Saturday, June 24, 2017

MUFTI ZUBERI AWASILI MKOANI KILIMANJARO KWA AJILI YA SWALA YA EID EL FITRI.

Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery akisalimiana na waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kuwasili katika ofisi za Bakwata wilaya ya Hai
 
Mufti wa Tanzania ,Abubakary Zubery akitia saini katika kitabu cha ageni mara baada ya kufungua rasmi ofisi za BAKWATA wilaya ya Hai.
Msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai
Msafara wa Mufti ukitoka katika uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) .
 
Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery akifungua kitambaa katika jiwe la Msini kuashiria kuendelea kwa ujenzi wa jengo hilo litakalo tumika kama Madrasa


WAFANYAO FUJO BAGAMOYO SIKU YA EIDI KUSHUGHULIKIWA.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga amewaonya wale wote watakaofanya fujo siku ya siku kuu katika mji wa Bagamoyo.
Akizungumza nyumbani kwake mara baada ya kufuturisha, Alhaj Majid alisema skiku kuu ya Eidi ni siku kuu ya kidini na kwamba tayari uislamu u meshatoa maelekezo juu ya kusherehekea siku kuu hiyo.
Alisema kumekuwa na tabia siku za siku kuu  katika mji wa Bagamoyo kuja vijana kutoka nje ya  Bagamoyo kufanya  fujo na hivyo kusababisha uharibifu wa mali na uvunjifu wa amani na  kusisitiza kuwa vitendo hivyo havitavumiliwa.
Mkuu huyo wa wilaya ambae pia ni Mwenyekiti  wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya, alisema ulinzi umeimarishwa katika maeneo yote ya wilaya ya Bagamoyo hasa katika  fukwe za Bahari ambapo makundi ya wageni yamekuwa yakifika  huko na kufanya fujo.
Alichukua nafasi hiyo kumuagiza mkuu wa Polisi wilaya ya Bagamoyo, kuhakikisha wale wote watakaohusika na vurugu siku ya Eidi wana chukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo viovu   vya uvunjifu wa amani katika siku za siku kuu.
Aidha, Mkuu huyo wa wilaya amepiga marufuku Disco toto ndani ya wilaya ya Bagamoyo katika kipindi  chote cha siku kuu nakuwataka wazazi kuwa na karibu na watoto wao ili kuwaepusha na madhara  yanayotokana na burudani ambazo zipo juu ya umri wao.
Aliwataka wazazi kuhakikisha watoto wanatembea maeneo salama na kurudi nyumbani mapema.
MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO ANAWATAKIA WANANCHI WOTE NDANI YA WILAYA YAKE SIKU KUU NJEMA YA EID EL FITRI.

ATAKAE ZEMBEA NA RBF KUKIONA- WAZIRI JAFO.

1
Serikali imesema haita wavumilia watendaji watakaoshindwa kusimamia ipasavyo mradi wa  Malipo kwa Ufanisi katika kuboresha utoaji wa huduma za Afya “Results Based  Finance” (RBF) ambao hivi sasa unatekelezwa katika mikoa minane hapa nchini.

Akifungua kikao kinacho wakutanisha  Makatibu Tawala wa Mikoa, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Maafisa Mipango kutoka mikoa inayotekeleza mradi wa RBF, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Seleman Jafo, amesema ni lazima kufanyike mabadiliko katika utoaji wa huduma za afya kuleta matokeo tarajiwa.

Naibu Waziri Jafo ametawataka Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri  kuhakikisha kuwa utekelezaji wa Mradi wa RBF unakuwa ni ajenda ya kudumu katika vikao vinavyofanyika kila mwezi ili kuwezesha kujua kiasi cha fedha zilizoletwa kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi huo ili kuweza kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo, ameiomba Benki ya Dunia ambayo ndiyo mfadhili wa mradi wa RBF kuangalia uwezekano wa kuwezesha utekelezaji wa Mradi wa huu kufanyika nchi nzima ili kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini kote.

Naye Mwakilishi  wa Benki ya Dunia Bibi Gayle Martine ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa hatua ambazo inazichukua katika kuhimiza suala zima la uwajibikaji  na kusema kuwa hali hiyo imeongeza shauku ya Wadau wa Maendeleo kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika kuleta mabadiliko ya kiutendaji na utoaji wa huduma za jamii.

Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Zainab Chaula amesema ili kufikia malengo chanya yanayotarajiwa  katika uboreshaji wa utoaji wa huduma za Afya kila mmoja katika eneo lake inabidi kutengeneza mpango kazi ambao ndio utakuwa dira ya utendaji kazi ili kuleta matokeo chanya.

Mradi wa Malipo kwa Ufanisi katika Kuboresha Huduma za Afya nchini Ulianza mwaka 2015  katika mkoa wa Shinyanga kama eneo la majaribio  ambapo hadi hivi sasa unatekelezwa katika mikoa nane ambazo ni Mwanza, Shinyanga, Pwani, Simiyu, Geita, Kigoma, Tabora na Kagera

Friday, June 23, 2017

RIDHIWANI KIKWETE APONGEZWA NA RAIS MAGUFULI.

