Wednesday, July 12, 2017

WAZIRI WA UJENZI PROF. MBARAWA AKAGUA MRADI WA BARABARA ZA JUU TAZARA.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akipata maelezo juu ya maendeleo ya mradi huo.
 
Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd inayojenga barabara za juu eneo la Tazara, Kiyokazu Tsuji (kulia) akitoa maelekezo kewa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati) maendeleo ya daraja hilo wakati alipotembelea kuangalia maendeleo ya mradi huo. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida akishuhudia.
Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd inayojenga barabara za juu eneo la Tazara, Kiyokazu Tsuji (kulia) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati) muonekano wa ramani ya daraja hilo na ujenzi unavyoendelea wakati alipotembelea kuangalia maendeleo ya mradi huo. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida akishuhudia.
.............................

WAZIRI wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa leo amevamia mradi wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam na kuridhishwa na kasi ya ujenzi inayoendelea chini ya Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd ya nchini Japan. 

Akizungumza katika ziara hiyo alisema lengo ni kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ili kuhakikisha unakamilika mapema kama ulivyopangwa.

Prof. Mbarawa alisema ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo ambao mara baada ya kukamilika utarahisisha shughuli za usafiri kwa wananchi watumiao barabara hizo mbili za Nyerere na Mandela jijini Dar es Salaam.

Mradi huo wa ujenzi unatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2018 huku ukitarajiwa kugharimu takribani shilingi bilioni 100, ambapo kati ya fedha hizo shilingi bilioni 93.44 zitatolewa na Japan kupitia Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), na Serikali ya Tanzania itatoa shilingi Bilioni 8.3.
 
Muonekano wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.

RC NDIKILO AKAGUA KIWANDA CHA MAJI SAFI KIBAHA.

Image may contain: 3 people, people standing and indoor
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Everist Ndikilo leo tarehe 12.7.2017 ametembeea kiwanda cha Kiwanda cha Masasi Food Products Co Ltd kilichopo Lulanzi Halmashauri ya Mji Kibaha. 

Katika ziara hiyo mkuu wa mkoa Ndikilo amejionea Awamu ya Pili ya Upanuzi wa Kiwanda hicho ambacho kimepanuliwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita. 

Kiwanda hicho ambacho ni cha Maji safi na salama ya kunywa kimepata mkopo kutoka TIB, na ambapo kwa sasa Kimekamilisha ufungaji wa mitambo uliofanywa na wahandisi kutoka nchini China. 

Aidha, Kiwanda hicho Kimeshafanya majaribio ya awali ya kutengeneza maji na kuyafunga ndani ya chupa za ujazo mbalimbali na kupasishwa kwamba kiko tayari kwa uzalishaji. 

Kiwanda kitakuwa pia na uwezo wa kuzalisha maji na chupa za kwenye "water dispenser". 

Mkuu wa mkoa wa pwani Mhandisi Ndikilo alisema Kiwanda hicho  kimekamilika kwa asilimia 95, na kwamba Kinatarajiwa kuanza uzalishaji ndani ya kipindi cha miezi miwili ijayo.
 Image may contain: textImage may contain: 1 person, standing 
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Everist Ndikilo akikagua mitambo inayotumika kuzalisha maji katika kiwanda cha Masasi Food Products Co Ltd kilichopo Lulanzi Halmashauri ya Mji Kibaha.
No automatic alt text available.No automatic alt text available.Image may contain: 1 person, standing and indoor
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Everist Ndikilo akikagua mitambo inayotumika kuzalisha maji katika kiwanda cha Masasi Food Products Co Ltd kilichopo Lulanzi Halmashauri ya Mji Kibaha.

TaSUBa YAPATA BODI MPYA.

index
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe anapenda kuufahamisha umma kuwa wajumbe wa bodi ya ushauri wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) wamepatikana kulingana na taratibu za uteuzi wa bodi hiyo kumalizika.

Bodi inaundwa na watu kumi akiwemo Mwenyekiti, wajumbe watano wa kuteuliwa kwa umahiri wao na wajumbe wanne wanaotumikia bodi hii kutokana na nafasi zao kwa sasa.

1.   George Daniel Yambesi – Mwenyekiti wa Bodi
2.   Lilian Godfrey Kihiyo (Brave Law Associates) – Mjumbe
3.   Benson Sethiel Lyimo (TIB) – Mjumbe
4.   Marco Mkomwa Aidano (NBAA) – Mjumbe
5.   Arbogast Wenceslaus Kimasa (Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali) – Mjumbe
6.   Gasper Mapunda (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) – Mjumbe
7.   Herbert F. Makoye (Mtendaji Mkuu TaSUBa) – Mjumbe
8.   Leah Kihimbi (Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa) – Mjumbe
9.   Haji Mbaruku Kejo (Mwenyekiti Chama cha Wafanyakazi TaSUBa) – Mjumbe
10.  Isdory S. Moshi (Rais wa Serikali ya Wanafunzi  TaSUBa) – Mjumbe
Ili kulijenga taifa lenye kuendeleza na kuzingatia tamaduni zetu Mhe. Mwakyembe anawatakia wajumbe wote kila la kheri katika kutekeleza majukumu yao ndani ya bodi ya TaSUBa.

Uteuzi wa bodi ya ushauri wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ulianza tarehe 19 Juni, 2017. 
Imetolewa na:

Zawadi Msalla
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
12/07/2017

Monday, July 10, 2017

TAARIFA KUHUSU WATUMISHI WALIOKATA RUFAA UHALALI WA VYETI

taarifa kwa umma-uhakiki wa vyeti

ZOEZI LA KUOROZESHA KAYA KWA AJILI YA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI KUANZA KESHO

WAL4
Baadhi ya Wadadisi wakielekezwa namna ya kutumia ramani wakati wa kufanya mazoezi ya kuorozesha kaya kwa vitendo na Mtalaam wa Ramani Jumanne Msuya wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (katikati) kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai, 2017.
 ...........................

WADADISI wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 wameaswa kuzingatia maadili ya kazi wakati wa zoezi la kuorodhesha kaya linalotarajia kuanza kesho ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utafiti huo.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa wadadisi hao, Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu, Sylvia Meku kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesema ili kufanikisha zoezi la uorodheshaji wa kaya, ni lazima wadadisi hao wakazingatia maadili ya kazi pamoja na kufuata taratibu zote za Utumishi wa Umma.

“Ofisi ya Taifa ya Takwimu inawaagiza kwenda kwenye jamii kwa ajili ya kuorodhesha kaya zitakazofanyiwa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Natumaini mtatii na kuheshimu maadili ya Utumishi wa Umma ili muweze kufanikisha kazi hii kwa ufanisi,” amesema Slyvia Meku.

Amesema Zoezi la Uorodheshaji wa Kaya litafanyika mikoa yote ya Tanzania Bara kwa takribani siku 15 kuanzia kesho Julai 11, 2017 na baadae kufuatiwa na utafiti wenyewe unaotarajia kuanza mwezi Desemba, 2017.

Sylvia Meku amesema utafiti huu unafanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango na baadhi ya Wadau wa Maendeleo kwa lengo la kuangalia kiwango cha umasikini nchini.