Tuesday, December 11, 2018

MAGAZETI YA LEO DESEMBA 11, 2018.

RUVU DARAJANI WALILIA MAZAO YAO

Baadhi ya wakulima katika bonde la Ruvu, kijiji cha Ruvu Darajani kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wakionesha miche ya mipapai iliyokatwa katwa katika mashamba yao, PICHA NA OMARY MNGINDO.
...........................................................


Na Omary Mngindo, Ruvu

WAKULIMA katika Kijiji cha Ruvu Darajani, Kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wameiomba Serikali kuingilia kati vitendo vinavyofanywa na watu wanaojiita wanatoka ofisi inayosimamia bonde la Ruvu wilayani humo, kwa kufyeka mazao waliyoyapanda. 

Wakizungumza na waandishi wa habari katika mashamba yao, wakazi wakijitambilisha kwa majina ya Ally Jeki,  Zaynabu Kikande  Shayo, Ally Jeki na Said Swaiba, walisema kuwa mwishoni mwa wiki wamevamiwa na watu hao waliokatakata mazao kwenye mashamba yao. 

Swaiba alisema kuwa siku ya tukio watu hao walipofika waliwachuku vijana wakaelekea nao kwenye mashamba hayo, kisha kuanza zoezi la kukata mazao pasipokushirikisha viongozi wa Kijiji, kitendo walichokieleza ni cha uonevu, huku wakiomba serikali ikemee jambo hilo. 

"Tunalima bustani nje ya mita 60 wanaodai ni mali yao, lakini cha kusikitisha hivi karibuni wamekuja kuivamia, wamekata mazao yetu ambayo wengi wetu tunayategemea kuendesha familia zetu, wengine tunasomesha kupitia kilimo hiki," alisema Swaiba.

Nae Samir Shayo alilalamika mipapainyake kukatwa baa watu hao ambao walipofika waliambatana na askari waliokuwa na silaha za moto,  kitendo kilichowaogopesha wananchi hao. 

"Kama mnavyoona, shamba langu lipo mbali na mita za 60 lakini hata kama wamechukua mita 100 bado wsingefika hapa, lakini wameamua kutufanya kitendo kibayabsana,  tunaomba serikali ikemee vitendo hivi vya kibabe," alisema Samir. 

Kwa upande wake Mjumbe wa serikali ya Kijiji cha Ruvu Ramadhani Natamani alisema kwamba mwezi wa nne mwaka huu walifika ofisini kwao wakawaeleza wanataka kuweka mipaka ya kuonesha mwisho wa kulimwa, lakini hawakuonekana tena 

"Cha kusikitisha Mtendaji wa Kijiji alipotaka kuwasogelea wajue kinachoendelea, aliambiwa asiwasogelee eneo walilokuwa wanakata mazao ya wakulima,  tunaomba uongozi wa Mkoa uingiliekati suala hili, " alisema Mnyamani.
 
Sehemu ya miche ya mipapai iliyokatwa katwa katika mashamba ya wakulima wa bonde la Ruvu kijiji cha Ruvu Darajani kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, PICHA NA OMARY MNGINDO.

TIMU YA MICHEZO YA BUNGE MSHINDI WA JUMLA WA MEDALI KATIKA MICHEZO YA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YALIYOFANYIKA BUJUMBURA NCHINI BURUNDI

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akipokea cheti cha ushiriki wa michezo ya Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka kwa Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson ambae ni kiongozi wa msafara wa wanamichezo wa timu ya michezo ya Bunge katika michezo ya Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Bujumbura, Burundi katika tukio lililofanyika tarehe 10 Desemba, 2018 katika uwanja wa ndege Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto) akimpongeza Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mjini Dodoma akitokea Bujumbura, Burundi katika michezo ya Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Naibu Spika aliongoza msafara wa timu ya michezo ya Bunge. Kushoto ni katibu wa Bunge, Mhe. Stephen kagaigai.
Wanamichezo wa timu ya michezo ya Bunge wakipokelewa na uongozi wa Bunge, watumishi wa Bunge wakiongozwa na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai walipowasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma wakitokea katika michezo ya Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Bujumbura, Burundi.
 
