Wednesday, March 27, 2019

VETA KUANZA KUTUMIA KISWAHILI KUFUNDISHIA

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, sayansi na teknologia Dokta Avemaria Semakufu amevitaka vyuo vya  ufundi stadi  kupunguza vigezo vya udahili wa wanafunzi  kujiunga katika vyuo hivyo ili kuwawezesha wahitimu wa darasa la saba kupata elimu na mafunzo ya ujuzi mbalimbali.


Dokta Semakafu  ametoa wito huo wakati wa warsha ya makabidhiano ya mitaala na mihtasari ya m mafunzo ya elimu ya ufundi stadi iliyotafsiriwa kwa Lugha ya Kiswahili ambapo amesema  vijana wengi wapo mitaani  na wanapenda kujiunga na vyuo vya ufundi (VETA)lakini  wanashindwa kutokana na masharti  kuwa magumu.


Aidha   Naibu katibu mkuu huyo amesema  kuwa kupatikana kwa mitaala ya Kiswahili katika vyuo vya ufundi kutasaidia kuongeza kasi ya nchi kwenda uchumi wa viwanda pamoja na uchumi wa kati  huku mkuu Mkurugenzi Mkuu vyuo vyamafunzo na  ufundi stadi (VETA) Dokta Pancras Bujulu  akabainisha mabadiliko ya mitaala  itakavyosaidia  katika ongezeko la udahili wanafunzi pamoja na  wataalamu nchi.


Kwa  upande wake  Dokta Annastella Sigwejo Kutoka Baraza la Taifa Elimu ya Ufundi  akabainisha lengo la mabadiliko ya mitaala hiyo kuwa ni kwasaidia watanzania ambao hawajabahatika kufika elimu ya sekondari huku mkufunzi wa chuo cha maendeleo ya wananachi  Msingisi Cha mkoani Singida  Bw. John Well Well ameishukuru serikali kufanya mabadiliko hayo kwani itawasaidia katika ufundishaji.


Warsha hiyo imehusisha wakufunzi kutoka vyuo vya maendeleo wananchi na wakuu wa vyuo vya ufundi Stadi .

KIKWETE AMALIZA CHANGAMOTO YA MAJI KWA WALIMU NA WANAFUNZI WA MBOGA SEKONDARI.

Mbunge wa chaline Ridhiwani Kikwete akikagua mradi wa kisima kirefi alioujenga kwa pesa yake katika shule ya sekondari mboga ili kuwaondolea changamoto ya maji walimu na wanafuni wa shule hiyo.
 ...................................
Na Shushu Joel,Chalinze.


MBUNGE  wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete amefanikiwa kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama iliyokuwa ikiwakabili walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Mboga iliyodumu takribani kwa kipindi cha miaka zaidi ya 10 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo.


Akizungumza mara baada ya kukagua na kujiridhisha kwa ujenzi wa mradi huo wa maji ya kisima kirefu kwa ajili ya walimu na wanafunzi wa shule hiyo, mbunge huyo alisema kuwa Jimbo la chalinze kwa ujumla linachangamoto kubwa ya maji lakini juhudi za uchimbaji wa visima virefu kwa ajili ya taasisi kama shule na za afya zinafanyika ili kutokomeza uhaba huo kwenye maeneo hayo.


“Maji ni uhai kwani kila kiumbe hai kilichopo   hapa duniani kinahitaji maji safi na salama ili kiweze kuishi hivyo ni jukumu langu kama kiongozi kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana kwa asilimia kubwa katika jimbo la chalinze”Alisema Kikwete.


Aliongeza kuwa ni kipindi kirefu walimu na wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya ukosekanaji wa maji lakini kwa kuanzia tumeanza na upatikanaji huo wa kisima kirefu ili pampu zitakuwa zinasambaza maji kwenye pointi zilizotengwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali shuleni hapo.


Pia amemtaka mkuu wa shule hiyo kuhakikisha miundombinu ya maji hayo yanalindwa ili kisima hicho kiweze kudumu kwa muda mrefu na si kukiharibu kwa makusudi ili mbunge aweze kutoa hela ya kukarabati.


