Monday, December 3, 2018

ABDULLAH AID, YAGAWA MSAADA WA VIFAA VYA MILIONI 50 VINGUNGUTI JIJINI DAR ES SALAAM.

 Mbunge wa jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam, Mussa Azzan Zungu (kushoto) Mwenyekiti wa Taasisi ya Adullah Aid Tanzania, Aref Yusuf (wa pili kushoto) Naibu Meya Manispaa ya Ilala, Omari Kumbi la moto (wa tatu kushoto, kwa pamoja wakimkabidhi Cherehani mmoja wa wanufaika wa msaada huo katika hafla iliyofanyika Ofisi za Abdullaah Aid Tanzania zilizopo Kiwalani Jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2018.
 
Mwenyekiti wa Taasisi ya  Adullah Aid Tanzania, Aref Yusuf akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa walengwa.
.........................................

Taasisi ya Abdullah Aid kwa kushirikiana na AL-IMDAAD FOUNDATION UK. ya nchini Uingereza imegawa vitu mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwa ni msaada kwa watu wenye uhitaji kwaajili ya kujikimu kimaisha.

Akizungumza na waandsihi wa Habari wakati wa kugawa vitu hivyo, Mwenyekiti wa Abdullah Aid Tanzania, Sheikh Aref Yusuf Abdurrahmaan amesema wamefikia uamuzi wa kutoa msaada wa vitu hivyo ili kusaidia watu wa hali za chini ambao sio rahisi kwao kupata vitu hivyo.

Sheikh Aref alisema vitu hivyo vilivyogaiwa kwa wahitaji ni pamoja na Mashine za  Popcorn 79, Baisakeli za walemavu 6, Pikipiki aina ya TVS 1, Bajaji aina TVS 1, Mashine za Cherehani 28, Mashine ya kumwagilia maji shambani 1, na Gari moja aina Cary, vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi milioni 50 ambavyo vimetolewa msaada kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Abdullah Aid Tanzania na Uingereza na Taasisi ya AL-IMDAAD FOUNDATION UK. ya nchini Uingereza.

Alisema wametoa msaada ambao utawanufaisha walengwa kwa muda mrefu ukilinganisha na fedha ambazo wakitumia zinaisha kwa muda mfupi bila ya kuwa na kumbukumbu.

Akitolea mfano, Sheikh Aref alisema vitu kama Cherehani, Mashine za Popcorn, Gari, Bajaji na pikipiki  vikitumika vizuri itakuwa sababu ya kujiongezea  kipato na kuweza kumudu gharama za maisha kwa mahitaji ya kila siku.

Aliongeza kuwa, utoaji wa vitu hivyo umetokana  na Mwenye kuwawezesha kufanya hivyo na kuongeza kuwa kadiri Mwenyezimungu atakavyowawezesha ndivyo watakavyoweza kufanikisha mahitaji mbalimbali kwa watu wenye uhitaji.

Aidha, ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wake Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutambua na kuthamini misaada mbalimbali inayotolewa na Taasisi hiyo hapa nchini huku akimpongeza mgeni rasmi katika hafla hiyo Mbunge wa Jimbo la Ilala Musa Azan Zungu kwa kukubali kufika katika ugawaji wa vitu hivyo.

Akizungumzia utaratibu unaotumika na Abdullah Aid katika kugawa misaada, Sheikh  Aref alisema Taasisi hiyo haibagui katika ugawaji wa misaada, bali inaangalia vitu walivyonavyo kwa wkati huo na kuhakikisha vinawafikia walengwa wenye uhitaji bila ya kujali dini zao.

Aliongeza kwa kusema kuwa, hiyo si mara ya kwanza kwa Taasisi hiyo kugawa misaada kwani imeshawahi kutoa misaada kwa waathirika wa mafuriko ambayo iliwafikia watanzania wote waliofikwa na madhara hayo bila ya kujali dini zao, rangi wala kabila.

Alifafanua kuwa, katika misaada inayotolewa kwa kuzingatia sheria ya uislamu ipo ile inayotolewa kama sadaka ambayo  hupewa mtu yeyote mwenye uhitaji hata kama sio muislamu, ama katika misaada inayotolewa kutokana na fungu la Zaka hii anaestahili kupwa ni muislamu tu kama maelekezo ya uislamu yanavyotaka ambapo katika hao waislamu pia wameainishwa makundi manane yanayostahili kupewa zaka.