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (mwenye koti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na wanamichezo wa timu ya michezo ya Bunge walioongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (mwenye tisheti nyeusi) baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mjini Dodoma wakitokea Bujumbura, Burundi katika michezo ya Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (katikati) akizungumza na wanamichezo wa timu ya michezo ya Bunge na watumishi wa Ofisi ya Bunge leo tarehe 10 Desemba, 2018 katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, wakati timu hiyo ilipowasili kutoka Bujumbura, Burundi katika michezo ya Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ikiwa ni kuwaeleza kwa ufupi mafanikio waliyoyapata katika mashindano hayo na ushirikiano ulioonyeshwa na watumishi wa ofisi ya Bunge kabla na baada ya mashindano

RAIS DKT. MAGUFULI AGAWA VITAMBULISHO 670,000 KWA WAKUU WA MIKOA KWA AJILI YA MATUMIZI YA WAJASIRIAMALI WADOGO WADOGO (MACHINGA) KATIKA MIKOA YOTE YA TANZANIA BARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wakati Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila alipokuwa akisaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo machinga kwa ajili ya mkoa wa Mbeya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wakati Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alipokuwa akisaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo machinga kwa ajili ya mkoa huo wa Kiliamnjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wakati mkuu wa mkoa wa Njombe Cristopher Ole Sendeka alipokuwa akisaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo machinga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wakati mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka alipokuwa akisaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo machinga .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwandri kabla ya kusaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo machinga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wakati mkuu wa mkoa wa Tabora Agrey Mwandri alipokuwa akisaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizingumza na Wakuu wa Mikoa, Mawaziri na Makatibu Wakuu wa baadhi ya Wizara, Mameneja wa Mikoa wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA, Wawakilishi wa Machinga kabla ya kutoa Vitambulisho kwa ajili ya Wafanyabiashara wadogo wadogo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Vitambulisho hivyo vitagharimu kiasi cha Shilingi 20,000/ kwa kila kimoja. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizingumza na Wakuu wa Mikoa, Mawaziri na Makatibu Wakuu wa baadhi ya Wizara, Mameneja wa Mikoa wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA, Wawakilishi wa Machinga kabla ya kutoa Vitambulisho kwa ajili ya Wafanyabiashara wadogo wadogo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Vitambulisho hivyo vitagharimu kiasi cha Shilingi 20,000/ kwa kila kimoja.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyokuwa akiitoa katika ukumbi wa katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Meneja wa Mamlaka ya Mapato TRA kwa mkoa wa Kilimanjaro Msafiri Mbibo ambaye alikataa rushwa ya Dola za kimarekani $2000. Rais Dkt. Magufuli ameagiza kuandikiwa barua ya kupongezwa kwa Meneja huyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Ardhi Wiliam Lukuvi wakati akiondoka kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono wakati akiondoka kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, PICHA NA IKULU.

NAIBU WAZIRI ATEMBELEA ENEO LITAKALOTUMIWA KUBANGUA KOROSHO YA SERIKALI

 Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya, akiwaonyesha mtambo maalum wa kuchemsha korosho wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele. Wataalam hao wametembelea eneo la SIDO kujiridhisha kama linafaa kwa ajili ya kuanza kubangua korosho iliyonunuliwa na serikali.
 Kaimu Meneja wa SIDO mkoa wa Mtwara, Zamla Dongwala, akimuonyesha mashine ya kukausha korosho Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji (hayupo pichani) wakati alipotembelea eneo la SIDO, mkoani Mtwara leo. Eneo hilo ni moja ya maeneo yaliyochaguliwa kuanza kutumiwa wa wabanguaji wa korosho wadogo kubangua korosho zilizonunuliwa na serikali.
 