RIU1 
Rais Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuwasili Jimbo la Chalinze wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu iliyomalizika jana  mkoani Pwani 
 1 
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akihutubia wakati wa ziara ya Rais Dk. John Pombe Magufuli katika jimbo la Chalinze mkoani Pwani jana.
RIU1  
Rais Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu iliyomalizika jana  mkoani Pwani jana
 RIU2 
Rais Dk. John Pombe Magufuli na Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete pamoja na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza juisi ya Sayona katika jimbo la Chalinze mkoani Pwani jana.
...................
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John  Magufuli , amempongeza  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete kwa kupiga hatua katika kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo lake.

Rais M agufuli ametoa Pongezi hizo alipokuwa katika ziara ya kikazi mkoani Pwani  na kutembelea Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo
Ziara hiyo ya Raisi ambayo ilikuwa na kazi ya Kufungua Miradi ilianza na ufunguzi wa Kiwanda kikubwa cha matunda cha Sayona kilichopo Mboga Wilaya ya Chalinze. 
Pamoja na kumkaribisha Mheshimiwa Mbunge alimuhakikishia Mheshimiwa Raisi juu ya KUMUUNGA mkono katika hatua anazochukua ikiwemo kupambana na Ufisadi na kuwahakikishoa Watanzania kutawala Uchumi wao. Mheshimiwa Mbunge alimueleza juu ya jitihada ambazo Wana chalinze wanazifanya kujikomboa katika Uchumi tegemezi.
Mheshimiwa Mbunge alimueleza Mh. Raisi jinsi Halmashauri yao ilivyofanikiwa kukusanya fedha kwa kuvuka kiwango cha makusanyo. " Mh. Raisi halmashauri yako hii ya Chalinze imefanikiwa kukusanya zaidi ya Asilimia 102 juu ya makadirio mbayo tulikuwa tumejipangia. 
Fedha hizi zitapelekwa katika miradi ambayo inagusa wananchi wa chini kabisa ikiwemo kuimarisha huduma za afya, maendeleo ya jamii, mikopo kwa wakina mama na vijana na pia miradi ya maji kwa ajili ya kupunguza makali.
"Mh. Raisi , tumejipanga pia kuhakikisha kuwa halmashauri yetu inajiwezesha yenyewe. Zaidi ya Milioni 200 zimepelekwa kuwasaidia wananchi maskini kimikopo na shughuli za maendeleo kwa ushirikiana na wadau wa maendeleo tumefanikiwa katika haya." Mbunge alieleza.
Pia mbunge alimuomba Mh. Raisi kutumia Chalinze kama sehemu ya ushuhuda wa hatua na jitihada anazochukua kukuza uchumi wa watu na maendeleo ya kweli yanayotazama uelekeo wa kiilani na ahadi zake. 
Mheshimiwa Mbunge alimueleza Mheshimiwa Raisi kuwa ," kama yupo mtu ambaye ana shaka na utayari wako na uchapakazi wako juu ya sera ya viwanda basi Mwambie aje Chalinze aje kuona jinsi mambo yanavyofanyika." Tunajua wewe ni kazi tu na sisi hapa chalinze ni kazi tu. "
Mheshimiwa Raisi alimshukuru Mbunge na kwa hakika alimpongeza kwa kumfananisha na Baba yake Aliyewahi kuwa Raisi Wa Jamhuri ya Tanzania wakati wa awamu ya Nne. Mheshimiwa Raisi alimfananisha na Nyoka mtoto. "Kwa hakika nimemsikia Mbunge wenu na nimeridhika kuwa Nyoka uzaa Nyoka".Nimekuona na ninakupongez unavyochapa kazi. Hongera sana ."
Pamoja na kumshukuru mbunge , Mheshimiwa Raisi aliwakabidhi Halmashauri ya Chalinze majengo ambayo yalitumiwa na Mkandarasi pale Msata wakati wa Ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia-Masata.
Baada ya kumaliza mkutano huo na kufungua kiwanda cha kuchakata Matunda cha Sayona, Mheshimiwa Raisi alielekea katika Halmashauri ya Bagamoyo ambako alifanya mambo mawili makubwa ikiwemo uzinduZi wa Barabara ya Bagamoyo Msata na Kiwanda cha kukausha Matunda kilichopo Mapinga, Bagamoyo.

MAGAZETI YA LEO TAREHE 23, JUNI 2017.

Thursday, June 22, 2017

WANAOPATA MIMBA SHULENI MARUFUKU KUENDELEA NA MASOMO: JPM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amepiga marufuku  wanafunzi wa kike watakaopata mimba shuleni kuendelea na masomo ya shule ya  msingi na Sekondari.

Rais Magufuli aliyasema hayo leo Juni 22, 2 017 Wilayani Bagamoyo alipokuwa akihutubia wananchi katika ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo- Msata yenye urefu wa kilomita 64 kiwango cha lami.

Alisema yapo maneno yanayosemwa mitaani  kwamba mwanafunzi akipata mimba shuleni anaruhusiwa  kuendelea na masomo baada ya ku jifungua.
 Mh. Rais alifafanua kuwa maneno hayo s i y akweli na kwamba hayo  nimaneno ya mashirika yasiyo ya kiserikali  ambayo yanajaribu kutetea  hata  kuporomoka kwa maadili.

Alisema haiwezekani kuruhusu mwenye mtoto arudi  shuleni kuendelea na masomo huku ananyonyesha, wakati wapo watoto  wanaotaka nafasi  hizo za kusoma.