Alisema jamii ya watanzania ina mahitaji ya vitu mbalimbali kutokana na Mwenyezimungu alivyoweka mgawanyo wa riziki hivyo wenye wanaostahili kusaidiwa wanapaswa kusaidiwa ili wapate wepesi wa sababu za kupata riziki.

Aliongeza kwa kusema kuwa, mpango huo ni katika kuunga mkono hujudi za serikali ya awamu ya tano ya kuwajali watu wanyonge na kwamba ndani ya uislamu kuna maelekezo maalum ya kusaidia jamii.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Abdullah Aid Uingereza, Shakir Majid amesema anashukuru kwa hatua hiyo waliyofikia ambayo Mwenyemungu amewawezesha kwa kushirikiana na Taasisi ya AL-IMDAAD FOUNDATION UK. ya nchini Uingereza kufanikisha misaada hiyo.

Alisema huo ni muendelezo na kwa uwezo wa Mwenyezimungu wanaweza kuendelea na mpango huo na kuwafikia watu wengi zaidi kupitia makundi yenye uhitaji.

Nae Kiongozi wa AL-IMDAAD FOUNDATION UK. ya nchini Uingereza Abduswamadu Mullah amesema kufatia ushirikiano walio nato na Abdullah Aid wataendelea kutoa misaada kwa Tanzania ili kusaidia watu wasiojiweza.

Alisema huo sio mwisho wa misaada yao kwa watu wasiojiweza Tanzania, bali wataendelea kuyafikia makundi tofauti na kusaidia mahitaji mbali mbali ya kijamii.

Akizungumza katika hafla hiyo, mgeni rasmi Mbunge wa Ilala Musa Azan Zungu alisema anaipongeza Taasisi ya Abdullah Aid kwa msaada huo na kwamba wamefanya kitu kinachohitajika katika jamii.

Alisema misaada kama hiyo ni muhimu kwani itasaidia kuwaongezea wananchi kipato na hatimae kuchangia katika maendeleo yao kwa kuwasomesha watoto wao na kuchangia katika pato la Taifa kwa ujumla.

Awali akimkaribisha Mbunge, Naibu meya wa Manispaa ya Ilala Omari Kumbi la moto alisema Taasisi ya Abdullah Aid ni Taasisi rafiki na manispaa ya Ilala kwakuwa imekuwa na msaada mkubwa katika matukio mbalimbali.

Alitumia nafasi hiyo kumpongeza Aref kwa kuijali manispaa ya Ilala na kufanya juhudi ya kuisadia serikali katika maswala ya kijamii.

Aidha, Naibu meya huyo wa Manispaa ya Ilala ambae ni Diwani wa kata ya Vingunguti alimuomba Mh. Mbunge kufikisha salamau kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwamba ndani ya Manispaa ya Ilala yupo mdau wa maendeleo anaejali maisha ya watu wa chini na kuchukua hatua ya kuwasaidia.

Alisema hakuna nguvu iliyotumika kumuomba misaada hiyo bali ni yeye mweneyewe kwa kuguswa kwake na maisha ya watu wa hali ya chini ameweza kutoa misaada hiyo ambayo itawasaidia wananchi wa kawaida katika kujiongezea kipato na kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Waliopata misaada hiyo ni makundi ya kina mama, kina baba, vijana, watu wenye ulemavu na wale wenye mahitaji maalum kwani vifaa hivyo itakuwa sababu ya  kuwawezesha kuinua vipato vyao katika maisha.

Wakizungumza mara baada ya kupokea misaada hiyo wananchi hao waliishukuru Taasisi ya Abdullah Aid kwa kushirikiana na AL-IMDAAD FOUNDATION UK. ya nchini Uingereza kwa misaada hiyo ambayo itawasaidia kujiongezea kipato.

Waliahidi kuitumia vyema misaada hiyo ambapo baadhi yao walisema itawasaidia kupata mahitaji ya kusomesha watoto na mahitaji ya kila siku.

Walitoa wito kwa Taasisi nyingine kuiga mfano Abdullah Aid kujitokeza na kufika mitaa ya watu wa hali ya chini ili kusaidia watu wanyonge kwa mahitaji mbalimbali.
 
 
 Mbunge wa jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam, Mussa Azzan Zungu (kushoto) akikabidhi Baiskeli za kutembela walemavu wa migugu, Msaada uliotolewa na Taasisi ya Abdullah Aid kwa kushirikiana na AL-IMDAAD FOUNDATION UK. ya nchini Uingereza.
  Mbunge wa jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam, Mussa Azzan Zungu akikabidhi mashine ya cherehani kwa walengwa wa msaada huo.
Mwenyekiti wa Abdullah Aid Uingereza, Shakir Majid (kulia) na
Kiongozi wa AL-IMDAAD FOUNDATION UK. ya nchini Uingereza Abduswamadu Mullah (kushoto) wakimsaidia mama moja miongoni mwa wanufaika wa msaada huo.