Fundi umeme akiwa kwenye hatua za mwisho kukamilisha matengenezo ya mashine ya kuchambua korosho kama alivyokutwa na mpiga picha wetu eneo la SIDO mjini Mtwara  (Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)

RAIS DKT. MAGUFULI ATOA VITAMBULISHO KWA WAJASIRIAMALI NCHI NZIMA

Na. Immaculate  Makilika – MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amegawa vitambulisho kwa wajasiriamali nchi nzima wenye mitaji isiyozidi shilingi milioni nne kwa lengo la kuwasaidia kufanya biashara zao kwa uhakika sambamba na kutambulika katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam, katika  kikao kazi na viongozi wa TRA, Rais Magufuli aligawa jumla ya vitambulisho 25,000 kwa kila Mkuu wa Mkoa, na kusema kuwa vitambulisho hivyo vimelengwa kutolewa kwa wajasiriamali wote nchi nzima wenye mitaji isiyozidi shilingi milioni nne ili viwasaidie kufanya shughuli zao mahali popote nchini, ikiwa ni pamoja na kutambulika TRA.

Ambapo Rais Magufuli alisema kuwa vitambulisho hivyo vinagawiwa bure, isipokuwa  kila mjasiriamali atatozwa gharama ya shilingi 20,000/= ikiwa ni sehemu ya gharama ya uandaaji wa kitambulisho husika.

“Kitambulisho hiki nimetoa mimi bure, sioni kama kuna mtu atakayekuja kuwasumbua, na kila Mkuu wa Mkoa atapata vitambulisho 25,000, ambapo atashirikiana na Wakuu wa wilaya ili kugawa vitambulisho hivyo kwa wajasiriamali walioko katika mkoa wake”

Halikadhalika, Rais Magufuli aliwataka wajasiriamali hao kuwa waaminifu, na kutokubali kufanya biashara za wafanyabiashara wakubwa wenye mitaji yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne.

Sambamba na hilo, Rais Magufuli alisisitiza watanzania kulipa kodi kwa kuwa kodi ndio msingi wa maendeleo kwa taifa lolote lile duniani, huku akiwataka TRA kupunguza viwango vikubwa vya kodi ambavyo wananchi wamekuwa wakivilalamikia.

Kwa upande wake, Gavana wa Benki Kuu, Profesa Florence Luoga alisema kuwa Benki hiyo imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ikiwemo kudhibiti matumizi haramu ya fedha,  kuhakikisha kuwa thamani ya fedha haiyumbi na kudhibiti matumizi ya dola kwa kufungia maduka ya kubadilishia fedha ambayo hayakuwa na leseni.

Profesa Luoga alisema  kuwa BOT iligunduwa kuwepo kwa maduka ya kubadilishia fedha 1,000 badala ya maduka 300 yaliyokuwepo awali na ambayo hayakuwa na leseni.

“Tunajadiliana na Waziri wa Fedha ili kuwezesha wananchi au wafanyabiashara kulipia bidhaa  kwa kutumia benki” alisema Profesa Luoga

Profesa Luoga  aliongeza kuwa kwa sasa hivi hali ya fedha ni nzuri na hivyo Serikali ina fedha za kutosha kufanya matumizi mbalimbali kwa kipindi cha miezi mitano ijayo na kuwataka wananchi wasiwe na hofu.

Aidha, aliongeza kuwa kabla ya mwezi Desemba kuisha , BOT itakuwa imeshatengeneza kanuni za kuwalinda watumiaji wa mabenki.

Naye, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Charles Kichere, alisema kuwa katika kipindi cha miaka ya Serikali ya Awamu ya Tano, TRA imefanikiwa kukusanya mapato ya jumla ya shilingi trilioni 42.9
Ambapo, katika kipindi cha robo mwaka wa fedha 2018/2019, Serikali kupitia TRA imekusanya kodi jumla ya shilingi trilioni 3.8.

Aidha, Kichere alisema kuwa licha ya changamoto mbalimbali zinazoikabili Mamlaka hiyo, wameweza kusajili jumla ya wafanyabiashara wadogo yaani wamachinga 97,256 huku takribani  asilimia 80 ya wafanyabiashara wanatumia mashine za EFD