Aidha Ridhiwani Alisema kuwa huduma hiyo ya upatikanaji wa maji si tu kwa ajili ya walimu na wanafunzi wa shule ya mboga bali itakuwa ni mkombozi wa upatikanaji wa huduma hiyo ya maji katika eneo hilo hivyo wananchi nao wanapaswa kupata nafasi ya uchotaji wa maji  kijijini humo kwa  ajili ya matumizi ya nyumbani.


Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo ya Mboga sekondari Lunge Mwalaba amempongeza mbunge Kikwete kwa juhudi zake anazozifanya katika jimbo la chalinze kwa ujumla katika shughuli za ukamilishaji wa maendeleo kwa wananchi,kwani kilio cha upatikanaji wa maji katika jimbo la chalimze  ni mkubwa lakini shule yetu ya mboga imekuwa ni kipaumbele sana kutokana na mazingira.


Aliongeza kuwa kutatuliwa kwa changamoto ya maji kutapelekea juongezeka kwa ufaulu kwa wanafunzi kwani maji yalikuwa yakiumiza vifwa vya watumishi wa shule kutokana na kuwatuma wanafunzi kwenda sehemu mbalimbali kutafuta maji ili waweze kupata huduma ya chakula,hivyo maji hayo yatarahisisha shughuli za usimamizi na uendeshaji wa shule pia ogezeko la ufanisi wa ufundishaji kwa walimu kutokana  na kipindi cha nyuma walimu walikuwa wakiwazia maji kwa ajili ya matumizi ya familia zao.


Aidha amemhakikishia mbunge huyo kuwa hakuna yeyote Yule atakayehalibu miundombinu ya maji hayo kwani si muda mrefu walikuwa wakilia kwa tatizo la kukosa maji hivyo kila mtu katika eneo hili ni mlinzi wa mwenzake katika mradi huu.


Naye Mjumbe wa kamati ya bodi ya shule Muhamed Mzimba amempongeza mbunge huyo kwa kufanikisha lengo lake la kuhakikisha taasisi za serikali zote katika jimbo la chalinze zinakuwa na visima virefu kwa kusudi la kutatua changamoto za maji,taasisi hizo ni pamoja na mashuleni,vituo vya afya na sehemu mbalimbali zenye kutoa huduma za kijamii zinapata visima vya maji.

 
Aliongeza kuwa uwepo wa kisima hicho katika shule hiyo kutafanikisha mambo mengi ya shule kuweza kusonga mbele kutokana na upatikanaji wake.


Kwa upande wake mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo Juma  Ally amempongeza mbunge wa chalinze kwa   kuichaingia shule yao  misaada  mbalimbali  katika  harakati zake za kuisaidia shule yao

MMOJA AFARIKI RUVU KATIKA MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI.

NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

MZEE mmoja aliyetambulika kwa jina la Visu Urembo (80),amefariki dunia baada ya kuchomwa mkuki kwenye sehemu ya ubavuni mwa mwili wake, katika mgogoro wa wakulima na wafugaji, uliotokea Lukenge, tarafa ya Ruvu, Kibaha Vijijini, mkoani Pwani.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP, Wankyo Nyigesa alisema tukio limetokea majira ya saa 12 alasiri, march 26 mwaka huu.


Alieleza, mzee Urembo kabla ya kufikwa na umauti alikimbizwa kituo cha afya Mlandizi, ambapo baadae alikimbizwa hospital ya Tumbi kwa matibabu zaidi lakini kabla ya kupatiwa matibabu madaktari waligundua kuwa umati umeshamfika.


Hata hivyo, Wankyo alibainisha, wafugaji hao waliingiza mifugo yao (ng’ombe) kwenye bwawa linalotumika katika shughuli za binadamu ikiwemo kunywa, kufulia, kupikia na kadhalika.


“Kwa kuona hivyo ndipo wakulima wakaenda kwa mhemko kuwazuia watoe ng ‘ombe wao lakini wafugaji walianzisha tafrani, ambapo walianza kurusha mikuki ,vitu vyenye ncha kali na kusababisha kifo cha mzee huyo na kujeruhi watu watatu “alifafanua Wankyo.