Naibu Meya Manispaa ya Ilala, Omari Kumbi la moto akimkabidhi Amiri Kisu funguo ya Gari yake ambayo inaonekana kwa nyuma hapo pichani.

Sunday, December 2, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI MKUBWA WA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA JIJI LA ARUSHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia maji yanayotoka katika moja ya visima virefu vilivyopo katika mradi huo mkubwa wa maji safi na usafi wa mazingira katika jiji la Arusha. Mradi huo utakapokamilika utaweza kuzalisha lita za ujazo milioni 200  kwa siku tofauti na sasa ambapo lita za ujazo ni 45 milioni wakati mahitaji ya jiji la Arusha ni lita za ujazo milioni 90.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Maji safi na usafi wa Mazingira katika jiji la Arusha. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Isaack Kamwelwe pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Alex Mubiru.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi mkubwa wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira utakaosaidia jiji la Arusha katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Kimyaki Arumeru mkoani Arusha.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Alex Mubiru wakati wa mkutano na wananchi wa Arumeru jijini Arusha mara baada ya kuzindua mradi huo wa maji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Arumeru mara baada ya kuweka  jiwe la msingi mradi wa Maji safi na usafi wa Mazingira katika jiji la Arusha.

Wananchi wa Arumeru wakishangilia wakati wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kijiji cha Kimnyaki Arumeru.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wakati akiondoka katika eneo la mkutano.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Meya wa jiji la Arusha Calist Lazaro mara baada ya kuwahutubia wananchi wa Arumeru. PICHA NA IKULU.

CCM PWANI YATOA AGIZO ZITO KWA WATENDAJI WAKE.

MNEC wa mkoa wa pwani (kushoto) akimsikiliza mwenyekiti wake katika kikao na watendaji wa CCM wilaya zote za mkoa wa Pwani.
......................................................

Na Shushu Joel, Kibaha.
MWENYEKITI wa ccm mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno amewaagiza watendaji wa chama hicho kuacha kufanya kazi kwa mazoe kama walivyokuwa wamezoea miaka ya nyuma.

Watendaji wa Ccm walio wengi wameshindwa kuendana na kasi ya awamu ya tano chini ya mwenyekiti wa taifa Dkt John Pombe Magufuli ambaye pia ni Rais wa Tanzania kwa watendaji wengi kufanya kazi za chama kipindi cjha chaguzi tu.

Akizungumza na watendaji wa mkoa huo mwenyekiti huyo aliwataka watendaji wote kuwajibika kwa wanachama wa chini katika kuwasaidia kutambua sitahiki zao kwani wanachama wa chini wamekuwa wakinyanyaswa na matajili huku viongozi wa chama wakiangalia tu na kushindwa kuwajibika katika kuwasaidia ili waweze kupata haki zao.

 “Watendaji wa chama wamekuwa wajijisahau katika uwajibika wao na kibaya zaidi wamekuwa ni watu wa kuagiza tu huku wakiwa wamekaa ofisini”Alisema

Aliongeza kuwa watendaji wa chama ndio mhimiri mkubwa katika chama hivyo ni lazima watendaji wote katika mkoa wahakikishe wanakuwa ni kiungo kikubwa kati ya uongozi na wanachama wea chini.

 Aidha amewataka watendaji kuwa wabunifu katika kipindi hiki kutokana na kuwa kipindi cha sasa ni kipindi cha siasa ni uchumi kwa kuwaelimisha wanachama juu ya umuhimu wa kuwa na vikundi vilivyosajiliwa katika vyombo husika ili waweze kukopesheka na kujijengea uchumi wao ambao utawatoa katika kipindi cha kuwa omba omba kwa watu.

Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa kupitia mkoa wa Pwani (NEC)Haji Jumaa amempongeza mwenyekiti huyo kwa kuona umuhimu wa kukutana na makatibu wote wa mkoa wa Pwani na kuwakumbusha wajibu wao katika utendaji.

Aliongeza kuwa watendaji wakisimama imara katika usimamizi wa mali za chama hali ya ccm itakuwa zaidi ya hapo ilipo sasa.

