta wanaoupokea kutoka kwa wakulima unakuwa kwenye ubora unaotakiwa.


“Serikali haitakuwa tayari kuona mnunuzi anakutana na Ufuta ambao utakuwa umechanganywa na mchanga , ndio maana tunawaambia viongozi katika vyama vyao kabla ya kuupokea Ufuta kutoka kwa mkulima na kuuingiza katika ghala ni lazima ufuta huo waumwage chini wajilidhishe ndio waupime”


Alisema Nsunza “Hatutakuwa tayaari kuona mtu anafanya hujuma yoyote katika hili, endapo mnunuzi atatoa taarifa kwamba amekuta mchanga ama takataka zozote katika Ufuta alioununua, viongozi wote wa chama husika Serikali itawawajibisha” Aliongeza Nsunza.


Nae Makamu Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika Lindi Mwambao kinachowaunganisha wakulima wa Wilaya za Lindi, kilwa na Manispaa ya Lindi Mkoani Humo Rashid Masudi aliwataka viongozi wa vyama vya Msingi wa chama hicho kuhalakisha maandalizi ya hesabu mara baada ya kukamilika kwa minada ili wakulima waweze kulipwa fedha zao kwa wakati.


Kwa upande wake Tadei Mbwago Mwenyekiti wa Namangale AMCOS alisema suala la kuuweka ufuta katika hali ya usafi ni jukumu la pande zote kuanzia kwa wakulima na wapokeaji hiyo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza ni vyema wakulima hao wakahakikisha ufuta wao unakuwa safi kabla ya kupeleka katika maghara kwa ajili ya kuupima ikiwa ni pamoja na kuupeta ili kuondoa majani na takataka zingine.


Akizungumza kwa niaba ya wakulima wengine Nuru Kambanga Mkazi wa kijiji hicho cha Namangale alisema anaishukuru Serikali kwa mfumo waliouweka wa kuuza zao hilo kwa njia ya mnaa kwani imewafanya wauze zao hilo kwa bei mzuri ukilinganisha na misimu iliyopita.


Katika Mnada huo wa Pili wa Chama kikuu cha Ushilika Lindi Mwambao jumla ya Makampuni 14 yaliomba kununua Ufuta huo ambapo Kampuni 6 kati ya hizo ndio yalifanikiwa kununua zao hilo kwa bei ya Juu ya Tsh. 2953/= na bei ya Chini 2905 ambapo jumla ya Tani 3220 na kilo 235 ziliuzwa
  
Baadhi ya wakulima wa zao la Ufuta katika kijiji cha Namangale Halmashauri ya wilaya ya Lindi Mkoani Lindi wakishuhudia uendeshaji wa mnada wa zao hilo.
 

BODI YA KOROSHO YATAKA WAKULIMA KUJISAJILI KWENYE DAFTARI LA WAKULIMA.

NA HADIJA HASSAN, LINDI.

BODI ya Kaorosho Tanzania imewataka wakulima wa zao hilo kujitokeza kwa wingi kujisajili kwenye Dafutari la kudumu la wakulima ili kupata taarifa sahihi za wakulima wa zao hilo kwa lengo la kujua maeneo halisi ya wakulima pamoja na mahitaji yao.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Francis Alfred alipokuwa akitoa salamu za bodi hiyo katika uzinduzi wa mafunzo ya Matumizi ya Viuwatilifu yaliyofanyika katika kata ya Maumbika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani Humo.

Alfred alisema usajili huo utawasaidia wao kama serikali kufahamu maeneo halisi ya wakulima kuanzia anapoishi na eneo la shamba la mkulima ikiwa ni pamoja na kufahamu mahitaji ya pembejeo za wakulima katika eneo husika.

Alisema bodi ya korosho imeshasambaza wataalamu wa bodi hiyo kwenye wilaya zote Nchi mzima ambazo zinalima zao hilo ili waongeze nguvunya kwa wataalamu ambao wapo wilayani wanaohusika na ukusanyaji wa fomu hizo za usajili lengo likiwa ni kukamilisha usajili huo ifukapo june 20 mwaka huu wa 2019.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Huo Godfrey Zambi alisema kuwa usajili huo licha ya kumtambua mkulima lakini pia Mkulima huyo ataweza kupatiwa kitambulisho kitakachomuwezesha kupata mkopo katika taasisi mbali mbali za kifedha.

Alisema jambo la usajili kwa wakulima ni muhimu kufanyika Kwani itawasaidia Serikali kuondokana na adha ya kuhakiki wakulima hao Mara baada ya kupeleka mazao hayo kwenye maghara kwa ajili ya mauzo pamoja na kutambua mahitaji halisi ya pembejeo za wakulima wa zao hilo na mahitaji Mengine Kama vile Miche na mbegu za mikorosho.

Ndemanga aliongeza Kuwa usajili huo pia utaisaidia Serikali kuzuia mianya ya wafanya biashara wanaowanyonya wakulima wanaonunua zao hilo kwa njia ya choma choma (kangomba).

Hata hivyo Ndemanga alitumia nafasi hiyo kukanusha juu ya uvumi unaoenezwa na baadhi ya wananchi kuhusisha usajili huo na utozwaji wa kodi kwa wakulima kuwa sio kweli, na kubainisha kuwa lengo lengo la usajili huo ni kupata taarifa za wakulima zilizo sahihi ili Serikali ijue namna ya kuwasaidia na kuwapa huduma