“Polisi tulifika eneo la tukio alfajir March 27 ,na kutuliza tafrani hiyo na sasa hali ni shwarii”.


Wankyo aliwataja waliojeruhiwa ,kuwa ni pamoja na John Kisukari Urembo (50) ambae ni mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Lukenge.


Wengine ni mtendaji wa kijiji cha Lukenge Maximillian Evarist (34) na Adam Onesha ambae ni mwenyekiti wa kamati ya maji kijijini hapo .


Kamanda huyo alitoa wito, jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi ili kuepukana na madhara kama hayo yaliyojitokeza.


Wankyo,alisema kila mtu katika nchi hii ana haki ya kuishi, kutumia ardhi hii, na hakuna mwenye mamlaka juu ya mwenzie ila inabidi kuacha kuingiliana mipaka iliyotengwa kwa ajili ya kundi jingine ili hali kukabiliana na migogoro hasa ya wakulima na wafugaji”alisisitiza Wankyo. 


Mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama aliyataka makundi hayo yaheshimiane na kujenga upendo badala ya kujiona kundi moja ni zaidi ya kundi jingine.

MWAKYEMBE AISHAURI NMB KUONGEZA VIWANGO VYA MIKOPO.

 Waziri wa Habari utamaduni sanaa na Michezo Dkt Halison Mwakyembe, (kulia) akimsikiliza Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya kusini, Janeth Shango (kulia)alipotembelea katika banda la maonyesho la Benk hiyo katika kongamano la  jukwaa la fursa za Biashara na uwekezaji za Mkoa wa  Lindi lililofanyika Manispaa ya Lindi Mkoani Humo 
.............................................. 

NA HADIJA HASSAN, LINDI

Waziri wa Habari utamaduni sanaa na Michezo Dkt Halison Mwakyembe ameishauri Benki ya National Microfinance Bank (NMB) Kuongeza kiwango cha mikopo wanayoitoa  ili kuwapa fursa Wananchi wengi kukopa


Waziri Mwakyembe ameyasema hayo jana alipotembelea katika banda la maonyesho la Benk hiyo katika kongamano la  jukwaa la fursa za Biashara na uwekezaji za Mkoa wa  Lindi lililofanyika Manispaa ya Lindi Mkoani Humo 


Mwakyembe alisema pamoja na Bank hiyo kujikita katika kutoa Mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali, wafanya biashara  na wakulima ni vyema wakaona umuhimu wa kuongeza kiwango cha fedha wanazozitoa kwa wafanya biashara hasa katika Mkoa wa Lindi ili uwekezaji uweze kuleta tija


"Baada ya jukwaa hili tengeni fedha za kutosha zaidi kwani baada ya jukwaa hili la fursa za Biashara kufunguliwa bira shaka wafanya biashara watapenda kukopa ili waweze kuwekeza" alisema Waziri Mwakyembe


Awali akitoa maelezo mbele ya Waziri wa Habari utamaduni sanaa na Michezo Dkt Halison Mwakyembe afisa mahusiano wa Banki hiyo Janeth Shango Alisema kuwa wao kama Benki ya NMB kwa kuzingatia fursa zilizopo Nchini wanaungana na Serikali kuhakikisha wanasaidiana katika kuhakikisha Wakulima wote wanafikia fursa wanazoziona katika mikoa yao


Alisema katika kukamilisha adhima hiyo kwa kipindi cha miaka mitano2015/2020 Bank yao  imetenga kiasi cha sh.Bilioni 500 kwa ajili ya kuwakopesha wakulima kote Nchini ambapo mpaka sasa tayari sh. Bilioni 450 zimeshatolewa kwa wakulima moja moja na kwa vikumdi


Aidha alisema kuwa pamoja na kutoa Mikopo hiyo kwa wakulima wadogo, wakubwa na wakati lakini pia Mikopo hiyo inatolewa kwa wafanya biashara wanaohusika na usafirishaji wa mazao hiyo ni kwa kuwa wametambua kuwa kilimo ndio uti wa mgongo kwa Nchi