“Makatibu wanapaswa kuwajibika kwa bidii ili kuhakikisha chama chetu kinazidi kuwa bora kuanzia ngazi za mashina mpaka taifa na hii inawezekana pale kila mmoja atahakikisha anakuwa mkali kwa yule mwenye nia mbaya na chama katika kutumia mali za chama ovyo”Alisema Jumaa.

Aliongeza kuwa zoezi la kuwasajili wanachama wa ccm kwa njia ya kielectronic ni jema kwani liwaongeza mapato ya chama na kukifanya chama kuwa juu zaidi ya hapo kilipo sasa.

Naye katibu wa ccm wilaya ya Kibaha vijijini Janeth Mnyaga ameupongeza uongozi wa ccm mkoa kwa kuwakutanisha na kuwataka kuwajibika katika shughuli zao za usimamizi wa chama katika ngazi za wilaya.

Hivyo aliongeza kuwa elimu iliyotolewa leo kwa watendaji wote iwe endelevu kwani inawapatia motisha katika uwajibikaji na usimamizi wa chama katika ngazi za wilaya.

Makatibu wa CCM mkoa wa Pwani wakimsikiliza mwenyekiti wa mkoa huo akitoa maelezo juu yao.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno aliyesimama akitoa maelekezo kwa watendaji wa chama hicho.

DC BAGAMOYO AAGIZA KUKAMATWA MHASIBU MKUU NA WASAIDIZI WAKE WATATU HALMASHAURI YA CHALINZE KWA UBADHILIFU WA FEDHA.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Bi Zainabu Kawawa ameagiza watumishi wa idara ya fedha katika halmashauri ya wilaya ya Chalinze wanaoshughulika na ukusanyaji mapato wakamatwe na kupisha uchunguzi kufuatia hali ya ukusanyaji mapato katika halmashauri hiyo kuwa chini ya kiwango tarajiwa, agizo hili amelitoa leo katika kikao alipokuwa akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo.

Watumishi alioagiza wapishe uchunguzi ni Mweka Hazina wa halmashauri Bwana David Rubibira, na wahasibu watatu ambao ni Waziri Ally, Jumanne Sanga na Maneno Kwambwa

Mheshimiwa Kawawa alisikitishwa na ukusanyaji mapato katika halmashauri ya Chalinze kuwa chini ya malengo na kudai kuwa kuna mianya ya ubadhirifu wa mapato kwani mapato ya halmashauri yakikusanywa kwa umakini yanafikia milioni 920 kwa mwezi kwa chanzo cha madini ya kokoto nje ya vyanzo vingine kwa maana ya milioni 33 kwa siku.

Hivyo kutokana na makisio hayo Mkuu wa wilaya hana imani na mapato yanayokusanywa katika halmashauri hiyo ambayo ni wastani wa milioni 550 hadi 659 kwa mwezi.

Aidha baada ya kikao hicho Mheshimiwa kawawa alimtaka Mkuu wa polisi Chalinze kuwaweka chini ya ulinzi na kuwachukua kwa ajili ya uchunguzi na baada ya uchunguzi kukamilika hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao kwa kusababisha upotevu wa mapato.

"Nimekuwa nikifuatilia ukusanyaji mapato kuna mianya mingi ya utoroshaji mapato, tusitafutane wala kujaribiana kwa kuvujisha mapato tumepoteza Mapato sana kwenye makrasha kwa siku tuna uwezo wa kukusanya milioni 33 ,kwa mwezi tuna uwezo wa kukusanya zaidi ya milioni 900, badala ya kufuatilia na kukagua mnakaa tu ofisini katika hili hatuwezi kuvumiliana hata kidogo,Mkurugenzi nakuagiza watumishi wanaohusika na mapato wakae pembeni kwa hatua zaidi kuanzia leo na vyombo vya usalama vifanye kazi katika kuchunguza haya." Mheshimiwa Kawawa aliagiza.


Saturday, December 1, 2018

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI PAMOJA NA RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA WAFUNGUA KITUO CHA KUTOA HUDUMA KWA PAMOJA MPAKANI NAMANGA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakimwagia maji mti mara baada ya kuupanda wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakiwa wameshikana mkono wakati  wakimwagia maji mti mara baada ya kuupanda wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakipanda mti mara baada ya mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakipata maelezo ya kituo hicho cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na   Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakipungia wananchi mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano pembezoni mwa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na   Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakifurahi nyimbo zilizokuwa zikipigwa na bendi ya polisi katika hafla ya ufunguzi wa vituo hivyo vya mpakani.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi funguo Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea funguo kutoka kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.